James Mathenge Kanini Kega

Parties & Coalitions

Born

31st October 1972

Email

mathenge@poweroptionsltd.com

Telephone

0733491066

Telephone

0710107939

All parliamentary appearances

Entries 891 to 900 of 959.

  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Asante Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili niafiki Hoja hii ambayo imeletwa na rafiki yangu, Mheshimiwa wa Nyali, Mohamed Ali, ambaye tunamjua sana kwa jina “Jicho Pevu”. Tunafurahia kwa sababu Hoja ambayo amewasilisha hapa ni muhimu sana, na yale aliyoyaangazia ni mambo ambayo yanaathiri watu wetu kila uchao. Lakini wakati Mhe. Ali jana alipokuwa anatoa Hoja hii, angetoa ilani kwa Wabunge kwamba leo tutakuwa tunaongea kwa Kiswahili ndiyo watu waweze kubeba kamusi. Nimeona sana wakati Mheshimiwa alikuwa anaendeleza Hoja hii, wengi walikuwa wameachwa vinywa wazi. Hawakuwa wanaelewa, hasa sisi ambao tumetoka bara. Lakini nitajaribu nione ... view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: kila mwaka kutoka vyuo vikuu. Lakini wakihitimu hawakai humu nchini. Wanahamia nchi za kigeni.Wanahamia nchi jirani na wengine nchi za Ulaya kwa sababu wanapata lishe bora huko. view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Mhe.Naibu Spika wa Muda, naomba sisi kamaWabunge lazima tufanye kazi yetu sawasawa na tuhakikishe kwamba waliotuchagua, walituchagua tuwashughulikie kiafya, ajira na mengine. Mhe. Mohamed Ali alisema hospitali za rufaa ni muhimu sana. Tuko na mbili, moja hapa Nairobi na ingine kule Eldoret. Tukiangazia maeneo ya uwakilishi Bunge, hasa nikitoa eneo langu la Bunge kama mfano, hatuna hospitali ya kiwango cha 4, hata hospitali ya kiwango cha 5. Tuko na zahanati peke yake. Wagonjwa kutoka eneo langu la uwakilishi Bunge wanasafirishwa zaidi ya kilomita 200 ili wapate huduma za afya. Lazima tuimarishe zahanati tulizonazo kule mashinani ili zile za kiwango cha ... view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Hili si jambo la mzaha. Ni jambo tunapasa kuangazia sisi sote pamoja na magavana. Naomba ya kwamba Hoja kama hii iwasilishwe katika gatuzi zote za taifa hili. Ni jukumu la serikali yoyote kuhakikisha kwamba wananchi wake wote wako na afya njema. Uzima wa kimwili ni jukumu la ugatuzi. Tukiwa na hospitali ya kiwango cha 6 katika kila gatuzi... Hospitali ya Rufaaa Kenyatta imekuwa na changamoto juzi. Wakati mwingine huwezi kulaumu madaktari kwa sababu kila siku wanafanya oparesheni nyingi kwa sababu wagojwa ni wengi na hatuna hospitali za kutosha. Tukiwa na hospitali za kiwango cha 6 kule Homa Bay, Nyeri ama ... view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Sitaki kupitisha hapo. Kama Wabunge tuko na bahati maanake tuko na bima ya afya. Inatushughulikia kwa kutuwezesha kuenda kutibiwa kule ng’ambo. Lakini walalahoi wa kule mashinani wakigojeka ama wakipata magojwa ambayo hayawezi kutibiwa humu nchini, watafanya nini? view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Naiafiki Hoja hii. Haitakuwa Hoja tu, tutahakikisha imetimizwa na Serikali ya Kitaifa na pia serikali gatuzi. view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Kwa hayo machache, naomba niketi. Asante sana. view
  • 7 Nov 2017 in National Assembly: Ahsante sana, Mhe. Spika kwa kunipa nafasi hii ili niomboleze na familia ya mwendazake Gavana wetu wa Nyeri. Kwa niaba yangu, familia na wale ninaowaakilisha katika eneo Bunge la Kieni, ninatoa rambirambi zangu kwa familia, jamaa na marafiki wa mwendazake gavana wetu. Alfajiri ya leo, tulipata habari ya kwamba Gavana wetu alihusika katika ajali ya barabara ambayo tulifikiri ni ajali tu ya kawaida. Na muda si muda, tukaambiwa ametuacha. Ni pigo kubwa kwa watu wa Nyeri tukiangazia kwamba marehemu Mhe. Gachagua, ambaye alikuwa gavana wa kwanza, alituacha miezi tisa iliyopita. Kwa hivyo, ni wingu kubwa la simanzi ambalo liko katika ... view
  • 7 Nov 2017 in National Assembly: Ninatoa risala zangu za rambirambi kwa familia na marafiki wa marehemu, na kwa watu wote wa Nyeri kwa sababu Waswahili wanasema akufaae wakati wa dhiki ndiye rafiki. Nimuomba Mwenyezi Mungu aifariji familia ya marehemu, na aiweke roho yake katika mahali pema peponi. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus