7 Nov 2017 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Spika. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
27 Sep 2017 in National Assembly:
Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili nichangie mjadala ambao uko mbele yetu, ambao ni kuangazia kalenda ya muhula huu. Kabla sijachangia, naomba unikubalie kwanza nikupe heko kwa kuchaguliwa katika muhula wa pili na pia kuchaguliwa katika kamati itakayosimamia vikao vyetu. Nilikuwa nataka kuchangia Hoja ambayo ilikuwa hapo mbele, ambapo tulikuwa tunaangazia wale ambao wataketi katika kamati hiyo. Pia, niseme kwamba wote ambao wamechaguliwa, ninawajua. Ni watu ambao wako na tajriba ya hali ya juu, uzoefu na watatupeleka mbele katika mijadala yote ambayo tutakuwa tukichangia hapa. Hii ni nafasi yangu ya kwanza kuongea katika Bunge la ...
view
27 Sep 2017 in National Assembly:
katika kiti ambacho umekalia na kwa sasa hivi, yeye ndiye Naibu Spika. Hata mimi naona siku moja, kwa majaaliwa, utakuwa Spika wa Bunge hili. Pili, muhula uliopita nilisema kwamba muhula huu nitajaribu sana niwe nikiongea katika lugha ya Kiswahili, lugha tunayoienzi. Wakati mwingine nikiangalia ama nikitazama mijadala kwenye Bunge la marafiki wetu wa Tanzania, mara nyingi wanatupa changamoto. Kwa nini sisi pia tusiwe na siku kando ambayo ni ya kujadili kwa lugha inayoeleweka na wananchi wale waliotupa kura? Wengi wetu hapa walipokuwa wakiomba kura walitumia lugha ya Kiswahili na ya mama. Ni wachache sana kwa wale wamechaguliwa katika Bunge hili ...
view
16 Nov 2016 in National Assembly:
Asante, Mhe. Spika. Ningependa kuungana na Waheshimiwa wenzangu ili nitoe risala za rambi rambi kwa jamaa na marafiki wa Mhe. Paul Otuoma ambaye tunafanya kazi naye katika Kamati ya Ardhi. Tulipokea habari hizo katika Kamati kwa mshangao mkubwa kwa sababu kijana wake amekua rafiki wa karibu wa Kamati yetu. Wakati tulikuwa tukitembea hapa na pale, alikuwa anakuja kutusalimia. Kwa hivyo, hili ni jambo ambalo linashtua sana. Wazazi wote wangependa watoto wao waje kwa mazishi yao. Hakuna hata mzazi mmoja ambaye angependa kumzika mtoto wake. Kwa hivyo, tunajua ni pigo kubwa lakini tunamuombea Mola, tunaiombea familia yake, and wale watu wa ...
view
16 Nov 2016 in National Assembly:
Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi.
view
4 Aug 2016 in National Assembly:
Asante, Mhe. Spika kwa kunipa nafasi kuchangia Hoja hii ya Mhe. Midiwo. Kwa hisani yako, ningependa kutoa risala za rambirambi kwa jamaa na marafiki wa aliyekuwa Mheshimiwa wa Nakuru Mjini, Mhe. Mark Mwithaga, aliyeaga dunia. Ningependa kufariji familia yake na ninaaomba Mungu awafariji. Hoja hii iliyoletwa na Mhe. Jakoyo Midiwo ni ya maana sana. Ukipekua magazeti matatu ya kitaifa leo, katika kurasa tano za mwisho, utapata yanawaelezea Wakenya vile watavyokuwa matajiri siku moja na kutoka kwa ufukara. Nimeangalia mambo haya na nimeona kuwa tumepoteza mwelekeo. Mataifa yanastawi kwa sababu watu wanafanya kazi. Tukiambia wananchi kwamba kuna utajiri bila kufanya kazi, ...
view
4 Aug 2016 in National Assembly:
Asante Mhe. Spika. Ningetaka kusema kuwa wanaoshiriki katika kamari sana sana ni watu wa mapato ya chini sana. Tunafaa kuweke sheria zitakazodhibiti hali hii. Wakati huu, tumeona ukora. Kuna watu ambao wanafanya biashara halali, lakini kuna wengine ambao ni tapeli. Kuna kampuni zaidi ya 20 ambazo zinafanya kazi hii. Yangu ni kusema kuwa Kamati hii iundwe mara moja na ipewe muda, hata kama ni siku 30, ili izunguke taifa hili. Hata ikiwezekana watembea katika mataifa ambayo yamekuwa na biashara hii ya kamari ili waone vile inavyofanywa ili Wakenya wasitapeliwe na wanaofanya biashara hii. The electronic version of the Official Hansard ...
view
4 Aug 2016 in National Assembly:
Kwa hayo mengi, ninaunga mkono Hoja hii. Ninaomba Bunge hili litunge sheria na tufanye hima ili tulete sheria ambayo itawakinga Wakenya kutokana na matapeli ambao wanawachukulia Wakenya kiholela.
view
30 Mar 2016 in National Assembly:
Thank you, Hon. Temporary Deputy Speaker for this opportunity. I rise to support the Motion. I thank my colleague, Hon. Wanyonyi, for bringing it to the House. Allow me to quote Abraham Lincoln, the former President of the United States (US), when he talked about elections. He said:- “Elections belong to the people. It is their decision. If they decide to turn their back on the fire and burn their behind, then they will just have to sit on their blisters. Get out and register and be ready to vote because bad leaders are elected by good people who do ...
view
1 Mar 2016 in National Assembly:
Thank you, Hon. Speaker. This is a public Petition by the residents of Kieni Constituency on Solio Ranch Land Dispute. I, the undersigned, on behalf of residents of Kieni Constituency draw the attention of the House to the following:- THAT, the Government of Kenya acquired 15,000 acres out of Solio Ranch for settlement of squatters in the year 2008; THAT, on account of alleged interference in the acquisition process by powerful politicians and Government officials, 6,000 of the 15,000 acres were allocated to a single person leaving only 9,000 acres for the intended settlement; THAT, during the profiling of settlement ...
view