22 May 2020 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Siku ya leo itabaki katika kumbukumbu. Nimesikiza kwa mapana na marefu. Nimesikiza Hoja yenyewe na tuhuma zilozoletwa kumhusu Naibu wa Spika na kuziweka mizani. Kwenye mizani nimeweka tuhuma pamoja na utenda kazi wake. Ukweli usemwe kwa sababu Mswahili husema mghala muue na haki mpe. Ukiweka katika mizani kazi aliyofanya, inaonekana ni kazi ambayo sisi wenyewe--- Napinga Hoja hii leo, kesho na hata milele. Huo ndio ukweli na ukweli unapaswa kusemwa. Yeye aliongoza hapa akiwa amekalia kiti hicho na ameleta tabasamu badala ya mgawanyiko katika hii Seneti yetu. Sisi wenyewe badala ya kumpa "kongowea"-- ...
view
22 May 2020 in Senate:
Bw. Spika, ninakubaliana naye mia kwa mia, kwa sababu baada ya kusema vile Naibu wa Spika ametenda kazi kwa ueledi, amesema kuwa anaunga mkono Hoja ya kumtimua. Itakuwaje unasema mtu amefanya kazi nzuri na badala ya kumpa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
22 May 2020 in Senate:
heko, unasema unamtimua. Huko ndiko ninasema ni kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa, na yeye mwenyewe lazima ajue Kiswahili. Kwa Sen. Sakaja, nitakuwa nimekosea kuja hapa kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili ambayo yeye haielewi wala haimanyi. Mimi sina uwezo wa kumsaidia bali ninamwambia sisi tunazungumza kwa lugha ambayo wenzangu wa kutoka pengine Pwani wanaifahamu. Ningependa kumwambia Naibu wa Spika, Sen. (Prof.) Kindiki, kwamba Biblia yangu inaniambia hata ijapokuwa unapitia katika bonde la mauti, usiogope kwa sababu Mwenyezi Mungu yuko pamoja nawe. Vile vile napenda nikwambie kwamba kama vile Yesu alivyokuwa amebebeshwa msalaba, kwa sababu naona ndugu yangu unaelekezwa Golgotha, naona ...
view
19 May 2020 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Nataka kuungana na wenzangu kupongeza uamuzi wako ambao ni wa busara. Hii kwa sababu janga la COVID-19 liko nasi na ni lazima tukubali kukumbatia teknolojia. Teknolojia ndio itatusaidia wakati huu mguu wa kuendelea na maisha yetu. Nimemsikiliza Sen. Mutula Kilonzo Jnr. akisema kwamba ni vizuri tutafute sehemu ambayo Maseneta wote wanaweza kutoshea. Nilimsikiliza kwa makini nikaona ni kama anaongea mambo mawili kwa wakati mmoja. Alisema kwamba tukumbatie teknolojia na pia tutafute sehemu ambayo Maseneta wote wanaweza kutoshea. Ni vizuri kukumbatia teknolojia kwa sababu tuko na ujuzi na vyombo ambavyo vinahitajika. Ni vizuri ...
view
19 May 2020 in Senate:
Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Kwanza, Taarifa hii ya Sen. (Dr.) Mwaura ni uwaledi mwingi. Heko kwake kwa kuileta katika Seneti. Serikali kuu imejaribu kiasi cha haja kwa sababu kuna ushuru fulani unaotozwa, tayari wameuondoa. Lakini ukiangalia katika kaunti zetu, utaona watu wanaouza vitu rejareja kama nyanya, nguo za mitumba na bidhaa nyingi barabarani, hao wanaendelea kutozwa ushuru wa kiwango cha Kshs50 au Kshs100. Wakati huu kuna janga la COVID-19 na kupata mnunuzi wa bidhaa si rahisi. Wanapata wateja kati ya 6.00 p.m. hadi 8.00 p.m . Curfew imewaathiri sana. Kwa hivyo, wanauza kwa muda ...
view
19 May 2020 in Senate:
mama na watu wengi wanaofanya biasahara za rejareja mithili ya watu walioiba. Wangewapa afueni wasilipe ushuru huo wakati huu wa ugonjwa COVID-19. Ikiwa hawa wauzaji rejareja hawatakufa na ugonjwa huu wa COVID-19, basi watakufaa njaa. Hii ni kwa sababu watu hawa hawana pesa za kununua chakula. Ningependa kuwaomba magavana wa kaunti zetu na wale wengine wanaohusika, waangalie watu wetu wakati huu. Angalau waondoe ushuru huo wa Kshs50 au Kshs100. Ushuru huo unatozwa wanaofanya biashara za rejareja kama ile ya kinyozi, wanaouza nyanya, mboga na nguo wakitembeza hapa na pale. Watu hawa ndio wanagandamizwa zaidi. Watu hawa hufanya biashara zao kwa ...
view
21 Apr 2020 in Senate:
Asante sana Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Ninampongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Afya kwa taarifa hii nzuri. Kwanza kabisa, jambo la kuwazuia wagonjwa katika hospitali limekuwa mazoea. Ukiangalia malipo yanayotozwa hospitalini baada ya yule mgonjwa anapokufa, unapata kwamba ni hela ambazo kwa ukweli hazina maana yoyote. Kwa mfano, sindano inayouzwa kwa Kshs3 unapata inauzwa kwa Kshs300 ili ada ya hospitali iwe kubwa hadi anashindwa kulipa. Ikiwa mgonjwa amekufa, ada ambayo familia yake inatozwa inaongezeka marudufu. Unashindwa hii ni nchi gani. Jambo lingine ambalo lina nishtua zaidi ni kwamba Mwenyekiti hangekuja kusema anataka taarifa yenyewe. Mwenyekiti angekuja katika Bunge hili ...
view
21 Apr 2020 in Senate:
Bw. Spika, ninataka kuwashukuru Maseneta wenzangu. Pengine kwa sababu ninatumia lugha ya Kiswahili inawachanganya kidogo.
view
21 Apr 2020 in Senate:
Nilianza kwa kusema kwamba, nampongeza Mwenyekiti wangu kwa kuwasilisha taarifa nzuri sana katika Bunge hili la Seneti. Nina uhakika kwamba wenzangu hawakunielewa kwa sababu nilitumia lugha ya Kiswahili. Wakati mwingine nitatumia lugha ya Kiingereza kwa sababu wamebobea kwa lugha hiyo sana. Bw. Spika, ninasema kwamba, tabia ya hospitali kuwazuilia wagonjwa kwa sababu ya kutolipa ada ya hospitali haikubaliki. Jambo ambalo nilikuwa na shida nalo ni kwamba Mwenyekiti wangu angekuja katika Bunge la Seneti na kutueleza hatua ambazo Kamati yake imechukua kutatua tatizo hilo. Sikusema ni makosa yoyote. Nimesema kwamba, ninampongeza kwa taarifa hiyo. Pengine ningeongea kwa lugha ya Kiingereza, Sen. ...
view