27 Mar 2025 in Senate:
Kuna uchunguzi na mapendekezo mengi tuliyofanya katika hii ripoti lakini tulikuwa na muda mchache sana kama vile Bw. Mwenyekiti alivyosema. Ninashukuru wafanyikazi wa Seneti kwa kujitoa mhanga, kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha ya kwamba hii ripoti ya zaidi kurasa 2,000 imeletwa leo bila kupitisha ule muda uliowekwa katika katika Kifungu cha 229.
view
27 Mar 2025 in Senate:
Katika uchunguzi wetu, tumeona ya kwamba kaunti nyingi zinatumia pesa lakini stakabadhi za kuonyesha kwamba zile fedha zimetumika kwa mujibu wa sheria haziko. Kwa mfano, mwanakandarasi amepewa sabuni ya kuleta stakabadhi za kulipwa kama vile invoices lakini amelipwa bila kuwepo kwa zile stakabadhi. Tuko na mapendekezo ya kufuatilia na ndio sababu Bw. Mwenyekiti akasema muda ulikuwa mchache. Kwa hivyo, lazima kuwe na muda zaidi wa kufuatilia ile miradi iliyofanywa katika gatuzi ili kuhakikisha hiyo miradi imefanyika na kwamba wananchi wanapata thamani ya pesa kwa lugha ya kimombo, value for money.
view
27 Mar 2025 in Senate:
Tumejiuliza kama kamati itakuwaje mmelipa pesa lakini wakati Mhasibu Mkuu wa pesa ya umma anapokuja kwa kaunti kukagua, hizo nakala zimepotea. Kuna gatuzi nyingi kama vile Bw. Mwenyekiti alivyosema ambazo hazina kamati za ukaguzi ama audit committees. Ukaguzi wa kwanza ni jukumu la kamati za uhasibu za kaunti tunazoziita internal audit. Zinafanya ukaguzi na yule Mhasibu Mkuu anapokuja kukagua, anategemea sana ile ripoti ya kamati ya uhasibu ya kaunti. Lakini kaunti nyingi zimekataa kuwa na hizo kamati kwa sababu kuna mambo wanayoficha huko ndani.
view
27 Mar 2025 in Senate:
Sitaki kuongea sana kwa sababu mimi naunga tu mkono hii Hoja. Lakini Mwenyekiti ameongea kuhusu suala la madeni au malimbikizi ya madeni ya kaunti ama pending bills ambazo zimelemaza maendeleo katika kaunti. Yale madeni yanatakikana kulipwa na tukisoma hii ripoti imependekeza ya kwamba taasisi za uchunguzi kama vile DCI na EACC wafanye uchunguzi ili kuona kama yale madeni yalilimbikizwa kihalali. Na kama kuna yale ya kikora, basi hao washukiwa wachukuliwe hatua.
view
27 Mar 2025 in Senate:
Kwa sababu Maseneta wanaotaka kuongea ni wengi, sisi kwa ufupi kabisa tunaiomba hii Seneti itupatie fursa tutembelee gatuzi zetu, tuone ile miradi inayosemekana imefanywa, kama imefanywa sawa sawa na kama kuna thamani ya pesa kutokana na pesa ambazo zinatoka kwa ushuru wa mwananchi.
view
27 Mar 2025 in Senate:
Serikali haina pesa. Pesa zozote zinazoenda kwa gatuzi zetu zinatokana na ushuru wa mwananchi. Kwa hivyo, sisi wote kama wananchi wa Kenya lazima tufungue macho ili tukiona pesa zinatumika vibaya tuweze kuripoti kwa asasi za uchunguzi. Lazima tuumwe na zile pesa zinazoenda kwa gatuzi zetu.
view
27 Mar 2025 in Senate:
Nikimalizia kabisa, asubuhi sikupata fursa ya kuongea kuhusu ule Mswada ambao tuko nao hapa leo wa County Additional Allocations Bill ambao umechelewa kwa muda wa miezi nane. Bunge la Kitaifa wanasema ya kwamba hawataki pesa za barabara ziende The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view
27 Mar 2025 in Senate:
kwa gatuzi zetu kwa sababu pesa ikienda huko inaenda kutumika vibaya. Nani hajui ya kwamba ufisadi mwingi uko katika maeneo bunge. Waheshimiwa wengi Wabunge wanafanya tender zao wenyewe. Nilikuwa mahali nikiongea na wananchi katika hadhara na mambo yangu ya uangalizi. Wananchi wanauliza inawezekanaje mheshimiwa siku hizi barabara zikitengenezwa zikiwekwa simiti zinakaa mwaka mmoja na kuharibika. Zamani barabara zilikuwa zinatengenezwa na kukaa kama miaka kumi na tano. Nikawaambia ni kwa sababu ya ufisadi na ulafi wa Wabunge. Wale Wabunge wanafanya tender zao wenyewe. Na kama hawajafanya tender zao wenyewe, ule ufisadi wa kuitisha hongo unakuwa mwingi sana. Sasa kama mwanakandarasi atakupatia ...
view
27 Mar 2025 in Senate:
Kwa hivyo, sisi sote tukubali kwamba ufisadi uko katika gatuzi zetu. Ni jambo la kuhuzunisha kwamba huu sio ule ugatuzi tuliolilia na kupitisha mwaka wa 2010; wa kupeleka pesa mashinani. Sisi ambao tunatoka katika eneo zilizo na idadi ndogo ya watu hatukuwa tunapata maendeleo kwa sababu tulikuwa tunaulizwa tunaleta kura ngapi katika meza ili watupatie maendeleo.
view
27 Mar 2025 in Senate:
Lakini leo pesa nyingi zinafika mashinani kwa sababu ya mfumo wa ugatuzi. Magavana, Members of the County Assembly (MCAs) pamoja na wananchi wanachagua miradi yao wenyewe na wanaisimamia inapofanyika katika gatuzi zetu. Kwa hivyo, kulingana na Kifungu cha 99 cha Katiba, sisi kama Maseneta tutasimama kidete kuhakikisha ya kwamba zile pesa ambazo zinatakikana kwenda kwa magatuzi, zimeenda. Tutafuatilia kuona ya kwamba zimetumika ili mwananchi aliye mashinani apate huduma bora.
view