All parliamentary appearances
Entries 401 to 410 of 461.
-
29 Sep 2010 in National Assembly:
Mr. Speaker, Sir, I withdraw but I will still repeat that---
view
-
29 Sep 2010 in National Assembly:
Mr. Speaker, Sir, I withdraw and apologize.
view
-
1 Sep 2010 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika ninakushuru sana kwa kunipatia nafasi hii. Ningependa kuunga mkono Hoja inayosema kwamba Bunge liende likizo hadi mwisho wa Septemba. Ningependa kuangazia mambo ambayo Bunge la Kumi limefanya. Wabunge katika Bunge hili wameshirikiana na kupitisha Miswada muhimu sana. Ingawa hivyo, tumefika wakati ambao lazima taifa liangazia mambo muhimu ya kuwaleta Wakenya pamoja. Kwa sasa tunasikitika kwa sababu serikali ya mseto inaonyesha dalili ya kutoelewana. Hii ndiyo inaleta kutoelewana kati ya wananchi. Ningependa kuomba serikali hii ya mseto ikiongozwa na viranja wawili kwamba ni muhimu serikali yao iongee kwa sauti moja. Katiba mpya imepitishwa. Mimi niliipinga lakini Wakenya wakaiunga ...
view
-
1 Sep 2010 in National Assembly:
mmoja anayefanya kazi kule. Alinipigia simu na akanieleza kwamba tangu taifa letu litoe masharti kufuatia usafiri wa Rais wa Sudan humu nchini, vuta nikuvute ambayo iko humu nchini imewapa wasiwasi, hata wengi waliogopa kulala jana. Leo hawajui ni nini kitajiri. Hawajui kutatokea nini kesho. Tungependa Serikali iombe msamaha Rais wa Uganda. Pia, tunataka Serikali ya Kenya iombe msamaha Serikali ya Sudan ili sisi na Wakenya walio huko wapate kuheshimiwa. Kuna wanafunzi wengi Wakenya ambao wanasomea Uganda. Katika eneo bunge langu kuna wanafunzi 7,800 wanaosomea katika vyuo vikuu vya Uganda. Hao wanafunzi walianza kutishwa baada ya Rais Museveni kukemewa katika uwanja ...
view
-
1 Sep 2010 in National Assembly:
On a point of order, Mr. Deputy Speaker, Sir. Is it in order for the Minister to say that every other Kenyan was given a peaceful serene environment to campaign and vote for or against the new Constitution, when I was harassed and picked up by the police when I was going to my office? I was locked up until the following day.
view
-
15 Apr 2010 in National Assembly:
Hoja ya Nidhamu, Bw. Naibu Spika wa Muda.
view
-
14 Apr 2010 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, nataka kusema kwamba kwa mara ya kwanza, namshukuru Waziri Mkuu kwa kufafanua vizuri kwamba maswala ya Katiba yatakuwa kulingana na demokrasia na hisia ya yeyote katika taifa la Kenya. Ni wakati muhimu ambapo taifa la Kenya litatatua kitendawili ambacho kimekuwepo kwa zaidi ya miaka 20; kuwepo Katiba ama kusiwepo. Kwa sasa, inajulikana kwamba kuna vikundi viwili; âlaâ, na ândioâ. Tungependa sisi mrengo wa âlaâ Waziri Mkuu athibitishe madai kwamba Serikali imepeana onyo kali kwa vyombo vya habari na wahusika wa utoaji wa habari kwamba taarifa isikuwe sawa kwa wanaounga Katiba na wanaoipinga, kwa sababu kwa ripoti yao ...
view
-
14 Apr 2010 in National Assembly:
Jambo la nidhamu, Bw. Naibu Spika. Sikutaka kujua kama Serikali itatoa usalama wa kutosha kwa wale wanaopinga Katiba Kielelezo. Bali nilitaka Waziri Mkuu aeleze Bunge hili kama Serikali imetoa vitisho kwa vyombo vya habari dhidi ya kuwapa nafasi ya kutosha wale watu wanaoipinga Katiba kielelezo kutoa hisia zao. Ninataka ufafanuzi juu ya jambo hili kutoka kwa Waziri Mkuu.
view
-
31 Mar 2010 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa fursa hii. Jambo la kwanza, ninaposikia kwamba Katiba hii imeweza kuleta sheria ya kuwezesha watu kuavya mimba, nasikitika. Sidhani kwamba haya ni maoni ya wengi wa Wakenya. Iwapo uavyaji wa mimba ukiidhinishwa na sheria, vijana wengi ambao kwa sasa wameweza kuoa na hali ya uchumi imekuwa ngumu, inamaanisha kwamba mke huyo anaweza kuchukuwa hatua kwa sababu sheria inamruhusu na kwenda kuavya mimba. Lazima tukirekebishe kipengee husika au tuiondoe kutoka Katiba kielelezo.
view
-
31 Mar 2010 in National Assembly:
Vile vile, Bw. Naibu Spika, maisha ya binadamu ni kitu muhimu, na ni lazima iheshimiwe. Naamini kwamba maisha yanaanza wakati mume na mke wanajamiana, ama wakati wanapokuwa na ile sherehe yao ya kuanza maisha au kutengeneza maisha ya mtu- --
view