Joyce Wanjalah Lay

Her story is of hope, hard work and resilience. Her father died before she completed her education but that did not stop her from pursuing her education later on as an adult. Even before joining politics she was passionate in helping and empowering her community.

All parliamentary appearances

Entries 11 to 20 of 169.

  • 9 Mar 2016 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninachukua nafasi hii kumpongeza Mhe. Millie Odhiambo kwa Mswada huu ambao umeweka alama katika nchi yetu ya Kenya katika kuwasaidia wale ambao hawawezi kupata watoto kwa njia ya kawaida. Mswada huu pia utaleta suluhu kwa wale ambao wanapata watoto kupitia kwa kina mama ambao wanawasaidia ili mtoto akizaliwa uwe unaweza kumpokea mtoto huyo kama mtoto wako siku ya kwanza bila kwenda kortini kupata stakabadhi ambazo ziko kamili. Sheria hii itawasaidia wananchi wengi wa Kenya. view
  • 2 Mar 2016 in National Assembly: Ninashukuru sana Mhe. Spika kwa fursa hii ya kuweza kuchangia Mswada huu kuhusiana na shamba za jamii. Kama tujuavyo, shida hizi za mashamba zimetukumba haswa sisi wakazi wa Pwani, Taita Taveta ikiongoza. Ni vizuri tukiwa na Mswada ambao unaweza kuambatana na Katiba yetu ya mwaka 2010. Lakini vile vile pia, tutasubiri wakati ambao utafika wa kuweza kufanya marekebisho kwa sababu kunayo marekebisho mengi ambayo yanastahili kuongezwa kwa Mswada huu. view
  • 2 Mar 2016 in National Assembly: Nikiguzia kipengele cha sita, kuhusiana na nyadhifa za serikari ya Kaunti, lazima zibainishwe wazi ni vipi. Kwa sababu, mashamba haya ya jamii yako chini ya serikari ya kaunti. Kwa hivyo, ni vizuri iwe wazi pale, je majukumu ya serikali ya kaunti kuhusiana na haya mashamba yatakuwa ni yapi? Vile vile wakati wanashikilia haya mashamba ya jamii itakuwa ni kwa muda ngani? Na kama niwao watakaokuwa wakiweka hazina hiyo ama kuna wakati mwingine ambao kunauwezekano kwamba kamati inaweza tengenezwa ili kwamba mambo yote yanayohusiana na ardhi ya jamii yapitie hiyo kamati. view
  • 2 Mar 2016 in National Assembly: Vile vile, lazima iwe wazi kwamba kuna mashamba ya jamii ambayo hayajasajiliwa. Haya mashamba, je, wakati mtu amekuja kama mwekezaji katika kauti hiyo, ni nani ambaye atahusika katika maswala hayo? Ni vizuri kama itakuwa wazi ili mtu yeyote ambaye anakuja kuekeza katika shamba za jamii, jamii hizo ziweze kuwakilishwa vilivyo. Manake wakati mwingine kuna mambo ya fidia, kwa mfano. Lazina tujue hiyo fidia ni nani haswa watakuwa wanaangazia. view
  • 2 Mar 2016 in National Assembly: Tukianganzia pia katika kipengele cha 37, tunaona kinazungumza kuhusu maswala ya ugawaji wa hiyo fidia. Ni vizuri wananchi wenyewe ama jamii ipatiwe nafasi, sauti na nguvu ya kuweza kuaamua kwamba ni nini haswa inataka kutoka kwa yule mwekezaji. Hii ni kwa sababu wakati mwingine hata si fedha labda zinatakikana; wanaweza kuamua kwa sababu huyu amekuja kuekeza kwao waweke ombi kwamba awatengenezee barabara au awajengee hospitali. Mambo haya yanaweza kutoka kwa wananchi wenyewe. view
  • 2 Mar 2016 in National Assembly: Vile vile nikiangazia katika kipengele cha 46, kunao watu ambao wameweza kukaa katika mashamba haya ya jamii bila idhini au stakabathi ambazo zinatakikana. Ni vizuri pia tujue kwamba kabla ya huu Mswada haujakuwa sheria, je mambo yao yanaweza kuangaziwa ili wasije wakawa hawataweza kufaidika sheria hii ikipita? Vile vile kunao Waingereza ambao waliondoka na kuacha mashamba makubwa makubwa. Haya mashamba ni vizuri tujue kama yatarudishwa kwa jamii ama serikali. Inafaa jambo hili lifanywe wazi. view
  • 2 Mar 2016 in National Assembly: Nikimalizia, kunao watu ambao wanakuja kuwekeza kwa mfano viwandani. Ni vizuri wananchi waweze kuelezewa madhara ya kazi hiyo ambayo huyo kama ni mbwenyenye amekuja kufanya. Hii ni kwa sababu tukiwa na uwazi utapata kwamba kukiwa na hatari yoyote ni vizuri hawa wananchi waweze kuelezwa na wao wenyewe wapate nafasi ya kuweza kuamua ni sawa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 2 Mar 2016 in National Assembly: kiwanda kiwekwe hapo au si sawa. Mambo haya yote yakiangaziwa katika huu Mswada, wakati utaletwa kwenye Kamati ya Bunge ninafikiri utakuwa wa kufana sana. view
  • 2 Mar 2016 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Spika. view
  • 17 Dec 2015 in National Assembly: Ahsante sana Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia kuhusiana na wale ambao wameteuliwa ili kwenda kusimamia Tume ya kupambana na ufisadi. Baada ya kusikiliza vile Mwenyekiti Wa Kamati ameongea, ni kuonyesha ya kwamba hao wote ambao wameteuliwa wako na umaarufu na vilevile wako na shahada za elimu za kuonyesha ya kwamba wamehitimu kwa kazi hii. Ningetaka kugusia kwamba Tume hii ni Tume ambayo inategemewa sana nchini Kenya katika mambo ya kupambana na ufisadi. Kwa sababu hii, tuko hapa kuzungumza leo kuhusu hawa ambao wameteuliwa na kuonyesha kwamba wale wengine ambao walitolewa, viongozi wa taifa hawakuwa na imani ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus