Joyce Wanjalah Lay

Her story is of hope, hard work and resilience. Her father died before she completed her education but that did not stop her from pursuing her education later on as an adult. Even before joining politics she was passionate in helping and empowering her community.

All parliamentary appearances

Entries 21 to 30 of 169.

  • 17 Dec 2015 in National Assembly: ndoto kubwa, matarajio makubwa na mipango mikubwa ya kusema kwamba wataweza kuangamiza hili jinamizi la ufisadi hapa nchini Kenya. Lakini tumeendelea tukiona kwamba ufisadi umeendelea kuzorotesha nchi yetu pamoja na uchumi wetu. Kwa hivyo, wajue kwamba Wakenya wote wanawaangalia ili tujue ni watu wangapi watapelekwa jela . Kusema kwamba mtu yeyote ambaye ametajwa katika mambo ya ufisadi akae kando ama atoke kazini tu, hiyo haisaidii.Wakati wanakaa kando ama wakati wanaacha kazi ni vizuri tupate kujua kama Wakenya hizo fedha wameiba, kama kunao ushahidi wowote kwamba wameiba hizo fedha, zitapatikana vipi na zitarudishwa vipi. Singeweza kutaja wote ambao wamewekwa hapo mbele ... view
  • 10 Nov 2015 in National Assembly: Hon. Speaker, I beg to give notice of the following Motion:- view
  • 10 Nov 2015 in National Assembly: THAT, aware that Article 21(3) of the Constitution mandates state organs to address the needs of persons with disabilities; noting that this vulnerable group continues to face numerous challenges in getting access to the Uwezo Fund, the Youth Enterprise Development Fund and the Women Enterprise Development Fund; deeply concerned that there is no clear mechanism to ensure that persons with disabilities get their share of the funds; this House resolves that 30 per cent of each of these funds be channeled through the Economic Empowerment Fund under the National Council for Persons with Disabilities. view
  • 30 Jun 2015 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Spika kwa fursa hii. Kwa kweli tumesubiri Ripoti hii kwa muda mrefu. Siku ya leo imewadia. Kitu ambacho wananchi wa Taita Taveta wanaomba ni kwamba haki itendeke. Ripoti inataka kuwe na uchunguzi wa kubaini kama haki ilitendeka kwa wananchi wa Taita Taveta katika kila mashamba ambayo walikuwa wanagawanyiwa kuanzia The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 30 Jun 2015 in National Assembly: shamba la Criticos ili tujue waliofaidika ni kina nani. Tunataka kujua kama waliofaidika ni wananchi ambao walikuwa hawana mashamba ama ni watu wengine. view
  • 30 Jun 2015 in National Assembly: Kwa hivyo, Ripoti inavyosema ni kwamba tuweze kuhakikisha ya kwamba tunajua mahali ukweli upo kwa sababu mambo ya mashamba yakiwachwa vile yako, huwa yanaleta shida. Yanaleta umwagaji damu na wananchi wanaanza kukosana wenyewe kwa wenyewe. Saa zingine inaweza kuwa kila kitu kimefanyika kihalali, lakini kwa sababu wananchi hawajaelezewa, hawawezi wakajua mahali ukweli upo. Kwa hivyo, ni vizuri kama kuna ukweli kisheria kuhusu chochote ambacho kilitendeka, tuwakalishe wananchi chini ili waweze kujua sheria na haki zilitendeka wapi. view
  • 30 Jun 2015 in National Assembly: Vile vile, tukigusia mambo ya mashamba upande wa Mwatate, katika shamba la makonge, limekua na utetezi kwa miaka mingi. Kumekuwa na wananchi ambao wamelia miaka mingi kwa sababu ya kunyanyaswa wakisema ya kwamba shamba hili la huyu bwenyenye ambaye analima makonge pale, ameingilia baadhi ya mashamba ya wananchi. Wamezunguka miaka mingi na ninakumbuka wako na kesi kortini hadi leo. Wamejitolea kuhakikisha ya kwamba haki imepatikana kutokana na kesi hii, lakini nguvu za wananchi ni chache kuliko za aliye na pesa nyingi. Akienda kortini, kuna njia anazotumia kuhakikisha haki ya wananchi haitendeki. Kulingana na Ripoti iliyosomwa mbele yetu, kuna barabara ambazo ... view
  • 30 Jun 2015 in National Assembly: Vile vile, Ripoti hii imegusia kuwa mwaka wa 1991, kulikua na wakati ambapo watu wa makonge walivamia mashamba wakakata mimea na chakula chote ambacho kilikua shambani. Huo mwaka, wananchi hawakupata fidia yoyote. Ni vizuri tuangalie hiyo fidia ili wananchi walipwe kwa sababu ni haki yao. Kama walikua wamelima chakula, najua mwaka huo walikaa njaa kwa sababu chakula chao kilikatwa. view
  • 30 Jun 2015 in National Assembly: Vile vile, lazima tuangalie katika Mwatate Settlement Scheme wapatiwe hati miliki kwa sababu wamekaa bila hati miliki kwa miaka mingi na hawajui kwamba kupata kile cheti ni utajiri wao. Hii ni kwasababu ukiambiwa una shamba lakini hauna cheti cha kuweza kumiliki, basi hautakuwa na ule utajiri ambao unaweza kujivunia. view
  • 30 Jun 2015 in National Assembly: Pia, kuna wananchi walioumia wakati walikuwa wanapigania mashamba. Walisema kuna wale waliumizwa na wengine wakaumwa na nyoka kwa sababu mahali yale makonge yamefika ni karibu na wananchi na yanaficha nyoka mle ndani. Wananchi wengi waliumwa na nyoka na wengine wakafariki. Kwa hivyo ni vizuri kuhakikisha kuwa haki za hizi familia zimetendeka. Vile vile, Mhe. Spika ulivyosema, kuwe na kamati ya kuhakikisha kwamba jambo hili ambalo limetoka katika Kamati ya Mashamba limefuatiliwa, kuhakikisha ukweli umetendeka na haki imefanyika kwa wananchi wa Taita Taveta. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus