24 Nov 2022 in Senate:
Mimi pia nimekuwa hapo na kusema ukweli, wale Wakenya niliowapata -kwa sababu kusema kweli Airport ya Doha ni ya Wakenya- kila mtu anakuonyesha furaha. Ilibidi niulize kama ni airport ya Wakenya au wameajiriwa.
view
24 Nov 2022 in Senate:
Nilipozungumza na hao Waarabu, walisema wanapenda Wakenya. Wao huajiriwan zaidi kwa sababu ya bidii yao ya kufanya kazi na pia kuwa watu wazuri sana. Balozi wa Qatar, Jabor Bin Ali, alipotembelea Bw. Spika aliuliza kwa nini hatujasikia mambo ya Qatar. Pia alisema kama kuna shida kama hiyo, twende kwa Balozi, tukae chini tuweze kuiangalia kwa kinaga ubaga.
view
24 Nov 2022 in Senate:
Kila Mara, mimi huuliza kwa nini ni Saudi Arabia peke yake? Kwingine kwaonekana lakini sana ni kwa Saudia na mpaka sasa sijaelewa. Nataka kueleza Seneta Veronica Maina ya kwamba juzi nilikuwa na Balozi wa Saudia aliyerudi tu juzijuzi. Alinipa kadi yake na akanialika kwake kuzungumzia jambo hili. Kitu cha kwanza nilizungumza naye ni hayo mambo ya vijana wetu kwenda kule na kusumbuliwa, kuadhibiwa na kuuliwa. Alisema labda tukae chini kuzungumzia haya mambo.
view
24 Nov 2022 in Senate:
Ningetaka kumwalika Seneta Veronica Maina ile siku tutakuwa na nafasi twende naye kwa sababu Balozi wa Saudia amenialika kwake ili tuzungumzie mambo haya. Pia, ningeomba “hustler Nation” kwa hii Serikali ya Mhe. Rais William Ruto itafute nafasi na kupea watoto wetu kazi hapa. Tusiwasumbue sana. Watoto wetu wanaenda kutafuta riziki yao kwa sababu imekosekana hapa.
view
24 Nov 2022 in Senate:
Tuliambiwa mama mboga na vijana wote watasaidiwa na pia kuna mambo ya “bottom-up.” Serikali hii imepewa nafasi ionyeshe ubingwa wa kupea vijana wetu kazi.
view
24 Nov 2022 in Senate:
La mwisho, nawapa pole wazazi na familia za wale wote wamepoteza watoto wao na ndugu zao huko Saudi Arabia. Inasikitisha sana kuona maiti ikiletwa kila siku. Kwa nini Saudia Arabia? Saudia Arabia iko karibu na kule sisi Waislamu tunaita Mecca. Tunashangaa ni kwa nini unyama huu unatendewa watu wetu wetu. Sisi tunajua Wakenya wana bidii katika kazi na wengi wao ni waaminifu. Labda nchi zingine zinalia vile sisi tunalia kwa hawa watu wetu.
view
24 Nov 2022 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, hili ni jambo la unyama na kusikitisha. Tunaomba Serikali ya Kenya na ya Saudi Arabia zitatue haya mambo. Pia, tuone wale waliotendewa unyama wakirudishwa au kulipwa fidia.
view
24 Nov 2022 in Senate:
Kama umepoteza jamaa wako, pesa haiwezi ikakusaidia. Lakini, hizo pesa zitasaidia wazazi ambao wasichana na vijana wao walioenda kufanya kazi lakini wakarudi kama maiti. Namshukuru dada yetu, Sen. Orwoba, kwa kutufungua macho kupitia mambo ambayo ameleta hapa. Amesema tuangalie mambo mengine ili tujue kama shida hizi zinaletwa na mawakala au kwenye wakaazi wa Saudi Arabia na kazi yao. Ikiwa mikataba yao imeisha, inafaa iangaliwe ili tujue mbona wanakumbwa na shida hizo. . Naomba kuunga mkono Hoja hii. Asante.
view
22 Nov 2022 in Senate:
Thank you, Mr. Temporary Speaker, Sir. Seriously, the use of hunger cries does not justify a decision to allow GMOs in this country. This is actually unsettling and a clear violation of the principles of human rights.
view
22 Nov 2022 in Senate:
GMOs were banned in 2012. I wonder where they have been resuscitated from. For this reason, we are concerned with our safety when it comes to GMOs. This is especially on our own consumption with this generic modified food, it is unacceptable.
view