Koigi Wamwere

Born

18th December 1949

Email

kwamwere@gmail.com

Telephone

0722905663

All parliamentary appearances

Entries 171 to 180 of 186.

  • 21 Jun 2006 in National Assembly: Mr. Deputy Speaker, Sir, again, I agree with the hon. Member that there are areas, including my constituency, where KBC radio and television waves do not reach. However, it is a bit far-fetched to ask the Government to hire Citizen Television staff to work for KBC in order to improve services. The improvement we are talking about will make KBC a better performer than Citizen Radio and Television. view
  • 21 Jun 2006 in National Assembly: Mr. Deputy Speaker, Sir, I visited the KBC premises two weeks ago. I am fully informed of the state of dilapidation of the buildings and their equipment. I am also aware that the KBC journalists and other staff need training in order for them to improve their services. It is in the interest of the Government to make sure that the KBC is the best performing television and 1476 PARLIAMENTARY DEBATES June 21, 2006 radio station in the country. view
  • 20 Jun 2006 in National Assembly: Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Naomba nichangie Hotuba ya Bajeti ya mwaka huu. Ilikuwa ni Bajeti yenye mema na maovu. Kwa kiwango fulani, ilimuinua maskini, lakini kwingineko ikamuangusha. Kabla sijazungumza juu ya upungufu wa Bajeti hii, ningependa kwanza kabisa kuipongeza Serikali kwa kutotilia maanani pesa za wafadhili wa kigeni katika Bajeti ya mwaka huu. Kama Serikali hii ingefanya hivyo, basi ingelikosea sana kwa sababu hakuna pesa zinazotolewa na wafadhili bila masharti. Masharti hayo yametufanya kuwategemea wageni sana kiasi kwamba mabalozi wa kigeni wakipiga chafya, nchi nzima inapata homa. Balozi akisema neno fulani na Rais aseme lake, magazeti yetu yatayaangazia ... view
  • 20 Jun 2006 in National Assembly: Lakini Waziri Msaidizi hana chochote! Tunataka Waziri mwenyewe kwa sababu tunatosha. Wakati kazi zinatolewa, ni vigumu Wilaya ya Nakuru kupewa chochote. Hatuwezi kusema tumepewa hata 1464 PARLIAMENTARY DEBATES June 20, 2006 balozi mmoja au katibu mkuu, au mkurugenzi katika kampuni yoyote ya umma. Hatupewi! Tunauliza, kama hii Serikali haipatii wakaaji wa Nakuru chochote, ni Serikali gani ambayo itakuja itupe? Rais mstaafu Moi alitunyima. Serikali hii nayo inatunyima; tunatakiwa tungojee Serikali gani ndio ije kukumbuka watu wa Nakuru? Hili ni swala ngumu ambalo ni lazima lifikiriwe. Bw. Naibu Spika wa Muda, Bajeti hii pia imesahau ya kwamba kuna wakaazi wengi sana ... view
  • 20 Jun 2006 in National Assembly: Nimeumwa kwa sababu kwangu kumejaa maskwota. Labda kina Kimunya hawana watu kama hawa kule wanakokaa na hawasumbuliwi nao. Kwa hivyo, hawaoni shida hiyo. Bw. Naibu Spika wa Muda, hakuna sehemu ya nchi hii ambayo ni muhimu kuliko nyingine. Kwa hivyo, ni lazima Bajeti hii ishughulikie Wakenya wote kwa namna sawa. Ni lazima sehemu zote ziwe sawa. Kwa hayo machache, naomba kuunga mkono. Lakini pia naiomba Wizara hii irekebishe upungufu ulio katika Bajeti hii. view
  • 31 May 2006 in National Assembly: Ahsante sana, Bw. Naibu Spika. Ninaomba kutoa mchango wangu kwa Hoja hii inayopendekeza tutafute namna nyingine ya kuimarisha vita dhidi ya ufisadi katika nchi hii. Ningependa kusema kwamba mpaka sasa, vita dhidi ya ufisadi vimekwama. Ninasema hivyo kwa sababu, ukiangalia hali ilivyo, utaona kwamba hakuna chochote kinachoendelea. Kwa kweli, ni kama tumepoteza vita dhidi ya ufisadi. Serikali, mahakama na Bunge, pamoja na wananchi, wamepoteza vita dhidi ya ufisadi. Kwa hivyo, tunakubali kwa moyo mkunjufu msaada wowote ambao tutapata kutusaidia katika vita hivi. Bw. Naibu Spika, ufisadi ni "ukoma" mbaya kuliko ule ugonjwa wa ukoma, kama tunavyoujua. Wafisadi ni wagonjwa wa ... view
  • 31 May 2006 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, nimeongea kuhusu watu ambao wamehusishwa na ufisadi. Sikumtaja mtu yeyote. Kama mhe. Ndolo hawajui, mwenye macho haambiwi "tazama". Uoga wangu mkubwa ni kuwa Rais anawaruhusu watu ambao wamehusishwa na ufisadi kumtembelea katika Ikulu. Watamuweka dosari. Ni lazima Rais siku moja asimame hadharani aseme: "Ikulu ni pahari patakatifu. Siyo pango la walanguzi. Sitaki kuona mhalifu yeyote akikaribia hapa". Watu ambao wametajwa katika ripoti za kamati ambazo zinachunguza ufisadi na waliopendekezwa kutoshikilia nyadhifa za umma, wanaendela kufanya hivyo. Hapa kuna kasoro kubwa. Wafisadi wamejaa Serikalini; kwa mfano, wako katika polisi na katika utawala wa mikoa. Bw. Naibu Spika, katika ... view
  • 29 Mar 2006 in National Assembly: On a point of order, Mr. Speaker, Sir. view
  • 29 Mar 2006 in National Assembly: Bw. Spika, jambo langu la nidhamu ni fupi sana. Ninataka kuuliza kama ripoti ya kamati imeporwa na gazeti fulani na kuchapishwa wakati ripoti hiyo bado haijafika Bungeni, je, gazeti kama hilo linaweza kuadhibiwa kwa namna yeyote? Je, vyombo vya habari vina uhuru wa kufanya wizi kama huo? Na wizi kama huo ukitendeka, ni hatua gani itachukuliwa? view
  • 29 Mar 2006 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus