All parliamentary appearances
Entries 11 to 20 of 186.
-
29 Aug 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, ni kweli Bw. Achieng'-Oneko alikuwa Waziri na alitoka Wilaya ya Nakuru. Lakini, alichaguliwa kwa misingi ya urafiki wake na hayati Rais Kenyatta. Bw. Murage, anatoka 3572 PARLIAMENTARY DEBATES August 29, 2007 Wilaya ya Kirinyaga. Yeye hatoki Nakuru. Kama angekuwa anatoka Nakuru, hangepewa hiyo kazi.
view
-
29 Aug 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna tatizo lingine ambalo ningependa tusaidiwe na Wizara ya Nchi za Kigeni. Hili jambo ni sifa mbaya ambayo Wakenya wamekuwa wakiipatia nchi hii. Ukisoma magazeti, utapata kwamba visa vya Wakenya wanaoshiriki katika kuharibu jina la nchi yetu huko ng'ambo vimeongezeka. Hivi majuzi tumesoma juu ya Wakenya waliofanya wizi huko Sudan. Aidha, juzi niliona katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Tanzania zaidi ya picha ishirini za Wakenya ambao wamehamia kule na wanafanya wizi. Isitoshe, tumekuwa tukisoma katika magazeti juu ya Wakenya wanaoshiriki katika wizi kule Marekani. Ninadhani kuna haja ya Wizara hii kutembelea Wakenya hawa ...
view
-
8 Aug 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa niaba ya Chama Cha Mwananchi (CCM), naomba kuunga mkono Hoja hii ya kudhibiti ubinafsishaji wa mashirika ya umma. Awali kabisa ningetaka kusema kwamba tumeshuhudia ubinafsishaji wa mashamba yetu ambao mpaka sasa haujaleta faida yoyote isipokuwa kuzidisha umaskini. Kama tunataka kuyafanyia mashirika yetu ya umma, yale ambayo tumefanyia ardhi yetu, ni wazi kwamba itakuwa vigumu sana nchi yetu kufaidika kutokana na ubinafsishaji zaidi wa mashirika ya umma. August 8, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 3037
view
-
8 Aug 2007 in National Assembly:
Chama Cha Mwananchi!
view
-
8 Aug 2007 in National Assembly:
Chama Cha Mwananchi ambacho kimo katika mseto wa Serikali hii.
view
-
8 Aug 2007 in National Assembly:
Ndiyo, sasa hivi.
view
-
8 Aug 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, hiyo ni kweli, lakini si hoja. Mashirika ya umma yalijengwa na pesa za umma na ni wazi kwamba umma ndio unapata hasara kubwa wakati mashirika yake yanauziwa watu binafsi kwa bei ya kutupa. Wakati huu, kuna haraka ya kuyauza mashirika ya umma. Hili ni jambo lisiloeleweka. Ni majuzi tu tumeona shirika la bima la Kenya Re-insurance likiuziwa watu binafsi, ijapokuwa kuna hisa chache ambazo zimekwenda kwa umma. Kitambo, tuliona Shirika la Reli likiuziwa kampuni ya kigeni. Sasa tuko katika harakati za kuuza mashirika ya simu ya Safaricom na Telkom. Bw. Naibu Spika wa Muda, kampuni ...
view
-
8 Aug 2007 in National Assembly:
On a point of order, Mr. Temporary Deputy Speaker, Sir. I hope the Chair heard the speaker refer to some "two communists" who have contributed before him. Is it in order for any hon. Member to refer to other hon. Members as communists, unless they have so declared?
view
-
1 Aug 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika, ninasikitika kwamba hatuna muda wa kutosha kwa sababu ningependa kusema mengi kuhusu kwa nini hukumu ya kifo haihitajiki katika nchi hii. Kwanza, makosa hufanyika na watu ambao hawana hatia wameuawa. Wale ambao wanafikiria ya kwamba kwa sababu mtu amekufa aliyemuua lazima apewe hukumu ya kifo, wanaongea kama hawajui kwamba kuna aina zingine za adhabu ambazo zinaweza kuzuia uhalifu. Sio lazima mtu auawe ndio tuzuie uhalifu. Isitoshe, kama umemuua mtu, huwezi kumurekebisha tena. Ukikosea na umuue mtu ambaye hana hatia, hayo makosa hayawezi kurekebishwa. Huyo mtu atakuwa amekufa bure. Mimi mwenyewe nilikabiliwa na hukumu ya kifo mara mbili. ...
view
-
1 Aug 2007 in National Assembly:
I bowed!
view