All parliamentary appearances
Entries 21 to 30 of 186.
-
1 Aug 2007 in National Assembly:
Absolutely!
view
-
1 Aug 2007 in National Assembly:
Jambo la nidhamu, Bw. Naibu Spika. Nashangaa ya kwamba Bw. Naibu Spika ameruhusu matamshi yaliyotolewa na Waziri Munyao kumaanisha ya kwamba yeyote ambaye anachukua msimamo tofauti na wake, ni mtu ambaye ana kasoro za kiakili. Nadhani hayo ni maneno yanayohitaji kuondolewa.
view
-
1 Aug 2007 in National Assembly:
You are right!
view
-
1 Aug 2007 in National Assembly:
Absolutely!
view
-
25 Jul 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, asante kwa kunipa nafasi hii fupi ili nami niunge mkono Hoja hii.
view
-
25 Jul 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, naunga mkono Hoja hii kwa sababu nchi hii ina haja kubwa ya kuzalisha kazi ili tuweze kumaliza uhalifu. Kuna watu wengi ambao wanaamini kwamba njia bora ya kumaliza uhalifu ni kuua kila asiyekuwa na kazi. Lakini ukiniuliza, dawa ya kumaliza uhalifu ni kuwapa vijana kazi. Tukiwapa kazi hatutakuwa na vikundi kama vile Mungiki, Sabaot Defence Force au Mombasa Republican Council. Hakuna njia nyingine. Tuwapatie vijana kazi kwa kutumia mbinu hii ambayo ilitumiwa Marekani na ikafaulu. Tunahitaji kuwatumia vijana kujenga mabwawa, barabara na tuwapatie mashamba. Nchi hii ina mashamba mengi ambayo hayatumiwi. Wale ambao hawayatumii mashamba ...
view
-
25 Jul 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, naunga mkono.
view
-
18 Jul 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, asante kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Hoja juu ya kuwatakia polisi masilahi na mishahara bora zaidi. Nadhani hili ni jambo ambalo haliwezi kupingwa na yeyote kwa sababu maofisa wa polisi, kama vile Wakenya wengine, wanahitaji mishahara na nyumba bora za kuishi. Zile nyumba wanamokaa zinazoitwa A-frame structure ni vyumba ambavyo havistahili kuwepo tena. Bw. Naibu Spika wa Muda, nakumbuka zamani sana tukibishana na Mkuu wa Polisi katika Mkoa wa Bonde la Ufa, Bw. Mbijiwe. Wakati nilisema polisi wanastahili kujengewa nyumba bora zaidi, niliporudi nyumbani nilikutana naye na akawa mkali sana kwangu akisema sina haki ...
view
-
18 Jul 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, nilikuwa nasema ni muhimu wakumbushwe kutekeleza kazi yao kwa usawa kwa sababu nadhani bado kuna tatizo miongoni mwa polisi. Kuna tatizo la kusema ya kwamba polisi wanatekeleza ule wito wao wa utumishi kwa wote bila ubaguzi. Wakati mwingine unakuta ya kwamba polisi wakihitajika kwenda kuwahudumia matajiri, wao huenda haraka kuliko wakati wanahitajika kuwahudumia maskini. Hili nalijua kwa sababu wakati mwingine hata utakuta kuna matajiri au viongozi wanafanya uhalifu ambao unaonekana hata katika runinga lakini unakuta hawashtakiwi. Je, kuna sheria mbili; moja ya viongozi na matajiri na nyingine ya maskini? 2584 PARLIAMENTARY DEBATES July 18, 2007 ...
view
-
18 Jul 2007 in National Assembly:
Bwana Naibu Spika wa Muda, watu hawa wamekosa haki kwa sababu kuna maofisa wakubwa katika polisi ambao wanawazuia kurudi kazini. Mmoja wao ambaye wamemtaja katika affidavit yao ni Bw. Kimaiyo. Aliwaambia kwamba akiwa mamlakani, watu hao hawatarudi kazini. Hii inafanya tujiulize: Sheria hii ya kupiga firimbi tuliipitisha ya nini kama hatukuwa na nia ya kuhakikisha kwamba inawalinda wanyonge ambao wanapiga firimbi kwa lengo la kusaidia Serikali kupigana na ufisadi? Ningetaka kusema kwamba, wakati polisi wanakataa kuwasaidia wapiga firimbi, ni kama wanatoa ishara kwa nchi nzima ya kuonyesha kwamba Serikali haina nia ya kupigana na ufisadi. Naunga mkono.
view