All parliamentary appearances
Entries 181 to 186 of 186.
-
29 Mar 2006 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, kujibu baadhi ya mambo ya nidhamu ni kunipotezea wakati!
view
-
29 Mar 2006 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba niongezewe dakika mbili ambazo zimepotea. Serikali hii imeufanyia Upinzani ufadhili wa hali ya juu kwa sababu imewaleta Serikalini hata kama hawana idhini ya kuwemo Serikalini. Shida iliyoko ni kwamba ukiwapa wapinzani shubiri, wanataka pima! Ukiwapa tabasamu, wanataka busu. Wanataka yote kwa pupa! Ndiyo sababu ni rahisi sana watakosa yote. Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kuzungumzia suala la ukabila. Rais angeongea zaidi kuhusu swala hilo. Ukabila ni adui mkubwa sana kwa nchi hii. Kama ningekuwa na uwezo, ningependa Wabunge waitazame filamu iitwayo "Hotel Rwanda." Hiyo filamu inaonyesha hasara ambayo inaweza kupatikana katika nchi kutokana ...
view
-
29 Mar 2006 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo hili liliongewa Bungeni. Hata hivyo, ninalotaka kusema ni kuwe na vigezo sawa. Waziri huyo alikiri kwamba kampuni ilimlipia bibi yake safari ya kwenda ulaya na akarudisha pesa hizo baadaye. Sasa ninauliza, kama kosa lilifanyika, litaisha kwa sababu pesa zilirudishwa?
view
-
29 Mar 2006 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, ninaongea juu ya mhe. Raila Odinga. Alikuja hapa na akasema kwamba ---
view
-
29 Mar 2006 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, huyo Waziri alifanya ufisadi na inatakikana achukuliwe hatua. Kwa hayo machache, ninaunga mkono.
view
-
28 Mar 2006 in National Assembly:
Jambo la nidhamu, Bw. Naibu Spika wa Muda. Waziri amesimama kwa jambo la nidhamu akitaka kujua kama jambo ambalo liko kortini linaweza kuzungumziwa hapa. Hili ni jambo ambalo linatakiwa kutolewa uamuzi na Kiti. Lakini sio Mzungumzaji aulizwe kama jambo liko kortini au haliko kortini. Ni muhimu Kiti kitoe uamuzi juu ya swala hilo.
view