Koigi Wamwere

Born

18th December 1949

Email

kwamwere@gmail.com

Telephone

0722905663

All parliamentary appearances

Entries 31 to 40 of 186.

  • 18 Jul 2007 in National Assembly: On a point of information, Mr. Temporary Deputy Speaker, Sir. view
  • 18 Jul 2007 in National Assembly: Mr. Temporary Deputy Speaker, Sir, my point of information is very harmless. I just want to inform view
  • 18 Jul 2007 in National Assembly: that, in fact, there has been a court ruling on the matter of Grand Regency Hotel, to the effect that those workers should return to work. To the extent of that court ruling, those workers cannot be expected to do anything more to deserve police protection to the very end. view
  • 18 Jul 2007 in National Assembly: Mr. Temporary Deputy Speaker, Sir--- view
  • 12 Jul 2007 in National Assembly: Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi ili nichangia mjadala huu kuhusu Hoja hii ya bajeti ya Wizara ya Usalama wa Ndani. Bw. Spika, ningependa kuanza kwa kusema kwamba katika kupigana vita dhidi ya uhalifu, ni muhimu watu wetu wafundishwe kuheshimu polisi, kama marafiki na walinzi wao. Wanafaa kuacha kuwaona kama adui. Kwa hivyo, ni jambo la kuhuzunisha na makosa makubwa mtu anaposikia kwamba polisi wameshambuliwa na kuuawa wakiwa kazini. Kama wengi wa Wabunge wenzangu walioongea hapa jana, naamini pia kwamba polisi wanastahili bima. Bima hii itahakikisha kwamba kwa bahati mbaya askari akikutana na kifo, familia yake itashughulikiwa. Pia, polisi wanastahili ... view
  • 12 Jul 2007 in National Assembly: 2490 PARLIAMENTARY DEBATES July 12,2006 view
  • 12 Jul 2007 in National Assembly: Bw. Spika ni ofisa mkuu wa Bunge. Bw. Spika, kihalali, polisi ni mkono wa Serikali wa kutekeleza sheria, kwa mujibu wa sheria. Bunge nalo linaunda sheria. Mahakama hutafsiri sheria na kutoa hukumu na adhabu. Kwa mujibu wa mpangilio huu, hata kama ameshikwa mshukiwa wa uhalifu wowote, hana hatia mpaka ahukumiwe na mahakama, ili imuachilie au impe adhabu. Hii ni kanuni muhimu ambayo inafaa kufuatwa na polisi. Nasema hivi kwa sababu, kama kazi ingekuwa inafanywa vile inavyofanywa sasa--- Tungekuwa tunaendelea na utawala uliopita, nadhani wengine wetu hatungekuwa hapa tukiongea. Tungekatwa zamani kama wahalifu. Mara nyingi tulishikwa kama washukiwa, lakini kwa bahati ... view
  • 5 Jul 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba kujibu. Kwanza nataka kuwashukuru waheshimiwa Wabunge wote waliochangia mjadala kuhusu Mswada huu. Tulisikiza kwa makini maoni yao yote. Tutakapoingia katika Kamati ya Bunge nzima, ni matumaini yangu ya kwamba Wabunge wataleta maoni yao kama marekebisho, ili tuweze kuboresha sheria hii. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna mengine ambayo yalisemwa kwa nia ya kuwafurahisha waandishi wa habari. Ni vigumu sana kuyajibu hayo kwa sababu hayawezi kujibika. Wabunge hao walikuwa wanajua kwamba wamepoteza mjadala. Kitu ambacho walikuwa na haja nacho ni kuwajulisha waandishi wa habari kwamba wako upande mmoja. Lakini sote tuko upande mmoja. Bw. Naibu ... view
  • 5 Jul 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, sitaongea sana. Lakini katika kukamilisha jibu, ninataka kusema kwamba hakuna yeyote ambaye anaweza kupewa uwezo wa kubomoa demokrasia katika nchi. Wakati mwingine, jambo hili linawezekana wakati ambapo vyombo vya habari vinapewa uhuru zaidi wa kutetea kitu kama ukabila. Jambo hili lilifanyika huko Rwanda na Somalia. Itakuwa ni makosa makubwa ikiwa nchi hii, badala ya kufaidika na uzoefu wa nchi nyingine, itarudia makosa yayo hayo ya kupatia vyombo vya habari uwezo wa kuvuruga nchi. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo machache, naomba kujibu. view
  • 5 Jul 2007 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba kuunga mkono Mswada huu wa sheria ya tumbaku. Kama alivyosema Waziri Msaidizi mwenzangu, hii ni hatua kubwa sana. Labda ni ya kwanza katika kaya hii yetu. Natumaini ya kwamba Wabunge wote, hasa Maj. Madoka, wataona haja ya kuunga mkono Mswada huu. Bw. Naibu Spika wa Muda, natumaini ya kwamba watu wetu wataweza kujua ya kwamba hakuna uungwana au uustarabu katika uvutaji wa sigara. Wengi wa wale ambao wanavuta sigara, hasa vijana, wavulana na wasichana wachanga, wanavuta sigara kwa sababu wanataka kuonekana kama waangwana wa aina ya kipekee. Ni rahisi sana vijana kushawishika kuvuta sigara ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus