All parliamentary appearances
Entries 41 to 50 of 186.
-
5 Jul 2007 in National Assembly:
- wale ambao wamekolea katika jela mpaka wamekuwa kama wafalme kiasi kwamba hakuna kitu hawawezi kuingiza katika jela--- Wale matrustee wakiwa na sigara zao, utakuta watu wanapanga laini wakati kunapeanwa nyama. Nyama inapeanwa vipande vidogo sana mara tatu kwa wiki. Vile nyama ni nadra, hakuna mtu ambaye hangetaka kula nyama hiyo. Lakini utakuta ya kwamba tamaa ya kuvuta sigara ni kubwa kuliko ile tamaa ya kula nyama. Unakuta watu wamepanga laini. Mtu anapewa sigara avute mara moja tu na kisha anairusha nyama yake kwenye bakuli. Mpaka unawahurumia watu hawa. Watu hawa hawapati nyama kwa miezi mingi na wakiipata wako tayari ...
view
-
5 Jul 2007 in National Assembly:
ni walipa kodi kama watu wa sehemu nyingine katika nchi hii. Mhe. G.G. Karikui hapa anatosha kuwa Waziri. Ijapokuwa alikuwa Waziri kwa muda mrefu sana. Nadhani sasa ingekuwa ni wakati wa kuwaachia watu kama sisi. Lakini tunachosema ni kwamba, hata kama hatutakalia viti hivyo, tunyimwe kwa sababu hatuna sifa, na siyo kwa sababu tunatoka Nakuru. Kuna wengi ambao wametunukiwa nyadhifa kubwa sana, na ni wavutaji wakubwa wa sigara. Tunauliza nchi ifuate nyayo za Nakuru katika kupiga marafuku uvutaji wa sigara. Hivyo, hivyo, tunauliza ya kwamba watu wa Nakuru, Laikipa na wakaazi wa Mkoa wa Bonde la Ufa ambao hawahesabiwi kama ...
view
-
4 Jul 2007 in National Assembly:
Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Wiki jana, Wizara yangu iliwasiliana na mheshimiwa Weya katika semina moja kule Naivasha na tulimfahamisha kwamba Wizara imetayarisha Mswada kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Kwa hivyo, jambo ambalo linatafutwa katika Hoja hii limeshughulikiwa vya kutosha katika Mswada huo. Mswada huo unaeleza kwa kikamilifu namna Serikali imeunda mfuko wa pesa ambazo zitatumika kusambaza teknolojia ya habari na mawasiliano katika kila pahali nchini. Serikali imeunda mpango maalum wa kuhakikisha kwamba kuna kijiji cha teknolojia ya tarakimu au digital village katika kila eneo la uwakilishi Bungeni. Kwa hivyo, ni wazi kwamba kinachotafutwa na Hoja hii kimeshughulikiwa ...
view
-
4 Jul 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, nilikuwa nimemaliza kujibu. Nimesema kwamba tumeelewana na mheshimiwa Weya na hatuna upinzani. Tunafikiria kwamba lengo la Hoja hii ni sawa na lengo la Mswada wa Teknolojia, Habari na Mawasiliano. Kama hataki kuondoa Hoja hii, sisi tuko tayari kuiunga mkono tukiamini ya kwamba aidha wiki hii ama wiki ijayo, tutaleta Mswada ambao utashughulikia Hoja hii.
view
-
4 Jul 2007 in National Assembly:
Jambo la nidhamu, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ningependa mhe. Mbunge aeleze kama halipotoshi Bunge anapodai kwamba Safaricom ni kampuni ya kimataifa, wakati asilimia 60 ya hisa za kampuni hiyo zinamilikiwa na Telkom ambayo ni kampuni ya taifa hili.
view
-
4 Jul 2007 in National Assembly:
He called it a multinational company.
view
-
4 Jul 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda---
view
-
4 Jul 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, kama ulivyoeleza, swala ambalo tunahitaji kulielewa vizuri ni kama hisa nyingi za kampuni ya Safaricom zinamilikiwa na watu kutoka nje ya nchi au watu wa hapa nchini. Kama hisa nyingi za kampuni hii zinamilikiwa na Wakenya kupitia makampuni yao, je, mhe. Mbunge, si analipotosha Bunge anapodai kwamba hii ni kampuni ya kimataifa? Ninachosema ni kwamba hii ni kampuni ya kitaifa.
view
-
4 Jul 2007 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba---
view
-
4 Jul 2007 in National Assembly:
Mr. Temporary Deputy Speaker, Sir, maybe, I can now explain in English what my contention is.
view