Lydia Haika Mnene Mizighi

Parties & Coalitions

Email

hycalydy@gmail.com

Telephone

0721452391

All parliamentary appearances

Entries 61 to 70 of 80.

  • 2 Oct 2019 in National Assembly: Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa ili niweze kujadili Mswada huu. Ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu ufisadi katika nchi yetu ya Kenya umekithiri sana. Hivyo basi, mambo mengi yamekuwa hayaendi ipasavyo. Mambo mengi hayaendi vizuri The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 2 Oct 2019 in National Assembly: kwa sababu ya suala hili la ufisadi. Mahospitali hayana madawa na watu wanakufa ovyo ovyo. Ukifuatilia sana, unapata ni kwa sababu ya ufisadi. Kuna kisa kimoja cha ufisadi kilichonishangaza sana. Kilinisababisha kutambua ufisadi umefanya watu kupenda mali zaidi, hata utu umewatoka. Dereva wa ambulance alienda kuchukua mgonjwa ambaye alikua ni mama mja mzito aliyekuwa karibu kujifungua. Lakini kufika pale, akasema kwanza anataka afungiwe kitu chake kidogo ambacho hakina risiti wala hakijulikani mahali popote akiweke mfukoni ndiposa waende. Ni huzuni kwa maana tulimpoteza huyo mama. Nilimshughulikia yule dereva vilivyo kwa sababu nilivyofahamishwa hali hiyo sikufurahi. Hiki ni mojawapo ya visa vya ... view
  • 2 Oct 2019 in National Assembly: Tumeona watu wengi, na majina tajika, yakihusishwa na ufisadi. view
  • 2 Oct 2019 in National Assembly: Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nilikuwa ninasema kwamba tumeona watu wengi ambao wamehusishwa na masuala ya ufisadi katika nchi hii ya Kenya lakini kufikia sasa, ni kama hatua inayofaa kuchukuliwa haijachukuliwa kwa sababu wengi wao wako huru. Wengi wao ni majina tajika na viongozi ambao tunaweza kuwaita kwa kiingereza role models . Hii inasababisha hali hii ya ufisadi kuonekana kama ni hali ya kawaida. Hakuna hofu kabisa ya mtu kutotaka kufanya ufisadi wa hali yoyote kwa sababu wale ambao wamehusishwa wako huru na wanaendelea kuishi maisha yao ya kawaida. Basi watu wanaona kwamba ufisadi umekuwa ni jambo la ... view
  • 2 Oct 2019 in National Assembly: Kwa hivyo, ninaunga mkono hukumu iongezwe na ifuatiliwe. Watu wanapopatikana kwa ufisadi, wahukumiwe ipasvyo. view
  • 2 Oct 2019 in National Assembly: Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 2 Oct 2019 in National Assembly: Hon. Temporary Deputy Speaker, asante sana kwa kunipatia fursa hii nami niweze kuichangia Hoja. Yale yaliyotokea yametuumiza mioyo sana. Naibu Spika wa Muda, kwa niaba ya wakaazi wa Taita Taveta, natoa rambirambi kwa familia ya Mariam na mtoto Mutheu, ambao walipoteza maisha katika mkasa huo. Hili ni jambo la aibu sana na la kusikitisha katika karne hii. Wakenya wanapoteza maisha kwa mambo ambayo yanaweza kuzuilika. Kuna utepetevu fulani na uzembe mkubwa katika shirika la huduma za feri. Ni lazima watu wawajibike kwa kazi ambazo wamepewa kuhudumia wananchi. Wakenya, na viongozi pia, ni lazima tutafakari ni vipi tumejiandaa kukabiliana na majanga ... view
  • 2 Oct 2019 in National Assembly: yanapotokea. Majanga aina tofauti tofauti yanaweza kutokea na ni vipi tumejitayarisha kukabiliana nayo? Nikimalizia, naendelea kutoa pole zangu. Hili liwe janga la mwisho na kila mmoja wetu aweze kuwajibika katika majukumu ambayo amepewa – ayafanye vyema ili tusipate mikasa kama hiyo siku zijazo. Asante sana, Naibu Spika wa Muda. view
  • 26 Sep 2019 in National Assembly: Thank you very much, Hon. Temporary Deputy Speaker, for giving me this opportunity to add my voice to this very important Bill. Having learnt what it entails, I take this opportunity to congratulate the Departmental Committee on Education and Research and the Chair for work well done. Most of the requirements and proposals in this Bill are very important. They are relevant in making our education system better, to upgrade our education sector and, most importantly, the ECDE. Having listened to most of us speak about this Bill, it is well articulated. It has touched most of the contentious issues ... view
  • 25 Sep 2019 in National Assembly: Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili niweze kuchangia Mswada huu ambao ni mzuri. Ninampongeza Mhe. Martha kwa kuweza kuleta Mswada huu Bungeni. Kama akina mama, tunahusika sana kutetea masuala kama haya kwa sababu mara nyingisisi ndio hukaa na watoto na tunajua ni muda gani unahitajika kukaa nao ili waweze kuwekwa katika hali iliyo sawa. Ninaunga mkono Suala la kuweza kuwa na muda unaofaa na mtoto mdogo kwa sababu muda huu ndio utakaoruhusu kuweza kumjua mtoto vizuri naye akujue na utaweza kumfundisha maadili yanayofaa. Mara nyingi tunawakuza watoto bila ya kuwa na muda nao na wanakosa ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus