Hon Mishi Juma Khamisi

Mishi actively participated in Likoni political campaigns in 1997 and 2002. She vied for Likoni parliamentary seat in 2007 and lost in party nominations which were marred by irregularities. She would like to see government funded drug rehabilitation centres established in Mombasa.

All parliamentary appearances

Entries 121 to 130 of 404.

  • 26 Nov 2020 in National Assembly: Bi Naibu Spika wa Muda, ninamalizia. Ninaunga mkono iwapo Hoja hii itakuwa na marekebisho yaliyopendekezwa na Daktari Mhe. Nyikal. Itakuwa Hoja itakayotimiza malengo yetu. Tunapozungumzia hii Hoja, lazima tujue tutatumia lugha aina gani itakayotuwezesha kutekeleza mapendekezo ambayo tumeyazungumzia. Ninaunga Mkono. view
  • 19 Nov 2020 in National Assembly: Asante sana, Naibu Mhe. Spika Wa Muda. Mimi pia napata nafasi hii kuweza kuzungumzia Hotuba ya Mheshimiwa Rais na niseme ilikuwa ya kizalendo sana. Alizungumzia mambo mengi sana. Nimeskia Waheshimiwa wenzangu wakizungumzia janga la Corona. Jamani hakuna ambaye hakumwona Mheshimiwa Rais aking’ang’ana wakati tulipata kesi ya kwanza ya Corona. Hata viongozi wengine tukiwemo sisi wenyewe tulisema ya kwamba Corona ni uongo na ni jambo la kutengenezea watu pesa na ni mambo ya propaganda . Kwa hivyo, mimi nataka niseme kuwa wakati tunazungumzia ufisadi katika mambo ya Corona, sisi Wabunge tuna jukumu la kuangazia mambo ambayo yalifanyika katika taifa letu la ... view
  • 19 Nov 2020 in National Assembly: Vile vile, Mhe. Rais alizungumzia kuhusu kujenga ajira laki moja ya vijana wetu. Nataka kushukuru mpango wa Kazi Mtaani . Huu mpango umeweza kuchukua vijana 26,000 katika kauti The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 19 Nov 2020 in National Assembly: 34. Kwa sababu janga la Corona linaendelea, vijana waweze kuendelea na huu mpango na uweze kuangalia vijana wote katika kaunti zetu 47. Pia, yale mapato wanapata yaweze kuangaziwa. view
  • 19 Nov 2020 in National Assembly: Namshukuru Mhe. Rais kwa kutujengea daraja katika Eneo Bunge langu likishikana na Eneo Bunge la Mvita. Kwa sababu ya mambo ya Corona, watu wa Likoni walikuwa na changamoto kubwa sana kujikinga na janga hili. Hivyo basi, daraja hili litaweza kutusaidia kwa ule msongamano na tuweze kusafiri na kuendelea na shughuli zetu. view
  • 19 Nov 2020 in National Assembly: Pia, Mhe. Rais alizungumzia ule mpango wa mambo ya boda boda. Hii ni njia moja ambayo itaweza kujenga ajira zaidi kwa vijana wetu kule nyanjani. Basi mpango kama huu uweze kusambaswa kule mashinani katika maeneo Bunge yetu na kauti zetu ili kujenga ajira. Mhe. Raisi alisema kuwa vijana wajitokeze ili waweze kupate mshahara na kuwa wamiliki wa fedha. Kwa hivyo, ni lazima wajenge uwezo katika kupata zabuni kama za madeski, za kufanya kazi ya kuleta vifaa vya kupigana na Corona na za ule mpango wa kutengeneza nyumba za kisasa katika makazi duni. Hii ni kwa sababu tunataka kuweka Wakenya katika ... view
  • 10 Nov 2020 in National Assembly: Asante sana, Bw. Spika kwa sababu Waswahili wanasema, bandu bandu humaliza gogo. Swala hili tulilizungumzia kwa muda mrefu sana, haswa sisi Wabunge wa kutoka sehemu ya Pwani. Na kila wakati tulipokuwa tukilizungumzia, lilikuwa linaleta tashwishi na hamasa nyingi haswa kule kwetu Pwani. Lakini, kama Serikali na Wakenya, tumeangalia swala hili na tukaamua tuwe na mazungumzo. Na kwa kuzungumza kwetu, tumeweza kupata suluhu; suluhu ambayo itakuwa inamwangazia Mkenya kule mashinani na pia kuzingatia mikakati ya Serikali, ile kwa Kiingereza tunasema symbiotic model ambayo kila mmoja katika wale washikadau watafaulu na maamuzi haya ambayo yamewekwa na Kamati ya Bunge ya Uchukuzi. Nataka ... view
  • 5 Nov 2020 in National Assembly: Thank you, Hon. Deputy Speaker. I beg to give notice of the following Motion: THAT, aware that the National Hygiene Programme (NHP), dubbed Kazi Mtaani, is a national initiative that was designed to cushion the most vulnerable but able-bodied citizens living in informal settlements from the effects and response strategies of the Covid- 19 pandemic; acknowledging that the first phase of the programme started in April 2020 covering eight counties employing over 26,000 workers while the second phase, which began in July 2020 was expanded to cover 34 counties employing over 200,000 workers and is expected to run for six-and-half ... view
  • 5 Nov 2020 in National Assembly: counties to address youth unemployment and further cushion the vulnerable members of society, and reviews the current remuneration of the workers in accordance with the Wage Order of 2018. view
  • 5 Nov 2020 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na dadangu Mhe. Wamaua. Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa hakika stakabadhi hii tunaita birth certificate, ni muhimu sana na ni cheti cha kwanza mtoto hupata akizaliwa. Stakabadhi hii ndiyo itaonyesha umri wa mtoto huyu ambaye amezaliwa katika Taifa letu la Kenya. Tumeona changamoto nyingi sana ambazo Wakenya wengi wamepata kupata stakabadhi kama hizi, haswa tukiangalia wenzetu kutoka kule sehemu za North Eastern. Wamekuwa na changamoto nyingi sana. Hata kule kwetu Mombasa imekuwa ni changamoto kupata stakabadhi kama hii. Stakabadhi kama hii hivi sasa ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus