Hon Mishi Juma Khamisi

Mishi actively participated in Likoni political campaigns in 1997 and 2002. She vied for Likoni parliamentary seat in 2007 and lost in party nominations which were marred by irregularities. She would like to see government funded drug rehabilitation centres established in Mombasa.

All parliamentary appearances

Entries 291 to 300 of 404.

  • 20 Apr 2016 in National Assembly: Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza natoa shukrani kwa Kamati ya Mashamba pamoja na Wanakamati kwa sababu wamekuwa wavumilivu na walihusisha jamii tofauti tofauti haswa zile ambazo zimekuwa na utata katika suala la ardhi haswa ardhi za jamii. Nataka kusema ya kwamba sisi kama Wabunge tuwe na moyo kama huu. Tushauriane na tuzungumzie ile Misuada muhimu sana. view
  • 20 Apr 2016 in National Assembly: Hivi sasa najua pia tutakuwa na sheria za ardhi. Tunataka tuwe na ushauriano kama huo. Tukae tuone kama tunaweza kuleta mabadiliko machache katika Mswada ule ndiposa tukija hapa tuwe tunazungumza kwa sauti moja. Ijapokua najua pengine kwa moja ama mbili unaweza kuwa mmetofautiana lakini kwa ujumla tuweze kupata sheria nzuri na Mswada ambao utatusaidia na utatatua yale masuala ya ardhi haswa hili suala la ardhi ya jamii. view
  • 20 Apr 2016 in National Assembly: Nawashukuru sana. view
  • 19 Apr 2016 in National Assembly: Thank you, Hon. Temporary Deputy Chairlady. I concur with the sentiments of the Chair of the Departmental Committee on Lands on the deletion of Clause 15. It is in order. I support it. view
  • 29 Mar 2016 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ya kuzungumzia Mswada huu kuhusu sheria ya ardhi. Hili ni suala ambalo ni nyeti na limeleta maafa mengi hapa Kenya. Jamii nyingi zimepigana kwa sababu ya mambo ya mashamba. Sheria hii imekiuka matakwa ambayo Wakenya walizungumzia katika Katiba. Sheria hii inasema kwamba kila pahali ambapo kuna majina “Tume ya Ardhi” yabadilishwe na majina “Waziri wa Ardhi”. Wakenya wengi walipata matatizo kwa miaka mingi waliyofanyiwa na Waziri wa Ardhi ndiposa wakasema kuwe na tume huru ambayo itaweza kutathmini suala la ardhi. view
  • 29 Mar 2016 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda, katika Kifungu cha 42 cha Mswada huu, wameondoa jopo ambalo liliwekwa katika kaunti zetu kutathmini masuala ya mashamba ilhali bodi hii iliwekewa watu ambao wametoka sehemu zile na wanajua masuala ya ardhi. Kifungu cha 44 cha Mswada huu kinazungumzia mambo ya dhuluma za kihistoria na kulikuwa na Mswada kamili ambao ulizungumzia mambo hayo. Sasa hivi, tumepewa maneno machache kuonyesha kwamba hizo dhuluma hazina umuhimu wowote ilhali hilo ni suala nyeti ambalo limeleta madhara. Kifungu cha 46 cha Mswada huu kinazungumzia kuwa Tume ya Ardhi itachaguliwa na Tume ya Kuajiri Wahudumu wa Umma. Itakuwaje tume ichague ... view
  • 29 Mar 2016 in National Assembly: mabadiliko katika Kenya yetu, tunapaswa kuangalia matakwa ya Wakenya katika Katiba yetu na tujue yalizungumzia nini. Matakwa ya Wakenya yamezungumziwa katika aya tofauti za Katiba yetu. Katiba inasisitiza kwamba suala la ardhi liachwe katika mikono ya tume huru lakini Mswada wote umebadilishwa na kila mahali penye tume huru pamewekwa Waziri wa Ardhi. Kwa takriban miaka 53, Waziri wa Ardhi aliachiwa suala la kutatua matatizo ya ardhi. Wakenya wamepata dhiki na madhila. Sasa hivi mambo ya kugawanya ardhi au kwa Kiingereza view
  • 29 Mar 2016 in National Assembly: ambayo yalikuwa katika Tume ya Ardhi yanasemekana yatapatiwa Waziri wa Ardhi. Yatarudi yale yale ya Waziri kukaa katika afisi yake Nairobi agawanye vipande vya ardhi awapatie awatakao na watu ambao wako mashinani katika makazi yale wakose ardhi. Hatutakubali katu. Ikiwa kweli tunataka kuambatisha sheria kwa mujibu wa Katiba, lazima tuwe wangwana na wakweli kama Wakenya kwamba hatutataka tena umwagikaji wa damu na kuona Wakenya wakifurushwa ovyo ovyo. Mswada wa Eviction Bill ulikuwa umetengezwa kupitia Land Act ambayo iko lakini hata Mswada huo pia umefanyiwa marekebisho na kuwekwa katika sheria hii kwa pamoja. Sheria hii imechanganya sheria nyingi na kuziweka pamoja. ... view
  • 29 Mar 2016 in National Assembly: Kwa hayo mengi ama machache, Wabunge wenzangu toeni macho hususan wale wanajua dhuluma za ardhi zimefanya nini Mkenya na dhuluma za ardhi zimesababisha maafa mangapi katika nchi yetu ya Kenya. view
  • 29 Mar 2016 in National Assembly: Asante sana. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus