Mishi actively participated in Likoni political campaigns in 1997 and 2002. She vied for Likoni parliamentary seat in 2007 and lost in party nominations which were marred by irregularities. She would like to see government funded drug rehabilitation centres established in Mombasa.
29 Mar 2016 in National Assembly:
Kutoka mwanzo, ninapinga.
view
23 Mar 2016 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nashukuru sana kupata---
view
23 Mar 2016 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Hata mimi nilikuwa hapa kitambo sana dada yangu Mhe. Fatuma. Kwanza, nataka kumshukuru Mhe. Wanga kwa kuleta Hoja hii ambayo ni muhimu sana kwa nchi yetu ya Kenya.
view
23 Mar 2016 in National Assembly:
Maradhi ya saratani ni sugu sana. Ni maradhi ambayo yamechukuwa maisha ya Wakenya wetu wengi, hasa akina mama kupitia saratani ya matiti na ya kizazi. Pia kwa wanaume, saratani ya kibofu imekuwa mbaya sana na imewapoteza akina baba wetu. Pia, vile vile, watoto wetu wengi wameweza kuangamia na kupoteza maisha yao kupitia saratani ya damu.
view
23 Mar 2016 in National Assembly:
Tatizo hili la maradhi haya limekuwa kwa sababu nchi yetu bado haijaweza kuwa na taasisi ama zahanati zinazoweza kupigana na maradhi hayo na kuweza kukimu wakenya wengi ambao wamepata hayo matatizo. Inabidi Wakenya wengi wasafiri kutoka sehemu mbali mbali za Kenya kwenda kwa hospitali yetu kuu ya Kenyatta ili waweze kupata matibabu, na zile huduma ambazo zinafanyiwa wagonjwa walio na saratani sampuli tofauti tofauti. Kuyatambua maradhi ya saratani imekuwa tatizo sugu kwa sababu madaktari wengi hawana taaluma ya kuyatatua. Hivyo basi, wagonwa wengi wanaotembea kwa hospitali ama zahanati zetu wanakumbana na utata. Kwa mfano, kwa akina mama, saratani ya matiti, ...
view
23 Mar 2016 in National Assembly:
. Ikiwa Serikali ingeweza kusambasa huduma kama hizo kwa hospitali za kaunti pale mashinani, basi hata wagonjwa hao wangeweza kupata afueni. Itakuwa vizuri kuliko kuwalazimu kusafiri hadi Hospitali ya Kenyatta ama kufanya Harambee kuchangisha fedha nyingi ili kwenda nchi za nje kutibu maradhi hayo.
view
23 Mar 2016 in National Assembly:
Maradhi kama hayo pia yanasababishwa na ndoa za haraka. Wasichana wetu wanapoozwa wakiwa bado mili yao haijakuwa tayari kuweza kuzaa ama kufanya ngono na wanaume, pia huleta matatizo kama hayo ya saratani ya kizazi. Hivyo basi, sisi kama viongozi pia lazima tuzungumzie swala la ndoa za haraka ili watoto wetu waweze kuiva na kuwa na uwezo wa kuolewa na kuzaa bila matatizo. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
23 Mar 2016 in National Assembly:
Vile vile, pia mambo ya ubakaji na kunajisi watoto wadogo pia inasababisha saratani ya kizazi. Hivyo basi, swala hili pia lazima tuliangalie sisi kama viongozi ili tulitatue. Maradhi ya saratani lazima yachukuliwe kama ya Ukimwi. Hayo maradhi yamekuwa ni janga na Serikali imeweza kuweka bajeti ya kitaifa kushughulikia watu ambao wana matatizo ya Ukimwi. Hivyo basi, wanaweza kupata madawa bure na wauguzi ambao---
view
17 Feb 2016 in National Assembly:
Asante sana, Naibu Spika wa Muda. Kwanza, ninataka kumpatia kongole Mhe. Mwaura kwa kuileta Hoja hii ambayo ni muhimu sana katika maisha ya ndugu zetu walemavu.
view
17 Feb 2016 in National Assembly:
Walemavu katika nchi yetu ya Kenya ni takriban asilimia 15. Hawa wanaishi na ulemavu tofauti tofauti. Pia, tuzingatie ya kwamba ulemavu ni kwa njia nyingi. Wengine wana ulemavu wa macho, wengine wana ulemavu wa masikio na wengine wana ulemavu wa vyungo tofauti tofauti. Katika Katiba yetu ya Kenya, katika kifungu cha 54(c) kinazungumzia umuhimu wa kuwezesha walemavu waweze kutembelea maeneo tofauti tofauti bila matatizo, waweze kupata usafiri bila kuwa na matatizo na pia waweze kupata habari au kupashwa habari bila kuwa na matatizo. Jambo hili haswa la habari naona ni changamoto kubwa sana. Lakini najua Mhe. Mwaura pia ana Mswada ...
view