Hon Mishi Juma Khamisi

Mishi actively participated in Likoni political campaigns in 1997 and 2002. She vied for Likoni parliamentary seat in 2007 and lost in party nominations which were marred by irregularities. She would like to see government funded drug rehabilitation centres established in Mombasa.

All parliamentary appearances

Entries 311 to 320 of 404.

  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Pia nataka kusema ya kwamba ndugu zetu wengi walemavu katika taifa hili la Kenya ni masikini. Umasikini huu umesababishwa na yale maumbile walio nayo. Wengi wameshindwa kwenda shule au kwenda kwa taasisi za masomo kwa sababu ya kukosa vifaa vinavyohusika kuweza kuwasomesha wapate taaluma. Hivyo basi wamekuwa wakiishi katika maisha ya uchochole. view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Vile vile Katiba yetu inazungumzia zile sheria ama haki za kimsingi. Imezungumzia kuwa mtu hatabaguliwa kwa rangi, kabila, dini na pia ikasema walemavu pia hawatabaguliwa. Hivyo basi tunaona mpaka sasa walemavu katika taifa letu wamebaguliwa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Tukiangalia majengo yetu mengi haswa ya umma hayajazingatia suala kama hili. Katika benki zetu, hospitali na mahoteli yahajazingatia haya. Hivi karibuni nilikuwa na Mhe. Sen. Godliver katika warsha ya Kamati ya Bunge. Tulipelekwa kwa hoteli moja ambayo inaitwa Medina. Ilibidi tukose kufanya warsha ile kwa siku ya kwanza kwa sababu ukumbi wa mazungumzo ulikuwa umewekwa katika gorofa nambari nne na ilikuwa ni ngazi pekee na kulikuwa hakuna lifti. Basi ilibidi Seneta aweze kuteta sana mpaka ikabidi tuache kufanya warsha hiyo tukasema tuifanye siku ya pili. Ilitubidi tuifanyie nje ya hoteli. Hatukuifanyia kwa ukumbi wowote. Hivo basi hata sisi katika Bunge ... view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Taasisi ya ujenzi ya kitaifa tunayoita kwa lugha ya Kiingereza “National Construction Authority”, inatakikana iweke mikakati na sera mwafaka za kuhakikisha ya kwamba majengo yalioko sasa na majengo ambayo yatajengwa yaweze kufanyiwa ukarabati ama yafanyiwe miundo msingi ambayo itawezesha ndugu zetu waweze kutumia njia hizo pasipokuwa na matatizo. view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Najua Kenya imeingia katika mikataba mingi sana ya kiulimwengu katika kutetea haki za walemavu lakini shida ni kwamba hatujazingatia na hatujaweka mikakati na kanuni mwafaka za kuhakikisha sheria hizi tumezifuata kulingana na mikataba na pia kulingana na Katiba yetu. Ikiwa sheria hizi hazikufuatwa ama mtu amezigeuka, basi kutakuwa na sheria gani ama kutakuwa na hatua gani ya kumwadhibu mtu huyu ama shirika lolote ambalo litakuwa limekiuka mikataba kama hii? view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Itakuwa vizuri sana washikadau wote kama vile lile shirika la walemavu la nchi yetu kwa jumla, wale wanaangalia mipango ya miundo misingi ya nchi yetu ya Kenya, wale wanaoshughulika katika mambo ya uchoraji, kutoa mapu zile za kutengeneza mijengo katika nchi yetu wakihusishwa. Washikadau hawa wote kabla hawajatekeleza mambo yao katika bajeti zao, ni lazima wafikirie kwamba tuna walemavu hapa Kenya takribani asilimia 15. Hawa tu ndio wataweza kutusaidia sisi kama Wakenya na kuwezesha watoto wetu kupata haki zao za kimsingi. view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Watoto wetu wengi, haswa wale ambao hawasikii na wale walemavu wa macho wameshindwa kuona alama za barabara na kwenye majengo. Kunatumika alama za kuonyesha ya kwamba ikiwa unaenda huku unafuata upande fulani. Wakati alama na ishara hizo zinatengezwa hutambulika ya kwamba kuna wenzetu walemavu ambao hawataweza kusoma ama kuzitambua kama vile sisi tunavyoweza kuzitambua. Tunajua tumepata majanga mengi sana hapa nchini kwetu Kenya kutokana na matatizo haya ya kuwa tumeacha kuzingatia walemavu. Walemavu wengi huishia katika majengo ambayo pengine kumetokea moto. Anataka kukimbia atetee roho yake lakini unapata kwamba kutokana na majengo yalivyojengwa, mlemavu kama huyu atabakia pale kwenye kiti ... view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Sisi kama viongozi wa taifa hili la Kenya tunataka tuwe msitari wa mbele kuhakikisha kwamba sheria hizi kweli zimetekelezwa kwa sababu mara nyingi sheria tunazitunga na zinakuwa pale tu kama sheria. Mtekelezaji ni nani na ni nani atakayehimiza sheria zitekelezwe ikiwa kutakuwa hakuna watu wa kuhimiza sheria na kuweka msukumo thabiti wa kuhakikisha kwamba walemavu wana haki kama Mkenya mwingine yeyote? Walemavu hawatachukuliwa tu kwa sababu tumeingia katika mikataba ya kiulimwengu ama kwa sababu Katiba imependekeza hivyo basi sisi tunafanya tu kama kuonyesha. Ni lazima iwe ni haki yao ya kimsingi na ni jambo ambalo litafanywa kwa mikataba vile inavyotakikana. ... view
  • 19 Nov 2015 in National Assembly: Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kumshukuru Mhe. Nyokabi. Hongera. Ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu unaenda sambamba na Katiba. Kuiwezesha sheria hii kufanya kazi ni lazima tuwe na miumdo mbinu na miundo misingi ya kuwezesha elimu ya uraia iwe ni ya lazima ili Wakenya waweze kuelewa kila kitu na wapate ufahamu. Pia, elimu ya watu wazima ama adult education inafaa iboreshwe ili watu waweze kupata habari na ufahamu. Pia, tukipitisha Mswada huu, tutaweza kufanya maamuzi bora na kushiriki vyema katika miradi ya kitaifa, kuijua miradi ya Serikali Kuu na miradi ya serikali ya ugatuzi. Tutaweza pia kujua ... view
  • 7 Oct 2015 in National Assembly: Thank you, Hon. Temporary Deputy Chairman. I also want to support the amendment to delete the word “youth” and substitute therefor the word “Kenyans”. According to our Constitution, all Kenyans have a right to equal employment opportunity. So, if we put it as youth only, it will mean that there might be a time when there is an opportunity and the people who have applied are not the youth. It will be a problem at that particular period; we say Kenyans so that the youth and other people can access employment. I support that amendment. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus