Hon Mishi Juma Khamisi

Mishi actively participated in Likoni political campaigns in 1997 and 2002. She vied for Likoni parliamentary seat in 2007 and lost in party nominations which were marred by irregularities. She would like to see government funded drug rehabilitation centres established in Mombasa.

All parliamentary appearances

Entries 31 to 40 of 404.

  • 10 Nov 2021 in National Assembly: Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii nami niweze kuchangia Mswada huu wa marekebisho machache ya Mhe. Didmus. Nampatia kongole kwa kuleta Mswada huu ambao utatatua tatizo sugu sana. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 10 Nov 2021 in National Assembly: Kwa hakika, kama Wakenya, tunajua kuwa unapofika miaka 60, unastaafu. Kuna wale ambao hustaafu kabla ya miaka 60 ndiposa kukawa na mikakati ya s cheme ya pensheni . Lakini, kumekuwa na changamoto nyingi sana. Wakenya wengi wamepata shida sana mikononi mwa maofisa tofauti tofauti katika mradi huu wa pensheni . Kuna ile tunayoita kwa Kiingereza view
  • 10 Nov 2021 in National Assembly: ama kundi fulani ambalo linatumia ufisadi katika mambo ya pensheni . Imekuwa kwamba mpaka uhongane ama utoe pesa kadhaa ndiposa uweze kupata pensheni yako kwa wakati unaofaa. Ndugu yangu Didmus amependekeza siku 60 ambazo ni mwafaka kabisa kwa aliyestaafu aweze kupata pesa za pensheni . Tukiangalia changamoto zinazofanya hizi scheme za pensheni kuwa na matatizo, mara nyingi sana tunapata ule uwekezaji wanafanya ni duni ambao hauleti mapato. Suala jingine ni usimamizi wa hii pensheni. Kuna usimamizi mbaya, ikiwemo ufisadi. Hivyo basi, inakuwa changamoto kupata pesa za kulipa watu pensheni. Pia, kuna waajiri wengine ambao wanakuwa muflis, ama bankrupt . Mtu ... view
  • 10 Nov 2021 in National Assembly: upitie ofisi nyingine. Ukitoka huko, unaambiwa utengeze barua fulani. Ukimaliza hii, unatengeza hii. Yaani ni urasimu mwingi. Nashukuru sana ndugu yangu Mhe. Didmus Barasa. Mambo haya ya uwekezaji wa pesa za pensheni lazima yaangaziwe kitaifa. Iwapo kuna utaratibu wa pensheni lakini inazembea na inaonekana sio ya kusaidia Wakenya walioko humo, lazima Serikali iwe na njia ya kuwaadhibu wasimimamizi wale kwa kosa kama hilo. Mkenya hawezi kuwekeza pesa zake akijua muajiri atawekeza zaidi ili mapato yakija aweze kurudishiwa zile pesa za pensheni, lakini kumbe pesa zile zinatumika kwa kiholela na tunakuwa na changamoto sana katika mambo ya pensheni. Familia nyingi zimeathirika ... view
  • 10 Nov 2021 in National Assembly: Asante sana, Mhe.Naibu Spika wa Muda. Nami naunga mkono uteuzi wa Wakenya wanne, ikiwemo akina mama wawili na akina baba wawili. Namshukuru Mhe. Rais na kusema huu ndio mtindo wa kwamba tuwe na asilimia 50 kwa 50 ya akina mama kwa akina baba katika uteuzi. Mamlaka haya ni muhimu sana kwa sababu yatalinda wale wanunuzi ama kwa Kiingereza consumers. Pia itaangalia njia ya usawa katika mambo ya biashara na soko. Kwa sababu, wakati mwengine tunaona kuweko kwa mvutano katika mambo ya biashara ama soko. Haswa hapa Kenya tumeona ushindani wa Airtel na Safaricom. Kwa hivyo, mamlaka haya ni muhimu sana ... view
  • 10 Nov 2021 in National Assembly: Nataka kumshukuru Mhe. Rais pia kwa ile Tume ya Ubinafsishaji lakini niwaambie wale Makamishna tafadhali Bandari ya Mombasa isifanyiwe Ubinafsishaji. Kwa hivyo, naunga mkono Mswada huu na kuseme kuwa wakati huu akina mama nafikiri tumepata mavuno katika uteuzi. Mhe. Rais, mtindo ubaki huo huo na akina mama tuwe mbele katika nyanja za uongozi sawia na akina baba na sambamba katika maamuzi na ujenzi wa taifa la Kenya. Naunga mkono Mswada huu kwa sababu walioteuliwa wote katika tajiriba ya kielimu na ya uzoefu wa kazi wamefuzu. Pia, katika Sura ya Sita ya Katiba, hawana jinai wala makosa ya uhalifu. Hatukuona memorandamu ... view
  • 10 Nov 2021 in National Assembly: Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Sisi wazazi ambao tunajua umuhimu wakunyonyesha tunaunga mkono sana Ripoti hii kwa sababu lazima mtoto mchanga apate maziwa ya mama. Lakini pia kuna wakati kuna changamoto pengine mzazi amezaa mtoto lakini anakumbwa na changamoto za maradhi fulani hivyo basi anaambiwa na daktari asimnyonyeshe mtoto. Ama pia mzazi anazaa lakini maziwa yake ni kidogo, na hayamtoshelezi mtoto. Hivyo basi, lazima kuwe na maziwa mbadala yakumtoshelesha mtoto. view
  • 10 Nov 2021 in National Assembly: Naunga mkono Ripoti hii ya Kamati kwa sababu lazima kuwe na kanuni haswa za kuangalia kama maziwa mbadala yatasaidia mtoto na yako na madini yanayohusika na yanayohitajika. Pia sasa hivi tunaona katika soko kumetokea maziwa sampuli tofauti tofauti ambazo wakati tunapatia watoto zinaleta shida haswa shida za maradhi ya tumbo. Kwa hivyo, lazima tuwe na njia ya kuangalia kama hayo maziwa mbadala ambayo yameingia katika soko zetu ni yale ambayo yamemulikwa na kuangaliwa na madaktari - haswa wale wanaosimamia afya ya watoto - ili tuwakinge watoto wetu dhidi ya maradhi yanayotokana na maziwa hayo. Vile vile, lazima tuangalie bei kwa ... view
  • 21 Oct 2021 in National Assembly: Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 21 Oct 2021 in National Assembly: Kwanza, nataka kutoa shukrani na kongole kwa Mwenyekiti wa Kamati hii ya Leba na Ustawi wa Jamii. Pia namshukuru Mhe Abdullswamwad kwa kutetea wafanyikazi wa bandari ambao ni vijana wetu, akina mama na akina baba. Kwa hakika Kamati imeangalia sheria kwa sababu sheria ni msumeno. Yakata mbele na pia yakata nyuma. Wafanyikazi wa bandari wamekuwa wakichangia Hazina Kuu ya taifa na uchumi wa taifa letu la Kenya pakubwa sana. Wafanyikazi hawa, mbali na kuwa kulikuwa na Covid-19 ama Korona, walimenyeka na kung’ang’ana kabisa kuzalisha na kuhakikisha kwamba mapato ambayo yanaingia katika Hazina Kuu ya taifa hayakupungua wala kuwa machache kwa ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus