Hon Mishi Juma Khamisi

Mishi actively participated in Likoni political campaigns in 1997 and 2002. She vied for Likoni parliamentary seat in 2007 and lost in party nominations which were marred by irregularities. She would like to see government funded drug rehabilitation centres established in Mombasa.

All parliamentary appearances

Entries 41 to 50 of 404.

  • 21 Oct 2021 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 21 Oct 2021 in National Assembly: Kwanza, nataka kutoa shukrani na kongole kwa Mwenyekiti wa Kamati hii ya Leba na Ustawi wa Jamii. Pia namshukuru Mhe. Abdullswamwad kwa kutetea wafanyikazi wa bandari ambao ni vijana wetu, akina mama na akina baba. Kwa hakika Kamati imeangalia sheria kwa sababu sheria ni msumeno. Yakata mbele na pia yakata nyuma. Wafanyikazi wa bandari wamekuwa wakichangia Hazina Kuu ya taifa na uchumi wa taifa letu la Kenya pakubwa sana. Wafanyikazi hawa, mbali na kuwa kulikuwa na COVID-19 ama Korona, walimenyeka na kung’ang’ana kabisa kuzalisha na kuhakikisha kwamba mapato ambayo yanaingia katika Hazina Kuu ya taifa hayakupungua wala kuwa machache kwa ... view
  • 19 Oct 2021 in National Assembly: Thank you, Hon. Speaker. I, the undersigned, on behalf of the residents of Mwananguvuze Village in Timbwani Ward of Likoni Constituency, draw the attention of the House to the following: THAT, Mwananguvuze Village, which is located in Timbwani Ward of Likoni Constituency, is a pre-colonial centre that was started in 1860 and traces its roots to Mzee Rashid Mbaya Mwazara, who was born in 1830, as well as Mr. Ali Juma Mwangare, born in 1927, and Mr. Mohamed Hamisi Mbaya, born in 1929; THAT, the land registered as Plot No.120 in Mwananguvuze Village is currently home to over 12,600 residents ... view
  • 19 Oct 2021 in National Assembly: THAT, the residents have recently been informed of plans by Mr. Mahesh Jatantilal Haria to assume ownership of the land under unclear circumstances and evict the residents from their ancestral land; THAT, efforts to address these concerns through various agencies have been futile; and, THAT, the issues in respect of which this Petition is made are not pending before any court of law, constitutional or legal body. THEREFORE, your humble Petitioners pray that the National Assembly, through the Departmental Committee on Lands with the support of the National Lands Commission: (i) conducts a fact-finding mission to Mwananguvuze Village to ascertain ... view
  • 1 Sep 2021 in National Assembly: Asante sana, Mheshimiwa Spika kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuunga mkono Hoja hii maalum ambayo imetuleta leo kuzungumzia wateuliwa wanne katika Tume ya Uchaguzi na Mipaka. Naunga mkono kwa sababu wateuliwa hawa wamefuzu katika tajriba ya kielimu, uzoefu wa kikazi katika utawala wa umma, usimamizi wa sekta za umma na mambo ya kisheria. Pia wateuliwa hawa hawakuwa na dosari katika mambo yoyote ya uhalifu ama kuwa na hoja ambayo ingebadilisha maadili yao ya kibinafsi. Tumeona ya kwamba Mheshimiwa Uhuru amezingatia jinsia; Ameweka kina baba wawili na kina mama wawili. Hivyo ni kutuonyesha ya kwamba kule tunakoelekea tutaweza kupata asilimia ... view
  • 1 Sep 2021 in National Assembly: zake na hatujawahi kusikia dosari yeyote ama ufisadi wa aina yeyote katika kazi ambazo amezifanya. Mhe. Spika, ningependa kusema kuwa tunatakiwa kuweka sura ya Kenya kila tunapofanya uteuzi. view
  • 1 Sep 2021 in National Assembly: Asante sana, Mheshimiwa Spika. Nataka nikubali ya kwamba ni wakati mwafaka kuweka sura ya Kenya katika uteuzi wetu. Isitoshe, tunaposema tunataka kuweka sura ya Kenya, lazima tuzingatie ya kwamba kwa kihistoria kuna jamii au makabila ambayo yalikuwa yamesahaulika pahali pakubwa sana katika uteuzi. Hivyo basi, wakati Rais wetu anafanya uteuzi, ni muhimu afikirie na kuwapa nafasi nyingi sana makabila yaliyokuwa yametengwa na yale ambayo ni machache. Hii ni kwa sababu hivi leo ukifika Pwani, kuna makabila ambayo yametengwa; Digo, Duruma, Pokomo, na Bajuni. Wako Pwani lakini wametengwa zaidi hata kule Pwani. Hata tukija huku Bara, sehemu ambayo Mheshimiwa Spika wetu ... view
  • 12 Aug 2021 in National Assembly: Asante sana, Naibu Spika wa Muda. Hata mimi nasimama kuunga mkono Mswada huu ambao unataka kuleta marekebisho kwa sheria inayozungumzia bima ya afya ya kitaifa ndiyo Wakenya wote waweze kupata afya bora. Afya imekuwa changamoto sana kwa Wakenya wetu haswa tukizingatia kumekuwa na matatizo na maradhi sugu kama saratani, kisukari na COVID ambayo tunaita korona. Tunajua Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye ni Raisi wetu katika liwaza yake ama zile Shabaha zake Nne, moja ni kuhakikisha kwamba Wakenya wote wataweza kupata afya sawia hata matajiri. Tukiangalia nchi zilizostawi ulimwenguni, tunaona ya kwamba suala la afya limepewa kipau mbele. Ambapo yule maskini na ... view
  • 12 Aug 2021 in National Assembly: kwamba lazima yule mwajiri na mwajiriwa waweze kulipa kiwango sawia kilicho sawa. Lakini lazima tuzingatie ya kwamba kuna wajiriwa wengi Wakenya wetu ambao ni maskini na mapato yao ni machache. Utapata ya kwamba mtu anafanya kazi katika kampuni inayopata mapato makubwa, imestawi na ambayo inaweza kutoa mchango mkubwa katika kufidia bima hii. Ni bora iwapo kampuni kama ile ambayo ina uwezo zaidi na mapato yake yako juu, mchango wao uwe mkubwa zaidi ya yule aliyeajiriwa. Hii ni kwa sababu walioajiriwa wanapata mapato ya chini sana na hawawezi kupata sawia na ule mwajiri ambaye anafaidika zaidi kutokana na biashara ya ile ... view
  • 12 Aug 2021 in National Assembly: Hospital au Aga Khan na hizo hospital zingine ni za watu binafsi ambazo pia malipo yao yako juu sana. Hata ukiwa na kadi, haiwezi kukusaidia kulipa malipo kama hayo. Kwa hivyo, ningesema kwamba mambo haya yote lazima yazingatiwe sana. Vilevile katika Mswada huu tunajua pia kuna ufisadi ambao umekuwa ukitendeka katika Hazina hii ya Kitaifa ya Bima ya Afya. Lazima kuwe na mikakati ya kuangalia je ufisadi kama huu ambao watu wametumia njia fulani kuiba fedha kama hizi ambazo zingemsaidia Mkenya katika mambo ya afya iangaliwe kwamba mashimo kama yale yatazibwa na itaweza kuangalia kwamba hakutakuwa kamwe na mambo ya ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus