Mishi actively participated in Likoni political campaigns in 1997 and 2002. She vied for Likoni parliamentary seat in 2007 and lost in party nominations which were marred by irregularities. She would like to see government funded drug rehabilitation centres established in Mombasa.
3 Aug 2021 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Kwanza kabisa, natoa shukrani zangu za dhati kwa Mhe. Aden Duale ambaye wakati alikuwa Kiongozi wa Walio Wengi alileta sheria hii. Pia, natoa shukrani kwa kiongozi Mhe. Wangwe kwa sababu amesoma Mswada huu wa Waqf. Mswada huu umeletwa ili kuvuta ile sheria iliyokuwa inasimamia mambo ya Waqf katika taifa letu la Kenya. Sheria iliyokuwa mwanzo imeacha mikakati mingi sana ya kuongoza na kutumika kwa Waqf ama rasilimali ambazo zinasaidia katika jambo kama hili.
view
3 Aug 2021 in National Assembly:
Waqf ni rasilimali ama mali ambayo mtu, watu ama mashirika, wanatoa kukidhia mali hayo kwa haja ya dini ya Islam. Waqf huwa katika mikakati ya sheria za mirathi na sheria za sakada kwa mujibu wa dini ya Islam. Mara nyingi, kumekuwa na shida nyingi sana katika rasilimali ambazo zimetolewa kwa Waqf. Kule kwetu Mombasa, kuna majengo yaliyotolewa na watu kwa nia ya kusaidia katika misingi ya dini ya Islam. Kama alivyosema Mhe. Duale, pengine mtu anaweza sema kuwa kodi inayotoka kwa nyumba yake isaidie makadhi ama isaidie kulipa maustadi ambao wanafundisha madrasa tofauti tofauti katika sehemu fulani. Kuna watu wanatumia ...
view
3 Aug 2021 in National Assembly:
Tume ya Waqf itasaidia haswa kuleta ukweli ama accountability and transparency, vipi fedha ama mali kama ardhi na majengo ambayo yametolewa kwa Waqf yako, hali yaliyotelewa ama yanatoa mazao kiasi gani na kama mazao hayo yanasaidia jambo lilinuiliwa katika waqf. Kwa mfano, kule Mombasa, unapata nyumba ambayo imetolewa kwa Waqf lakini imekodishwa kufanya biashara ambayo ni kinyume na dini ya Kiislamu. Jengo moja kule Mombasa lilikodishwa kuweka kilabu kinachoitwa Salambo. Katika kilabu, kuna mambo ya pombe lakini katika dini ya Kiislamu, pombe ni haramu. Kwa hivyo, ni lazima kuwa jambo ambalo litanuiliwa ama biashara ambayo imetolewa kwa Waqf iwe katika ...
view
3 Aug 2021 in National Assembly:
wanazipeleka katika mambo ambayo hayakunuiliwa katika zile rasilimali zilizotolewa kwa Waqf. Wakati tunachagua wale trustees ama tunateua wale makamishna, ni lazima wawe ni watu ambao watawakilisha Waislamu. Waislamu wako katika pembe nyingi sana za taifa letu la Kenya. Hiyo pia itawakilisha makundi ama organisations ambazo zinatambulika kuwakilisha Waislamu ili ziweze kufuata misingi ya kidini pasi na kufuata misingi ambayo ni tofauti. Kwa muda mrefu, watu wamekuwa hawajui hesabu wala mapato ya rasilimali ama mali kama hizi ambazo zimetolewa kwa ajili ya Waqf. Sheria hii itaweka wazi na bayana kwamba katika rasilimali ama mali haya, mapato na mazao yake ni haya. ...
view
3 Aug 2021 in National Assembly:
Hon. (Dr.) Chris Wamalwa.
view
8 Jul 2021 in National Assembly:
Nilikasirika Naibu Spika wa Muda kwa sababu niliweka kadi yangu mbele ya watu wengi zaidi hapa, lakini sikupata nafasi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
8 Jul 2021 in National Assembly:
Nashukuru pia nimepata nafasi hii kidogo nami niunge mkono Mswada huu kwa sababu hata Pwani kuna sukari. Tulikuwa na kiwanda cha Ramisi ambacho kilikuwa kiwanda cha umma na kikafa hadi sasa. Ningependa kusema ya kwamba, bodi hii ambayo itatengenezwa itaweza kusaidi kuleta soko la sukari yetu hapa Kenya. Hivyo basi, kuboresha uchumi wetu wa kitaifa na uchumi wa wakulima wetu wa sukari.
view
8 Jul 2021 in National Assembly:
Vile vile, wale wenye cartels wanaoleta sukari haramu, sukari ambayo itakuwa na madhara ya kiafya katika taifa letu la Kenya, wanaweza kudhibitiwa kupitia bodi hii ambayo itakuwa imetengenezwa kuangalia majukumu kama hayo. Vile vile, katika mambo ya utafiti, ni vizuri kwamba tukifanya utafiti ili kuweza kuboresha mazao tuweze kupata mazao zaidi na tupate tofauti nyingi katika huu mmea wa sukari ama wa miwa, ili tuweze kupata sukari kwa kiwango cha hali ya juu sana.
view
8 Jul 2021 in National Assembly:
Vile vile, wakulima wetu kupata hisa hamsini na moja katika kampuni ambazo ni za watu binafsi na pia katika zile kampuni za kusaga, itawapatia nguvu sana wakulima wetu wa miwa. Hilo litakuwa ni jambo la kupunguza wale watu ambao wana ubinafsi katika mambo ya uchumi wa sukari. Vile vile, wakulima wengi hawajalipwa malipo ya fedha zao katika kilimo hiki. Hivi sasa, kupitia bodi hii ambayo itakuwa imetengezwa na sheria hii ya sukari ambayo inaitwa Sugar Act, hayo mambo yote hayatakuwa changamoto, bali litakuwa ni jambo la kuboresha mambo hayo.
view
8 Jul 2021 in National Assembly:
Hazina ambayo itakuwa imetengezwa kupitia ule ushuru ambao tunauita levy, itaweza kusaidia sana watu kuweza kuchukua mikopo na kufufua vile viwanda ambavyo vimekufa, ama vile ambavyo vimedorora katika wakati huu. Nataka niseme ya kwamba, sukari ni kilimo cha kuweza kuleta uchumi wa kenya kama kilimo cha kahawa na majani chai. Kwa hivyo, ni kilimo ambacho sisi kama taifa lazima tukichukulie kwa njia ya hali ya juu, ili tuweze kujenga ajira pia kwa vijana wetu na kuweza kuboresha uchumi katika county zetu haswa zile ambazo zina kilimo cha sukari ndiyo tuweze kuendeleza nchi yetu kwa pamoja.
view