Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1281 to 1290 of 1995.

  • 29 Dec 2020 in Senate: Vilevile katika Kifungu cha tisa, World Anti-Doping Agency (WADA) itakuwa taasisi huru katika nchi ambayo haitaegemea upande wowote kwa Serikali ama kwa shirika lolote la michezo katika kutekeleza jukumu lake. Hii ni muhimu kwa sababu bara nyingine itakuwa inalemea upande mmoja na federation fulani. Ina maana kwamba hawataweza kutoa uamuzi huru katika masuala muhimu kama haya. view
  • 29 Dec 2020 in Senate: Katika Kifungu cha 31, Sports Tribunal ama jopo la kusimamia masuala ya kesi za michezo limepewa uwezo wa kuangalia na kusikiliza kesi ambazo zinahusiana na ukiukaji wa sheria hii ya anti-doping . Hii ni muhimu kwa sababu masuala kama haya mara nyngine inabidi yapelekwe katika taasisi za kimataifa kama vile Court ofArbitration for Sport (CAS) Louisiana, Ufaransa, ambayo ni ghali. Vilevile sisi kama Wakenya hatuna uwezo wa kuchukua mawakili kwenda kusikiliza kesi kama hizo. view
  • 29 Dec 2020 in Senate: Taasisi hii ya Sports Tribunal imepewa jukumu la kuangalia therapeutic use view
  • 29 Dec 2020 in Senate: . Hizo ni zile dawa ambazo zinatumika kutibu magonjwa fulani ambazo pia zinaleta athari ya mtu kuonekana kuwa ametumia dawa za kusisimua misuli. view
  • 29 Dec 2020 in Senate: Hii itaipa nafasi Sports Tribunal yetu ili kusaidia kutatua masuala ambayo yanaweza kutatuliwa papa hapa nchini Kenya. Kama kutakuwa na suala lolote la kukata rufaa, rufani ile inaweza kufuatwa katika taasisi za kimataifa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 29 Dec 2020 in Senate: Taasisi hii pia imepewa jukumu la kuweka kanuni zake binafsi. Hawatatumia zile za kimataifa. Wana uwezo wa kuweka kanuni zao binafsi ambazo zitaweza kusaidia kuendesha kesi kwa haraka zaidi katika taasisi zile. view
  • 29 Dec 2020 in Senate: Bw. Spika, tumeona hii sheria inawalenga wana michezo ambao wanacheza michezo moja kwa moja. Hata hivyo matatizo yako pia katika hizi federation zetu za michezo. Ukiangalia, labda inayofanya kazi ya kuonenkana ni Athletics Kenya pekee. Ukiangalia kwa mfano, Football Kenya Federation ina matatizo chungu nzima. view
  • 29 Dec 2020 in Senate: Timu zetu zinazokwenda katika nchi za kimataifa kucheza michezo kama vile juzi Gor Mahia, walienda Algeria wakafungwa mabao sita kwa bila. Walienda bila kocha ambaye anasaidia timu ile kujiandaa kwa michezo ya kimataifa kama hii. Baada ya kuipitisha sheria hii, kuna haja ya kurejelea Sports Act. Tuangalie ni vipi tunaweza kuwasaidia wanamichezo wetu ili wasiteseke mikononi mwa walaghai ambao wanatumia f ederatio n kama vitega uchumi vyao binafsi. Bw. Spika, tukiangalia hapo nyuma, juzi tulipokuwa na kura ya Football Kenya view
  • 29 Dec 2020 in Senate: kuna wadau wengi ambao walilalamika kwamba hawakuhusiswa katika kura zile. Walikimbilia Sports Tribunal, lakini ilikiuka amri ambayo walikuwa wametoa awali kuhusiana na swala lile lile. Walisema kwamba kura inaweza kuendelea licha ya kwamba Sports Registrar alikuwa amesema kwamba FKF haijatekeleza yale masharti ambayo yalikuwa yamewekwa kama sheria kuhakikisha kwamba wanafanya uchaguzi ambao ni huru na wa haki. Bw. Spika, mbali na kuangazia wachezaji ama wanamichezo ambao wanahusika katika michezo moja kwa moja, iwapo tunataka kukuza michezo na kuinua vipaji katika nchi yetu, kuna haja ya kuangazia hizi federations kama vile utendakazi wao na jinsi wanatumia fedha. Bw. Spika, kulikuwa na ... view
  • 29 Dec 2020 in Senate: ambayo ililetwa ili kukuza michezo. Je, imetumika vipi mpaka sasa kuinua michezo? Kwa nini timu zetu kama hizi zinazoshiriki katika michezo ya kimataifa--- Kwa mfano, juzi Gor Mahia walipokuwa wanaenda Algeria, walikuwa na shida ya kupata tikiti za ndege kuenda kukaa kule kwa siku tatu ama nne kuhakikisha kwamba wanacheza mchezo ule. Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Naunga mkono hii sheria ambayo inakusudiwa na hii Anti-Doping Bill. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus