All parliamentary appearances

Entries 1 to 10 of 97.

  • 15 Jun 2017 in Senate: Mr. Temporary Speaker, Sir, I second. view
  • 14 Feb 2017 in Senate: Asante Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Marehemu Boy Juma Boy alikuwa akiniita “Sister Du”. Tukiwa hapa Seneti, kisima chetu ni kimoja kwa sababu ni wakati wa kiangazi. Kama ulivyo jionea jana, Sen. Boy Juma Boy alikuwa maji mafuu na mvuvi kafu. Ya malishoni haya letwi mjini. Lakini tungeyaleta hapa leo pasinge kalika. Tuna roho ya simanzi kuomboloze kaka yangu “Brother Du” Boy Juma Boy kwa huzuni. Bahati huwa ina tuangaza lakini huwa haitupi ahadi. Ingekuwa ina fanya hivyo tunge kuwa naye Boy Juma Boy. Tunafaa tujue kuishi vyema kama hapa Seneti. Kijiti kimoja hakijengi nyumba. Jana niliskia vizuri ... view
  • 28 Dec 2016 in Senate: Asante Bw. Spika kwa kunipa muda huu. Naomba kwanza kukushukuru kwa umahiri wako. Pia nawapa kongole wenzangu kwa ukakamavu wao. Kama unavyojua, yasemekana ngoma ya vijana haikeshi. Kwa hii ngoma ya leo ya hili Bunge la watu wazima, tumeonyesha umahiri wetu. Tumeonyesha kuwa sisi ni watu wazimu. Mtu mzima huwa hawashi. Mtu mzima huzima. Twatarajia tuwe na wakati mwema. Nchi yetu ni nzuri sana. Hakuna nchi ambayo yaweza kututosheleza sisi sote. Kwa hivyo twaomba tuwe na matarajio mema katika siasa. Twataka tuwe na amani nchini. Kama nilivyosema hapo awali, hakuna nchi ambayo itatutosha sisi sote. Tukitoka mbio hapa, ni nchi ... view
  • 16 Nov 2016 in Senate: Mr. Temporary Chairman, Sir, I think my Senator is in order because today, Kilifi County is full of--- view
  • 19 Oct 2016 in Senate: Bw. Spika, wiki mbili ni muda mrefu sana. Hakuna hata maji ya kunywa. Sijui kama muda huo ni mwafaka. view
  • 19 Oct 2016 in Senate: Bw. Spika wa Muda, wimbi mkali hufuatwa na shwari kwa sababu wimbi huwa na nguvu zaidi. Tumekuwa mbioni kama Seneti. Sasa ni fursa yetu kurudi nyumbani. Mimi ninafuraha kwa sababu nitakuwa nyumbani. Nimefurahi zaidi kwa sababu ndugu yangu Sen. Hassan amesema kwamba atarudi nyumbani ili awaeleze watu ukweli. Kule kwetu kuna ugonjwa ambao unaitwa ‘ongea, danganya mpwani’. Ugonjwa huo unashika macho na mtu wa Pwani huwa haoni vizuri anaposhikwa na ugonjwa huu. Niwajibu wetu kama viongozi kurudi nyumbani ili tuwaelimishe watu. Ugonjwa huo unaposhika macho, hata Serikali itengeneze barabara, mtu wa Pwani hataiona ile barabara. Serikali imeleta maendeleo mengi Pwani, ... view
  • 13 Oct 2016 in Senate: Bw. Spika, kwanza naomba kumpongeza kakangu, Sen. Haji. Ukweli ni kwamba mnyonge anyongwe lakini haki yake apewe. Mimi ni mzaliwa waVipingo. Jamii ya Makonde wanaishi Vipingo. Kwa hiyo, nitavaa junga niungane na jamii ya Makonde kwa sababu mimi nililelewa nao kule Vipingo. Makonde walikuwa wakikata makonge kule Vipingo. Tumekaa na wao Vipingo miaka mingi sana. Wazazi wao na babu zangu walikuwa wanafanya kazi mahali pamoja, Kwa hivyo, ni huzuni kubwa kuona mimi nimekuwa Seneta na niko hapa na watu wangu ambao tulicheza nao nikiwa mchanga hawana vitambulisho. Ningekuwa nimetoka nje, watu wangeshangaa labda imekuwaaje kwa sababu ni watu ambao tulilelewa ... view
  • 13 Oct 2016 in Senate: Bw. Spika wa muda, ninampa pongezi Sen. Kagwe. Unamwona ana simanzi nyingi anapotukumbusha kuhusu teknolojia. Naomba kutoa hongera kwa Serikali yetu. Kama unavyojua, akopaye deni akilipa huwa ameondoa lawama. Kwa hivyo, vile Serikali ilivyokuwa imeahidi kuwa itapaeana vipakatalishi kwa watoto wetu, hilo ni deni ambalo linaendelea kufutwa. Kama mama, ama mzazi na wale mama wengine, sote tuna raha kubwa kwa sababu watoto wetu wameondolewa ule mzigo wa vitabu waliyokuwa wanabeba hadi mwendo ukabadilika. Pia, walijipata wafupi kwa mzigo mkubwa wa vitabu, lakini teknolojia itapunguza ile bughdha ya kubeba mzigo mkubwa sana wanapoenda shule ama kurudi nyumbani. Bw. Spika wa Muda, ... view
  • 13 Sep 2016 in Senate: Bw. Spika, hakuna afaye akakosa mzishi. Naomba kuwauliza swali watu wa Kaunti ya Nyeri. Adhabu ya kaburi aijuaye ni maiti. Gavana alisema kuwa amekuwa mgonjwa na mara kwa mara hali yake ya kiafya haijakuwa ya kupendeza. Mara nyingi amekuwa nje ya kazi. Wakati alipokuwa hospitalini, nani alikuwa anamshikilia gavana wadhifa wake? Ni kama Bw. Gavana amebwaga zani. Ukibwaga zani, hubwaga zani kwake. Asante, Bw. Spika. view
  • 14 Apr 2016 in Senate: On a point of order Mr. Temporary Speaker, Sir. Is Sen. G.G. Kariuki in order to say that second and third wives are not supposed to inherit his money? view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus