28 Oct 2015 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, chemotherapy machines normally destroy the normal body cells. That is why the appointments are not as frequent as maybe Kenyans would like them to be.
view
28 Oct 2015 in Senate:
Bw. Spika, nami nakuunga mkono nivae hii njuga nikaribishe viongozi wangu wa Kaunti ya Kilifi na wale wa Kaunti ya Vihiga.
view
28 Oct 2015 in Senate:
Bw. Spika, nivae njuga.
view
28 Oct 2015 in Senate:
Bw. Spika, pia mimi navaa njuga kukaribisha viongozi wa Kaunti za Kilifi na Vihiga. Ukiona mbari jua zinduna iko nyuma. Hili sio kundi la mwisho kuja kututembelea hapa. Ninawasihi watu wa Kilifi wajisikie nyumbani na wajimwage katika jiji hili. Mimi ni mmoja wenu na pia Seneta maalum. Watu wa Vihiga pia nawakaribisha. Tunaye Sen. Khaniri hapa. Yeye ni kiongozi wa maendeleo kabisa. Kwa hivyo, mjihisi nyumbani na wengine waje pia kwani mikono yetu i wazi kuwalaki. Karibuni.
view
28 Oct 2015 in Senate:
Asante Bw. Naibu Spika kwa nafasi hii. Ninampongeza Sen. Haji kwa huu Mswada wa Sheria. Mswada wenyewe umebobea kama mwenyewe. Hongera Sen. Haji. Ninatoa hisia zangu kuhusu mikasa ambayo inaweza kutupata. Wakati mwingine tunailaumu Serikali lakini kwa mfano pale kivukoni Likoni Ferry, kuna yale maboya ambayo yamewekwa kwenye ferry lakini hatujui kama yanafanya kazi. Ukiwa kwa ndege, unapata tangazo kwamba kuna boya chini ya kiti cha abiria lakini ni wangapi ambao wanaweza kulitumia kukitokea ajali? Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna wakati nilikuwa Budalangi na hakukuwa na mvua wala ishara yoyote ya kunyesha lakini vyombo vya habari vilisema kuna mvua ...
view
21 Oct 2015 in Senate:
Bw. Naibu Spika, nampa hongera Sen. Khaniri kwa kuleta jambo hili. Kitambulisho ni stakabadhi muhimu sana. Kule Kilifi, kuna vitambulisho vingi sana ofisini kwa chifu. Watu wetu hawajui pa kuvipeleka vitambulisho hivyo au labda watu hawana akaunti za benki au uajiri. Kamati hii ni lazima ihakikishe kwamba vitambulisho hivyo vimepewa wenyewe. Najua wengi wetu wataenda kuvitafuta kura itakapowadia. Kama kawaida, sisi huenda mbio dakika ya mwisho kutafuta stakabadhi za kutumia kupiga kura.
view
23 Sep 2015 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, we are the majority Members of the Committee on Health as you can see. Do not blame us; we are going to be organized.
view
23 Jul 2015 in Senate:
Asante sana Bi. Spika wa Muda. Namshukuru Sen. Orengo kwa kuleta Hoja hii. Mgeni njoo mwenyeji apone. Naomba kumkaribisha ndugu Obama hapa Kenya. Rais Obama ni kaka yetu na pia Rais wa Marekani. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
24 Jun 2015 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, I would like to thank Sen. Kagwe about yesterday’s happenings. We are supposed to be active and sober when the media is around. The Cabinet Secretary was being asked suggestive questions including the issue of Goldenberg and so on. The media will always report negative things. When you talk about Goldenberg, the media might think that the Cabinet Secretary was involved. When we call the media, we should know that those are outsiders and they like reporting negative things. Therefore, we have to be careful and accountable for what we say.
view
23 Jun 2015 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, I would like to thank the Chairman for the comprehensive Report.
view