11 May 2021 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, before you finished your Communication, you had mentioned something about the Third Reading. I wish we could stop the sun; we cannot. I wish we could stop the lunch hour; we cannot. However, we are ready to vote for the Third Reading. I am proposing to you, under Standing Order Nos.31 and 1 that you call Committee of the Whole and Third Reading, so that we can vote and leave this Chamber after finishing business altogether. Owing to its momentous position and what we are doing today, I do not see the reason we should take a ...
view
11 May 2021 in Senate:
.: Hoja ya nidhamu, Bi. Naibu Spika. Ninamuomba Kiongozi wa Walio Wengi atusikize kwa makini. Hili sio jambo la kupuuza. Ninaomba iwapo ingewezekana Hoja hii ingechapishwa kwa Kiswahili katika Orodha ya Shughuli za Bunge. Kisha, Kiongozi wa Wengi pamoja na yule atakayemuunga mkono, waendeleze Hoja hii kwa Kiswahili. Rais Suluhu alisema anafurahia Kiswahili chetu kwa sababu kiko na ucheshi. Kwa hivyo, ni wakati wetu na jukumu letu pia tujadiliane Hoja hii kwa Kiswahili. Nakala niliyonayo hapa imeandikwa kwa Kiswahili. Ninashangaa kwa nini Kiongozi wetu anaanza kwa Kingereza ilhali nakala ambayo anataka tuunge mkono imeandikwa kwa Kiswahili. Je, huu ni ungwana?
view
11 May 2021 in Senate:
Asante, Bi Spika wa Muda. Kwanza ninamshukuru Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa Hotuba yake ambayo imeleta maridhiano. Kwa jamii ya Watanzania ndugu zetu tukubalie tuendelee kuwapatia risala zetu za rambi rambi kwa kumpoteza kiongozi wao, Rais John Pombe Magufuli. Mungu amrehemu na amlaze mahali pema peponi. Jambo ambalo Rais wa Tanzania alifanya au Hotuba ambayo alitoa imekomboa mambo ambayo yamewashinda wanaume. Viongozi wanaume wameshindwa kuleta uwiano katika Afrika Mashariki. Imebidi mwanamke awaonyeshe viongozi wanaume njia. Jambo hili ni la muhimu. Wale ambao kama sisi tunapigia debe Mswada kama ule ambao tumepitisha leo. Ni kwa sababu katika maoni ...
view
11 May 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
11 May 2021 in Senate:
Tunataka tuwe na kampuni moja ya ndege kama vile tulikuwa na kampuni moja ya ndege zamani. Pia, tunaweza kuwa na kampuni ya reli na kampuni za vitu vingi hata mawasiliano kama ilivyokuwa kabla ya Jumuiya hii kuvunjiliwa mbali mwaka wa 1977. Je, ni kwa nini? Ndio kwa sababu tunasema uongozi umelegea. Tungekuwa na mtu kama Rais Suluhu kabla hatujafanya mkataba wa ujenzi wa reli tulioufanya na Wachina, ambayo inapitia kwako, ingekuwa rahisi. Deni hili ambalo tuko nalo na hawa Wachina halingekuwepo. Bi Spika wa Muda, hivi maajuzi nilitembelea nchi ya Dubai. Nimesikia kwamba wamefungua bandari yao Tanzania ili wafanye biashara ...
view
11 May 2021 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, bandari yetu kuna dock au kizimbani . Kuna mfanyibiashara mashuhuri ambaye amekomboa sehemu ya kufanyia biashara. Sisi Wakenya tumeshindwa kutafuta mtu ambaye tunaweza kuungana naye ili tufanye public privatepartnership katika bandari ya Mombasa ili tuimarishe huduma. Wafanyibiashara wengi wanahamia Rwanda au Tanzania. Ni lazima tujiulize ni kwa nini wanafanya hivyo. Mimi hupenda sana kuwaona wanyama wa porini. Kuna wakati nilienda pamoja na familia yangu Tanzania kuwaona wanyama. Tulienda Manyara, Ngorongoro, Kirawira na Mbuga ya Wanyama ya Serengeti. Nilishangaa kuona sehemu ambazo mbuga za wanyama zimetengewa ili kudumisha sekta ya utalii. Bei za hoteli za Kirawira, Serengeti, ...
view
11 May 2021 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, mimi ninaona kama ni malaika ametumwa ili tufanye hii kazi. Nimetumia barabara aliyozungumzia inayotoka Voi hadi Mwatate. Hiyo barabara ilikuwa mbovu sana na kuna sehemu za utalii za kifahari. Wale ambao hamjatembea sehemu hiyo kuna hoteli maarufu inayoitwa Salt Lick Safari Lodge. Kuna mahali pa kifahari ambapo hema hutengenezwa huko Mwatate. Mnaweza kutembelea sehemu hiyo ukielekea Tanzania wakati barabara hiyo itakamilishwa. Waheshimiwa maraisi hawa wawili wamesema watajenga barabara hiyo ili kuimarisha mawasiliano kati ya wananchi wa mataifa haya mawili. Kutoka Arusha hadi Manyara ni karibu kilomita 500 au 600. Hakuna babarabara yoyote kama hiyo nchini Kenya. ...
view
11 May 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
11 May 2021 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, zamani Watanzania walikuwa wanaambiwa waje Kenya ile waone dunia. Sasa ni wakati wetu kwenda Tanzania ili tuangalie nchi ambayo inaendelea kudumisha uchumi wake kwa njia ambayo inafaa.
view
11 May 2021 in Senate:
Kuna jambo lililotajwa kwenye hotuba hii kwamba kule Tanzania kuna Kilonzo, Kioko na Maasai. Hii inamaanisha jamii za Tanzania na jamii za Wakenya mpakani ni familia moja. Wakati babake Gavana wa Makueni aliaga dunia mwaka 2014, tumlimzika karibu na Ziwa Chala, upande wa Tanzania. Tulipikiwa mapochopocho ya ajabu na Wanyamwezi. Walikuwa wametengamana na Wakenya.
view