25 Mar 2015 in National Assembly:
Wakati wowote mtu anautata kuhusu lugha ambayo angependa kutumia, Kipengele cha 50 cha Katiba yetu kimesema kuwa ana haki ya kuhakikisha kwamba kuna mkalimani ambaye amelipwa ndio sheria itafsiriwe kwa ile lugha ambayo anaelewa zaidi. Umuhimu wa kuhakikisha kwamba lugha ya Kiswahili imetumika, ni jambo ambalo ni lazima tuliangalie kwa karibu.
view
25 Mar 2015 in National Assembly:
Kwanza, mawasiliano yatakua mema kati ya wale wote ambao wanahusika katika utumizi wa maswala ya kisheria. Mengi yamezungumzwa hapa kuhusu vile mawakili na baadhi ya watu hutumia lugha hii ya Kiswahili kujiletea utajiri. Nikionekana labda natetea mawakili hawa, kati ya matawi yote ya kiserikali yakiwemo hasa mahakama, na ambayo hasa mara nyingi utata wa lugha hii hutokea, kuna umuhimu wa kuhakikisha kwamba mahakimu wetu mara kwa mara, wanapelekwa katika warsha ndio waelewe vile maswala kama haya yanaendelea. Kwa hiyo, ningependa kusisitiza kwamba kuna haja ya kuhakikisha kuwa hata askari wetu ambao mara nyingi ndio huwa vianzilishi vya kesi hizi, wanafahamu ...
view
25 Mar 2015 in National Assembly:
Ningependa pia kuungana na wenzangu.
view
25 Mar 2015 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, kongole zangu kwa Mhe. Wanga kwa kujaribu kunena Kiswahili ambacho tunakitazamia. Ningetaka kumalizia kwa kusema kuwa katika jamii zetu, swala la watu kusoma Kiswahili limekua shida sana. Kuna watu wengi sana ambao Kiswahili hawakielewi. Kwa hivyo, ningetaka kuungana na wanenaji wenzangu ambao wamesema kuwa kuna haja ya kuhakikisha kwamba ile elimu ya watu wazima ambayo imekuwa ikitolewa imeregeshwa ndio watu waweze kurudi shule ili wapate mafunzo na wahakikishe wameelewa maswala haya.
view
18 Mar 2015 in National Assembly:
Shukrani, Bi. Naibu Spika wa Muda kwa fursa hii. Nilikuwa nafanya ushauri wa karibu na mhe Kamoti.
view
18 Mar 2015 in National Assembly:
Mhe Naibu Spika wa Muda, ningependa kuchukua fursa hii kuunga mkono Hoja hii. Nampa shukrani zangu mheshimiwa Kigo Njenga kwa kuleta masuala The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
18 Mar 2015 in National Assembly:
haya. Kinachonivutia zaidi katika Hoja hii ni kwamba inapendekeza tuanzie mashinani. Hoja hii imezungumza hasa kuhusu watoto wetu wa shule. Hii ni ishara kwamba tunaenda kuambatana na yale wahenga walisema, kwamba ni lazima samaki tumkunje angali mbichi. Tunazungumza kuhusu masuala ya pombe, hasa pombe ambayo haijahalalishwa na sheria. Sijui kama mheshimiwa Kigo alikosea, lakini alisema kwamba pombe ya mnazi ni baadhi ya zile pombe haramu. Nataka kusawazisha maoni haya. Mnazi si haramu. Pombe hii inatoka kwenye mti aina ya mnazi na haina matatizo yoyote.
view
18 Mar 2015 in National Assembly:
Ningependa kusema kwamba unywaji pombe, hasa miongoni mwa vijana, umedidimiza uchumi sana. Vijana wanapoingilia unywaji pombe wanakosa kujihulisha na masuala ya maendeleo. Hivyo basi ni kweli kwamba kuna haja ya NACADA kujizatiti zaidi kwa kuibua mbinu mwafaka ambazo zitahakikisha suala hili linashughulikiwa vilivyo. Tatizo hili halihitaji tu suluhu kutoka kwa Serikali peke yake. Hili tatizo ambalo linatuhitaji sisi viongozi na wazazi kulitilia maanani. Hoja hii inazungumzia hasa matumizi ya pombe haramu katika miji yetu. Sharti tukubali kwamba jinsi tunavyoishi makwetu ni muhimu. Kwa mfano, si vema kuwatuma watoto wadogo dukani kununua pombe. Wazazi wakome kufanya hivyo. Sharti tuhakikishe tumewaonyesha watoto ...
view
18 Mar 2015 in National Assembly:
Ni muhimu walimu wetu wachangie katika kukuza watoto wetu kwa njia nzuri. Najua haya masuala yako kwenye syllabus ambazo walimu wanafuata. Ningependekeza kwamba washikadau wote wahusike katika kutatua tatizo hili. Lazima wahusike kwa njia nzuri kwa sababu kama suala hili halitaangaziwa vyema, huenda ikawa tumefungua nafasi ya baadhi ya watu kuleta ufisadi. Mimi ninaamini kunazo sheria ambazo zinadhibiti unywaji pombe. Ni sheria ambazo zikifuatwa kwa njia nzuri basi hatutakuwa na matatizo kama yale yamezungumziwa na wanenaji wenzangu.
view
18 Mar 2015 in National Assembly:
Kwa hivyo, ninaiunga mkono Hoja hii. Ningependa kwa mara ya pili kumshukuru mhe. Kigo kwa kuileta Hoja hii. Ninaiunga mkono.
view