All parliamentary appearances
Entries 191 to 200 of 1513.
-
5 Jun 2018 in National Assembly:
Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii niongeze sauti yangu kama wenzangu walio tangulia kuzungumza juu ya suala la Hotuba ya Mhe. Rais aliyohutubu hapa Bungeni na nchi nzima. Ukweli ni kwamba suala hilo lipo ndani ya Katiba. Alikuja kuhakikisha kuwa amewakilisha Hotuba hiyo ambayo ni muhimu kulingana na Katiba yetu. Tunatarajia kila wakati tukifungua Bunge jipya, Mhe.Raisa atahutubia nchi.
view
-
5 Jun 2018 in National Assembly:
Ningependa kuangazia masuala mawili. Suala la kwanza ni kuhakikisha kuwa Wakenya wanakaa kama kitu kimoja. Mhe. Rais mwenyewe alitutangulia kwa kuomba msamaha kwa Wakenya wote ili watu wasameheane baada ya kutoka kwenye siasa ambayo ilikuwa kali na ya kivumbi mno. Alianza kwa kushikana mkono na kiongozi wa Upinzani mwezi wa Machi. Alipokuja hapa pia alisukuma mbele suala hilo kwa kulizungumzia na hivi majuzi kwa maombi ya kitaifa, vile vile aliangazia suala la umoja na undugu wetu na umuhimu wa Wakenya kuwa kitu kimoja na kujua maana ya msamaha.

Jambo la pili ni kuhusu ugonjwa wa ufisadi. Mhe. Rais ameamua kukabiliana nalo. Hapo awali, alianza vita hivi lakini vikapata misukosuko hapo katikati. Lakini sasa inaonekana kuwa vita vimeshika kasi. Ni lazima tupigane na ugonjwa huu na tuushinde, la sivyo, utaangamiza Kenya. Hivyo basi naunga mkono Mhe. Rais kwa kazi nzuri anayofanya na vile vile kuhakikisha kuwa pesa ambazo zinazotumika zisifujwe ovyo ovyo. Naona ameingilia kwa upande wa wafanyakazi wa Serikali kuwa ni lazima wafanye kazi vile inavyotakikana haswa wale wanaohusika kwenye shughuli za kuhakikisha kuwa kandarasi zote zinazopeanwa katika idara mbali mbali tofauti za Serikali ziweze kufaidi wananchi.

Kama wenzangu walivyotangulia kusema, jambo hili lifanywe na amelianza vizuri lakini watu wengine wasilitumie kama njia ya kuwaondoa wenzao kazini ama kuumizana kikazi ama kwa kulipana kisasi. Tunaomba kuwa suala hilo lifuatiliwe kabisa kwa kihakika na kila mtu apate haki yake. Lakini wale ambao watakaopatwa wamefuja pesa za umma, haswa wenye The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.

kupeana kandarasi kiholela holela ama kiovyo ovyo, ni lazima wapate adabu. Adabu yenyewe ni kupelekwa kortini na kuhakikisha kuwa mahakama pia imefanya kazi kwa upande wake. Vita hivi haviwezi kushindwa na mtu mmoja. Ni lazima zote tuungane pamoja tumuunge Mhe. Rais mkono, haswa sisi Wabunge wa Bunge la 12 na tumpe motisha ya kuendelea na vita hivi. Vita vya ufisadi sio vita vyepesi. Ni vita vizito. Vinahitaji sisi zote kushikana na kiongozi wetu ili tufanye kazi pamoja.

Nampea pongezi na hongera zangu Mhe. Rais kwa sababu sasa hivi tumepata habari kuwa akina mama wawili, Binti Kanze Dena pamoja na Munira Mohamed wamepatiwa kazi kwenye cheo cha juu. Binti Kanze Dena amechaguliwa kuwa naibu mzungumzaji mkuu wa Mhe. Rais. Nawapongeza na kumpa hongera Mhe. Rais. Asante sana kwa kutupatia nafasi hiyo kama akina mama tuweze kufanya kazi hizo.
view