All parliamentary appearances
Entries 501 to 510 of 1513.
-
17 Dec 2015 in National Assembly:
Ukiangalia stakabadhi za Lilian Omollo zinaonyesha kuwa ana ujuzi na anaweza kazi. Hivyo basi, ninaunga mkono nikimtakia kila la heri, na ningependa alete ujuzi na haswa, yale mafunzo aliyopata huko upande wa Nyanza katika Serikali ya Jubilee ili aweze kutuonyesha na kutuwezesha kufanya kazi kama Wakenya kwa ujumla. Ninaunga mkono.
view
-
17 Dec 2015 in National Assembly:
Thank you, Hon. Speaker. I rise to second the nomination of Dr. Nicholas Muraguri as the Principal Secretary for the Ministry of Health.
view
-
17 Dec 2015 in National Assembly:
I sit in this Committee. Dr. Nicolas Muraguri has been the Director of Medical Services and the main technical advisor to the Jubilee Government. He has a lot of experience in terms of what he is already doing. He holds two Masters Degrees, as we have already been told. More so, he had a stint at the United Nations, where he worked for three years in UNAIDS. Combining all that, he has all it takes to be the PS and to work to influence the policy of Government in terms of health for Kenyans. Dr. Muraguri is quite young but ...
view
-
17 Dec 2015 in National Assembly:
With those remarks, I beg to second.
view
-
17 Dec 2015 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika. Pia nami nataka kuunga mkono Hoja hii haswa kwa sababu ufisadi umekuwa kidonda sugu hapa Kenya. Ufisadi umekuwa kama ugonjwa wa saratani ambao unakula nchi chini kwa chini.
view
-
17 Dec 2015 in National Assembly:
Mhe. Rais ameanzisha vita dhidhi ya ufisadi. Bila shaka, Philip Kinisu akiwa kama Mwenyekiti, Dr. Dabar Abdi akiwa kama mmoja wao, Paul Mwaniki, Sophia na Rose Mghoi, wote hao wanaonekana kuwa wako na kazi ngumu ya kufanya. Lakini kazi wanaokwenda kufanya ni kuwezesha Mhe. Rais kupigana na vita hivyo na kupunguza ufisadi hapa nchini, ili Wakenya waweze kufurahia maendeleo ya nchi hii pasipo na ufisadi.
view
-
17 Dec 2015 in National Assembly:
Ukiangalia shahada zao, ni sawa kabisa. Ukiangalia kazi zile walizozifanya, zimewawezesha kufika pale walipo. Vile vile, ni Wakenya wanaofaa. Ukiangalia pia upangaji wao, ni watano tu. Lakini Mhe. Rais amejaribu kupanga kila eneo la Kenya ili vita dhidi ya ufisadi viwezekane.
view
-
17 Dec 2015 in National Assembly:
Mwaka huu ulikuwa mgumu kwa Wakenya wote. Lakini mwaka pia ulikuwa na mafanikio maanake tuliona Rais wa Merikani akitutembelea na tukamuona Baba Mtakatifu wa Kikatoliki akija kututembelea. Bila shaka, tutafunga mwaka tukiwa na baraka nyingi sana ili mwaka ujao, vita hivvo viwe vimewezekana, ili tuweze kushinda ufisadi.
view
-
17 Dec 2015 in National Assembly:
Tunavyoelekea wakati wa Krisimasi, nawatakia Wakenya Krismasi nzuri na mwaka mpya ulio na mafanikio. Tutaweza vita dhidi ya ufisadi mwaka unaokuja.
view
-
17 Dec 2015 in National Assembly:
Naunga mkono.
view