Ramadhan Seif Kajembe

Born

3rd May 1944

Post

P.O. Box 88031, Mombasa, Kenya

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

langoni@swiftmombasa.com

Email

Changamwe@parliament.go.ke

Telephone

0722414707

Telephone

0721609777

All parliamentary appearances

Entries 81 to 90 of 516.

  • 15 Feb 2012 in National Assembly: Bw. Spika, kwanza, ninataka niseme kwamba sijapotosha Bunge. Pili, ninataka niseme kwamba Wizara yangu na kamati inayohusika na mambo ya mazingira, tulikubaliana tufanye mkutano Kisumu na Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira akamtuma mwakilishi wake. Hawa Wabunge ambao wanasema wanahusika zaidi – na mimi ninaamini kuwa wanahusika – wote walikuwa wana kazi Nairobi na wakatuma mwakilishi wao! Walimtuma--- view
  • 15 Feb 2012 in National Assembly: Bw. Spika, ninasimama kidete kusema kwamba Wabunge walialikwa na wakatuma mwakilishi wao kule Kisumu ambaye alikuwa Mheshimiwa--- Mheshimiwa yuko pale! view
  • 15 Feb 2012 in National Assembly: Bw. Spika, ile kamati ya mazingira na Wabunge hawa, tuliwaalika na nina ushahidi. Mheshimiwa Outa pekee aliyekuja pale akasema; “Wale Wabunge wenzangu mumewaalika, lakini wako na shughuli zingine. Kwa hivyo mimi ninawawakilisha na tutazungumza.” Tulizungumza na tukaelewana! view
  • 15 Feb 2012 in National Assembly: Bw. Spika, Ziwa Victoria zinasimamiwa na nchi tano nazo ni Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi. Swala la kurekebisha Ziwa Victoria hupitiwa tu katika Baraza la Mawaziri wa Mazingira wa Afrika Mashariki. Swala hili limezungumzwa vya kutosha na kuna mkataba ambao umefikiwa kati ya nchi hizi tano za Afrika Mashariki, kwamba Benki kuu ya Ulimwengu itatoa pesa katika mafungu manne ili kuondoa hii kwekwe katika Ziwa Victoria. Pia, serikali zinazohusika za Afrika Mashariki zilipewa nafasi yao, kwamba zitaongeza pesa kusafisha hii Kwekwe. Mpaka sasa, Benki Kuu ya Ulimwengu imetoa Kshs178 milioni wakati tunangoja pesa nyingine za Serikali kuu. Hata hivyo, ... view
  • 15 Feb 2012 in National Assembly: Lakini ninataka uniruhusu, Bw. Spika, niseme kuwa wakati Bw. Outa alikuwa pale, zile kamati zimeweka hii kandarasi kutengezwa katika sehemu za Waheshimiwa Wabunge, alilalamika kwa kusema zile kamati zingine hazikuwajulisha Wabunge wao na nikatoa agizo, kama Waziri Msaidizi wa Mazingira, kwamba wakati huu pesa hii ikija, badala ya Waheshimiwa Wabunge kuwaachia kamati katika maeneo yao ya ubunge, Wabunge watawakilishwa kikamilifu. Nimetoa amri hiyo, Bw. Spika, na itafuatwa. view
  • 15 Feb 2012 in National Assembly: Bw. Spika, mimi pia nimesikia maneno hayo, kama alivyosikia Bw. Wamalwa, lakini sina chembe chembe za kitaalam kuhusika na utengenezaji wa majeneza kutumia kwekwe hii. Lakini ninataka niseme kuwa katika vikao vyetu katika Wizara, tumeligusia jambo hili na wataalamu wetu wanajaribu kuzungumza. Tumewaambia watuletee taarifa kamili juu ya swala hili. view
  • 15 Feb 2012 in National Assembly: Bw. Spika, katika majibu yangu hapo awali, nimesema kwamba hivi karibuni, tutatangaza yule ambaye atachukua kandarasi kutengeza hii njia na hili daraja. Katika majibu yangu hapo awali pia nilisema kwamba tayari tumeweka mtaalamu kutupatia bei, yaani consultant na amesema kuwa ripoti yake itamalizika mwisho wa mwezi huu wa February. Ninataka nikuhakikishie kuwa maneno hayo yanaharakishwa ili kwamba--- view
  • 15 Feb 2012 in National Assembly: Mhe Spika, labda lugha hazikuchuana, lakini nimesema kandarasi itamalizika kabla ya mwisho wa mwezi huu; mwisho wa mwezi huu tutatoa kandarasi ili sehemu ile ijengwe. Mhe Spika, nataka labda nifahamishe Bunge kitu, kwa ruhusa yako-- - view
  • 15 Feb 2012 in National Assembly: Asante. Nataka nifahamishe Bunge kwamba kazi ya kuondoa kwekwe katika Ziwa Victoria ni ushirikiano wa nchi tano na tuna mktaba na chi tano. Hakuna nchi moja inaweza kusema itafanya kazi kivyake. Jambo hili litasilishwa katika Baraza la Mawaziri. Kitu nataka kusema ni kwamba nazungumza kama Waziri Msadizi wa Mazingira. Ninamjulisha Mhe Rege kwamba mradi huu utatekelezwa haraka iwezekanavyo. Pia nataka niseme kwamba daraja liko na ninakubaliana na Wabunge kuwa haliko katika hali nzuri. Litatengenezwa na nataka nikwambie nina fedha; kama litaangukiwa na mmonyoko wa udongo tutaundoa mmomonyoko wenyewe. view
  • 15 Feb 2012 in National Assembly: Mhe Spika, narudia tuu. Jawabu langu ni kwamba Wizara yangu inakubaliana na Wabunge kwamba daraja limezoroteka. Pia nimesema kwamba pesa zilizotumika Kshs 178 million kulikuwa na wataalamu ambao walikuwa wameshikana na kamati katika maeneo ya ubunge ya hawa Wabunge. Nakubaliana nao kwamba hawakushirikishwa wakati wa kutumika kwa pesa hizo; hawakushirikishwa katika utendaji kazi huu. Lakini sasa nawahidi nikiwa mimi mwenyewe kwamba wakati huu pesa zikiingia nitawaita pamoja. Tutawashirikisha. Msiwe na shaka juu ya jambo hili. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus