22 Mar 2017 in National Assembly:
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Hotuba ya Mhe. Rais. Kwa kweli, taifa nzima lilikuwa linatarajia mengi kutoka kwa kinywa cha Mhe. Rais kuliko hata yale ambayo aliyazungumza. Kwanza, Wakenya walikuwa wanataka yeye kama Amiri Jeshi Mkuu atueleze hali halisi ilioko nchini Somalia ambako vijana wetu wa kike na wa kiume katika sare rasmi wanapoteza maisha yao. Pia, tulikuwa tunatarajia atakuja kuzungumzia idadi ya wanajeshi waliopoteza maisha yao kule ni wangapi, na wale ambao wameachwa bila waume wao wanasaidiwa namna gani. Vile vile, tulikuwa tunatarajia atueleze ameelekea vipi na Wizara ya Mambo ya Nje ...
view
22 Mar 2017 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, tukizungumzia habari ya stima ambayo Mhe. Rais alizungumzia, sasa shule nyingi zinakatiwa stima, zinakuwa kwa giza. Anasema kwamba yeye ameweka stima lakini shule nyingi zimeshindwa kulipa gharama ya stima. Shule nyingi zimerudi gizani. Hapo hajafuatilizia kujua hali halisi ilivyo. Akizungumzia kuhusu suala la barabara, sisi kwetu Mombasa tunasema, hata kama watu wanaona ni uchungu, hakuna barabara hata kilomita moja ama mbili ambayo imejengwa na pesa ambazo tunalipa kama kodi. Barabara zinajengwa kule karibu zote ni zile ambazo tunapata misaada na mikopo kutoka Benki ya Dunia ama Uingereza. Sasa, hapo ndio anasema ametengeneza barabara lakini kwetu ...
view
16 Nov 2016 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika kwa kunipatia fursa hii ili nipenyeze sauti yangu kwa Hoja hii muhimu. Nawasihi Wabunge wampitishe ndugu yetu Julius Ayub Githiri kwa haraka kwa sababu ni jambo ambalo linaathiri taifa hili pakubwa, hasa katika sehemu ya Kisauni ambayo naiwakilisha. Vijana wameathirika pakubwa na mambo ya dawa za kulevya na ni vyema sana tumpitishe mwenyekiti huyu haraka ili aingie na aanze kazi yake ya kuwasaidia vijana. Taifa hili kama ninavyojua liko mikononi mwa vijana ambao, kwa idadi kubwa, wanaendelea kuathirika kupitia kwa mambo ya dawa za kulevya na ulevi, hasa kama ilivyokuwa katika mikoa ya Pwani na Kati. ...
view
5 Oct 2016 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ingawa nilikuwa nimebonyeza kwa ile ya makavazi ya hayati Mzee Jomo Kenyatta, nitaendelea na hii pia ambayo imenifikia sasa.
view
5 Oct 2016 in National Assembly:
Ni vyema sana tupeleke viongozi wa dini katika shule zetu kwa sababu kulingana na hali ilivyo sasa, wanafunzi wanakua bila imani ya dini kwa sababu muda mwingi wanautumia wakiwa shule. Ni vigumu kwao kwenda katika madrassa au sehemu ambazo watafundishwa Biblia. Ni vyema sana viongozi wa dini zote wapelekwe katika shule. Wenye imani ya Kiislamu wapelekewe walimu wa Kiislamu kama maimamu ama masheikh. Wenye imani ya Kihindu na The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
5 Oct 2016 in National Assembly:
ya Kikristu pia wepelekewe walimu wao ili watoto wetu wakue katika mazingira ya dini, kupendana na huruma. Huo ndio wakati pekee ambapo mtoto akiwa shuleni aone dini imewekwa katika somo, atachukua na uzito. Kulingana na mazingira yaliyoko sasa mitaani, ni vyema sana watoto wetu wapate mafunzo ya kidini. Wanafunzi wakue katika maadili ya kidini kuanzia shule za chekechea, shule za msingi na zile za sekondari. Ikiwezekena, wakati mitihani inapotungwa, wawekewe maswali hayo ili wakifanya mtihani, waone umuhimu wake. Kila siku kabla hawajaingia madarasani, wawekwe katika sehemu za imani zao ili wafundishwe hali halisi jinsi dini inavyosema, aina ya upendo na ...
view
5 Oct 2016 in National Assembly:
Nilikuwa nimebonyeza kuhuzu suala la makavazi ya hayati Jomo Kenyatta. Itabidi nipenyeze neno moja ambalo halikuzungumziwa hapa. Katika makavazi hayo, kuwekwe taratibu za watu watakaoenda pale, wasiwe wataenda kumuomba kwamba awasaidie. Itakuwa kinyume na imani. Iwekwe sehemu ambayo watu wataomba Mungu kwa sababu hata tukiwaruhusu watalii waingie, kikubwa ambacho marehemu aliyetangulia mbele zake anahitaji ni maombi. Kwa hivyo, kuwe na sehemu ya maombi ambapo watu watakuwa wanamuombea. Kwa hayo mengi, ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda.
view
1 Sep 2016 in National Assembly:
Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili niweze kupenyeza sauti yangu hasa katika Hoja hii ya ushirikiano baina ya Serikali yetu ya Kenya na Uingereza kupitia muungano wa majeshi. Mimi nitaunga mkono Hoja hii ikiwa taratibu fulani zitafuatwa. Kwanza, wahakikishe kuwa mahali ambako jeshi hili litakuwa likifanyia mazoezi, zile silaha zote ambazo hazikulipuka zilipuliwe ili mahali pale pawe salama. Wakenya wengi sana wamepata ulemavu kwa ajili ya silaha ambazo Waingereza walitumia na kuchimbia chini ya ardhi yetu. Nazungumza haya kwa sababu nilikua askari kwa miaka tisa. Tumetembea sehemu nyingi ambako kambi za Waingereza ziko. Mabomu ...
view
1 Sep 2016 in National Assembly:
Kwa hiyo, madhara yanakuja kuliko faida. Kwa hivyo, tuwe na utaratibu na msimamo kama Serikali kwamba taratibu fulani zifuatwe ili tuweze kuwakubalia.
view
1 Sep 2016 in National Assembly:
Kwa hayo machache, nakubali na nakataa. Ikiwa taratibu zitakuwepo, nitakubali. Ikiwa hakuna, nitakataa.
view