All parliamentary appearances
Entries 31 to 40 of 286.
-
26 Nov 2019 in National Assembly:
Tans Nzoia, Marakwet and other places who have given out food. I have seen Kenyans are united and willing to help those in need. I do not wish to say much because I want to give time to my colleagues to speak on this issue.
view
-
26 Nov 2019 in National Assembly:
As a House, we need to think twice. As I have mentioned, the Deputy President did not go there as the Government, but as a human being. He saw the suffering that is why he gave out his helicopter to help.
view
-
26 Nov 2019 in National Assembly:
Exactly, Hon. Deputy Speaker. You put it right. Tomorrow, you can pick the Hansard. I have never said it. I did not even mention his name as an ordinary person, but I said he came there as a human being. He felt it. Why am I saying that? Do you want me now to go further?
view
-
12 Nov 2019 in National Assembly:
Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi ili pia nichangie Mswada ambao uko mbele yetu. Ninashukuru Mheshimiwa ambaye aliketi na akawaza na akaleta Mswada ambao tunaongea juu yake.
view
-
12 Nov 2019 in National Assembly:
Sisi wengine tumetembea na tumeona mengi. Ninatoka Kapenguria. Ukisikia Kapenguria, kuna wale wanaongea kuhusu “Kapenguria Sita”. Wakati niliingia katika Bunge la Nane, nilipata Mzee Mheshimiwa Paul Ngei akiwa anazunguka hapa akiwa kwa ile baiskeli ya
view
-
12 Nov 2019 in National Assembly:
The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
-
12 Nov 2019 in National Assembly:
kuzungushwa. Wakati unamtazama na ukiangalia historia ya Kenya kuhusu wale ambao walipambana mpaka wakafika pale, alikua mmoja wao. Baadaye nikaona Mheshimiwa Ochieng Oneko na Hayati Kenyatta. Ni jamii moja inayojulikana lakini wale wengine watano hakuna mtu anayetaka kuongea juu yao. Kwa hivyo, miongoni mwetu, kuna wale ambao hawajui bei ya petroli kwa sababu wanabebwa kila mahali na wengine. Wengine wetu hapa wanafanya biashara na Serikali na kuna wale ambao wanatoka hapa na kuenda kuhudumia watu wao. Sasa tusifike mahali pa kusema kwamba mtu aende ajitengenezee kwa sababu wengine tumefika hapa hivi. Kusema hivyo, kwa njia nyingine, ni matusi.
view
-
12 Nov 2019 in National Assembly:
Hivyo basi ninataka kuunga mkono na kusema kwamba wenzetu ambao wamekuwa hapa wamekuja kutusikiliza. Mimi nilikuja hapa katika Bunge la Nane na mshahara ambao nilianzia kulipwa ulikuwa Kshs150,000. Wengine waliniambia kuwa nilikuwa na bahati kwa sababu mshahara ulikuwa umeongezeka. Watu walikuwa wamefurahi sana. Ukitaka kuchukua mkopo hata wa kununua gari au kujijenga au kusaidia familia yako ama waliokuchagua, ilikuwa ngumu. Sisi kama Wajumbe ambao tuko hapa, Mungu ametupenda na akatuleta hapa, na watu wetu pia Mungu akawasababisha kutuchagua, tusije tukaweka wenzetu vibaya. Leo ni wao na kesho atakuwa mwingine hapa hivi.
view
-
12 Nov 2019 in National Assembly:
Mimi pia wakati mmoja sikuchaguliwa Bungeni. Nilikuja mara mbili halafu nikabaki nje. Niliona kwamba kubaki nyumbani ni shida. Wakati watu wanaongea, wengine hawaelewi na hawajaonja shida ya kuwa nje na wananchi hawajali. Wanafikiri kuwa wewe bado uko sawa. Mwingine anasema wewe ni wetu.
view
-
12 Nov 2019 in National Assembly:
Nafupisha kusema kuwa niko katika Kamati ya Huduma ya Wabunge. Nimeenda India, na ufikapo huko, yule Mjumbe wa zamani, anapewa tikiti mara nne kwa mwaka ya kusafiri mahali ambapo anataka akitumia ndege. Anapewa karibu mara kumi na tano kwa kusafiri kwa reli. Pia, anapewa matibabu kwa jamii yake. Sijui ni nini inayofanya tusiwaangalie wenzetu jambo hili linafanyika kwengine. Nimeenda karibu nchi tatu na wanajali wenzao waliotumikia watu mbeleni.
view