10 Nov 2022 in National Assembly:
Kwa hivyo, sina shaka kwamba Seneta aliyetajwa ako na uwezo wa kutuwakilisha katika Tume. Lakini ukweli ni kwamba ODM wametulaghai. Mhe. Spika si mgeni kwa ulaghai wa ODM. Shukran, Mhe. Spika.
view
26 Oct 2022 in National Assembly:
Shukrani, Mheshimiwa Spika wa Muda. Ningependa kukupongeza kwa uteuzi wako kama msaidizi wa Spika. Ningependa kuchukua fursa hii kuwashukuru wapiga kura wa Laikipia Kaskazini kwa kunipa nafasi nyingine kuhudumu katika Bunge la Awamu ya Kumi na Tatu. Mheshimiwa Spika wa Muda, Wabunge wote walioketi hapa siku ya leo walipigwa msasa na darubini na wapiga kura waliowachagua. Wote watakubaliana nami kwamba huko The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
26 Oct 2022 in National Assembly:
kupigwa msasa na darubini waliopitia kwa wananchi haikuwa kazi rahisi. Kazi ya Bunge hili ni kuwapiga msasa wale waliopendekezwa na Rais kuwa mawaziri kwa sababu ya ustawi na maendeleo ya jamii ya Kenya. Mheshimiwa Spika wa Muda, kazi inayomsubiri Rais wetu mpendwa wa nchi hii ni kubwa inayohitaji uadilifu na uaminifu, na bila shaka haiwezi kufanywa na watu ambao maadili yao yana tashwishi. Kutoka kwa jamii ya wafugaji, ningependa kumpongeza na kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa maana ninapotazama watatu ambao wameteuliwa katika jamii ya wafugaji, akiwepo aliyekuwa Kinara wa walio wengi Bungeni, Mheshimiwa Aden Bare Duale, bila shaka maadili yao sio ...
view
26 Oct 2022 in National Assembly:
Mheshimiwa Spika wa Muda, nilikuwa natazama Katiba ya Kenya asubuhi hii, na Sura ya Nne inazungumzia haki ya Mkenya. Baadhi ya haki iliyozungumziwa ni haki ya Mkenya na mali yake kuwa salama. Lakini sasa hivi, wananchi wa Kitui wanahangaishwa na Wakenya wenzao. Ukitazama Laikipia Kaskazini, tunahangaishwa na majambazi wanaotoka kaunti jirani. Wengi wetu tumepokonywa haki yetu tuliyopewa na Katiba ya Kenya; haki ya mali na nafasi yetu kulindwa. Haki nyingine ambayo Wakenya wengi wamepokonywa ni elimu ya msingi, ambayo ni haki ya kila mtoto Mkenya. Mheshimiwa Spika wa Muda, leo hii ukitembea Kaunti ya Baringo, haswa eneo Bunge la Tiaty, ...
view
26 Oct 2022 in National Assembly:
nafasi ili azishughulikie kesi zake 35 halafu nafasi hii ipatiwe Wakenya wengine wasio na doa, kasoro wala tashwishi ili waweze kuwatumikia Wakenya . Nikirejelea swala la Bi. Peninah Malonza, huyu mwanamke maskini analaumiwa kuwa hakuweza kuzungumza. Sio mara ya kwanza kwa wanawake kulaumiwa. Katika shamba la Edeni, Adamu ambaye alitangulia kula tunda walilokuwa wamekatazwa kula katika hilo shamba, alimlaumu Hawa kwa kosa lake, ilhali yeye ndiye aliyetangulia pale. Ni yeye angekataza lile tunda kuliwa. Wanataka kumfanya binti Malonza kama kafara bure. Iwapo ni kupita, basi sharti huyu binti pia apitishwe. Shukrani, Mheshimiwa Spika.
view
4 Oct 2022 in National Assembly:
Thank you, Hon. Speaker. Indeed, I want to confirm to this House that Jubilee Party is a Member of the Azimio la Umoja One-Kenya Coalition Party.
view
4 Oct 2022 in National Assembly:
I want to tell my colleagues in Kenya Kwanza Coalition that I am an independent woman and I did not come to Parliament through some party waves; I created my own wave. I am a member of Jubilee and Azimio la Umoja One-Kenya Coalition. Many people have talked about coercion and duress and they leave me wondering what sort of cowards we have in this House. Does coercion mean some Members have been held at gunpoint, knifepoint or could they not scream for help or what exactly was the problem? Hon. Speaker, many people have been talking and referring to ...
view
4 Oct 2022 in National Assembly:
Hon. Speaker, I may not want to respond to Hon. Ichung’wa but I want to inform him that I am properly schooled, I am literate therefore I can read the Constitution. I was only explaining that we cannot purport to defend the same Constitution which we want to defile. As I wind up, I was saying that some Kenyans fought for the democracy we enjoy today while others died for it. As somebody mentioned, indeed there is slave trade in this country and that is why young people are desperately going to Saudi Arabia. They are going there because they ...
view
9 Jun 2022 in National Assembly:
Mhe. Spika, ninashukuru kwa kunipatia nafasi hii. Kwanza kabisa, napenda kumshukuru Maulana kwa neema na fadhili na kwa kutuhifadhi tangu tulipoanza Muhula huu wa 12 katika Bunge hili. Mhe. Spika, kwa njia ya kipekee nakushukuru wewe kwa kazi nzuri uliyofanya katika Bunge hili. Zaidi ya yote, ningependa kukuarifu kwamba Muhula wa 13 Mwenyezi Mungu akitujalia nitahesabika kama mmoja atakayerudi katika Jumba hili. Mhe. Spika, uko na kazi nzuri na kubwa ambayo umechangia kurudi kwangu hapa. Nawashukuru zaidi wananchi wa Laikipia Kaskazini ambao kwa mara ya kwanza tangu Kenya kupata uhuru walimchagua mwanamke kama Mbunge kutoka eneo bunge hilo ijapokuwa natoka ...
view
9 Jun 2022 in National Assembly:
inasikitisha kwamba ndugu aliyeongea, Mhe. Ichung’wah Kimani, ambaye anatoka Kikuyu, walianza kujenga shule huko kabla ya mkoloni kuondoka. Yeye anapewa fedha sawa na mimi ambaye ninaanza kujenga shule. Kwa hivyo, ni matumaini yangu makubwa kwamba jambo hilo litashughulikiwa ili tuweze kuona usawa katika ugavi wa rasilimali katika nchi hii. Nikilamalizia, nataka kusema kwamba wale ambao tuko katika mrengo wa Azimio tunajua Baba the 5th atakuwa Rais. Mhe. Spika, ni aibu kueneza uongo na fitina kwamba Mhe. Raila Amolo Odinga amekashifu sekta ya mitumba. Alisema atafufua ukulima wa pamba.
view