23 Feb 2023 in National Assembly:
Kinara wa Waliyo Wachache Bungeni alipozungumza alisema kwa kimombo kwamba wanataka kuchukua hatua za kinidhamu. Utasikiza alivyosema. Mhe. Junet aliposema kuwa wale wanataka kuenda kuchukua nafasi zao katika Kenya Kwanza waende, ninamjulisha kuwa hatuendi. Iwapo wana njia yakutupeleka watafute tingatinga watupeleke. Tutakaa kwenye huu mrengo. Ndugu yetu ambaye ni Kinara wa Wachache hana ule uvumilivu wa kusikiza mawaidha yanayotofautiana na yake. Kwa Kiingereza inaitwa intolerance. Kila mmoja aliye kwenye jumba hili alichaguliwa na alitumia mali zake, akili na hata muda wake kutafuta kura, kujitafutia na kutafutia mrengo wake wa kisiasa. Tusifike hapa watu waanze kuhujumu wenzao kwa sababu wengine wetu ...
view
23 Feb 2023 in National Assembly:
mbaya zaidi kuliko ile imla tuliyoshuhudia katika hii nchi miaka iliyopita. Hatuwezi kuomba mtu ruhusa ya kuenda ikulu.
view
23 Feb 2023 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda naomba nikushukuru. Wahenga wanasema mficha uchi hazai.
view
23 Feb 2023 in National Assembly:
Mheshimiwa Spika ninavyoelewa mimi ni kwamba, kila Mheshimiwa katika Jumba hili ana wajibu wa kuhakikisha kuwa serikali imewajibika. Awe wa upande ule ama upande huu. Ninashangaa kizaazaa ambacho ndugu yetu Kinara wa Waliowachache anataka kuleta kisiri ni cha nini. Iwapo kizaazaa kipo, wasifanye kisiri bali walete kinaga ubaga kwa kuwa chama ninachosimamia… Wajua waswahili husema paka akiondoka panya hutawala. Mhe. Uhuru alipoondoka Jubilee kwa sasa mimi ndiyo Kinara wa chama wa muda. Iwapo wana ODM wanataka mazungumzo basi wazungumze nami. Naomba Kiongozi wa Waliowengi Bungeni alinde uhuru na haki za Wabunge. Ashirikiane na ndugu zetu kwenye Bunge. Waache kwenda Jeevanjee. ...
view
23 Feb 2023 in National Assembly:
Kinara wa Waliowachache Bungeni alipozungumza alisema kwa kimombo kwamba wanataka kuchukua hatua za kinidhamu. Utasikiza alivyosema. Mhe. Junet aliposema kuwa wale wanataka kuenda kuchukua nafasi zao katika Kenya Kwanza waende, ninamjulisha kuwa hatuendi. Iwapo wana njia yakutupeleka watafute tingatinga watupeleke. Tutakaa kwenye huu mrengo. Ndugu yetu ambaye ni Kinara wa Wachache hana ule uvumilivu wa kusikiza mawaidha yanayotofautiana na yake. Kwa Kiingereza inaitwa intolerance. Kila mmoja aliye kwenye Jumba hili alichaguliwa na alitumia mali yake, akili na hata muda wake kutafuta kura, kujitafutia na kutafutia mrengo wake wa kisiasa. Tusifike hapa watu waanze kuhujumu wenzao kwa sababu wengine wetu wameenda ...
view
23 Feb 2023 in National Assembly:
The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
23 Feb 2023 in National Assembly:
Mheshimiwa Spika ninavyoelewa mimi ni kwamba, kila Mheshimiwa katika Jumba hili ana wajibu wa kuhakikisha kuwa Serikali imewajibika. Awe wa upande ule ama upande huu. Ninashangaa kizaazaa ambacho ndugu yetu Kinara wa Waliowachache anataka kuleta kisiri ni cha nini. Iwapo kizaazaa kipo, wasifanye kisiri bali walete kinaga ubaga kwa kuwa chama ninachosimamia… Wajua Waswahili husema paka akiondoka panya hutawala. Mhe. Uhuru alipoondoka Jubilee kwa sasa mimi ndiyo Kinara wa chama wa muda. Iwapo wanachama wa ODM wanataka mazungumzo basi wazungumze nami. Naomba Kiongozi wa Waliowengi Bungeni alinde uhuru na haki za Wabunge. Ashirikiane na ndugu zetu kwenye Bunge. Waache kwenda ...
view
10 Nov 2022 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Spika. Inafahamika kwamba awali, kuna Hoja ilipitishwa na Jumba hili kuhusiana na uteuzi wa Makamishna wa Tume ambayo tunazungumzia juu yake. Kubatilishwa kwa Hoja hiyo katika Bunge la Seneti si jambo geni na hatutaki kuambiwa kwamba ni Seneti inabadilisha. Hii ni mazoea na tabia ya ndugu zetu katika mrengo wa Azimio ambao ni ODM kufanya siasa za udanganyifu.
view
10 Nov 2022 in National Assembly:
Wao wanacheza siasa za ulaghai na unafiki. Ndugu zetu kutoka ODM ni wanafiki wabaya sana. Nataka kusema nikisimama kwenye Jumba hili kwamba tulipojiunga nao, hatukushurutishwa ama kulazimishwa. Tukitaka talaka, hatutashurutishwa. Tutawataliki jinsi tunavyotaka.
view
10 Nov 2022 in National Assembly:
Mimi nasema hivi kwa sababu nilipokuwa nagombea kiti changu katika Eneo Bunge la Laikipia Kaskazini, Mhe. Junet na kiongozi wa chama chake walikuja kumpigia debe aliyekuwa mshindani wangu katika chama cha ODM. Na kama hiyo haijatosha, wametufuata na dhuluma katika Jumba hili. Sisi tukiomba nafasi yetu katika Tume siyo tafadhali. Ni haki yetu. Sisi tukiomba kuwakilisha watu wetu katika kamati za bunge hii siyo tafadhali kwa maana tulipigania. Ndugu zangu wa muungano wa Kenya Kwanza msubiri maanake hamkuwa makasisi katika ndoa yetu na hamtakuwa makasisi katika talaka yetu.
view