Sara Paulata Korere

Parties & Coalitions

Telephone

0727027937

All parliamentary appearances

Entries 351 to 360 of 416.

  • 25 Feb 2015 in National Assembly: Ninashukuru mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa pia kumshukuru Mbunge aliyeweka Hoja hii mbele yetu na kwa busara kubwa ambayo ametumia. Itafahamika kwamba dhuluma waliofanya hao wabeberu kwa nchi hii ni nyingi sana. Tukisema Mau Mau, itafahamika kwamba kila kabila la Kenya lilikuwa na view
  • 25 Feb 2015 in National Assembly: yao na inategemea kila kabila liliita Mau Mau yake nini. Waliyoyafanya hao wabeberu katika nchi hii na kuwadhulumu watu wa Kenya yalikuwa mabaya na mengi sana. Kwa mfano, waliwafunga mashujaa wetu, mmoja wao akiwa ni hayati mwanzilishi wa taifa hili Mzee Jomo Kenyatta. Itafahamika kwamba tukiongea juu ya mashujaa na dhuluma ambazo walifanya wabeberu, na tunataka fidia ilipwe ili kufidia wale ambao walipata madhara kutokana na wabeberu na mambo waliyofanya. Itakumbukwa kwamba wanawake wa nchi hii walifanya mambo mengi kupigania uhuru wa Kenya. Lakini mara nyingi, wanawake wamesahauliwa katika kufidia mashujaa. Itafahamika kwamba wanawake wengi waliwachwa na mzigo wa kulea ... view
  • 25 Feb 2015 in National Assembly: Kwa hivyo ni muhimu tutilie mkazo iwapo tunataka haki itendeke. Inatubidi tufahamu yale ambayo yaliaachwa na hawa wabeberu. Zile taabu ambazo tulirithi na tungali tunaishi nazo ziangaliwe. Mashujaa wote wafidiwe bila kujali wametoka sehemu gani. view
  • 25 Feb 2015 in National Assembly: Bi. Naibu Spika wa Muda, baadhi ya wale ambao walikuwa askari wa kikoloni, yaani British Army, walifanya mazoezi katika sehemu tofauti tofauti za nchi hii. Baada ya kutoka katika sehemu hizo,waliacha mabomu ambayo mpaka leo yanaendelea kuwaua wenyeji na kuathiri mifugo. Walifanya mambo mengi ambayo ni ya kuvunja moyo sana. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 25 Feb 2015 in National Assembly: Kwa hivyo, ningependa kusema kwamba Hoja aliyowasilisha mhe Wangamati ni muhimu sana. Naomba wabunge wenzangu tuunge mkono Hoja hii. view
  • 25 Feb 2015 in National Assembly: Aidha, tutilie maanani suala la kuibua njia ambazo zitawafaidi mashujaa, hasa wale ambao wangali hai. Tunajua kwamba wengi bado hawajafa. Ni muhimu tuangalie masuala ya ardhi ili kwamba ardhi iliyonyakuliwa irudishiwe wale wanaostahiki kumiliki ardhi hiyo. view
  • 25 Feb 2015 in National Assembly: Bi. Naibu Spika wa Muda, naomba kuunga mkono Hoja hii. view
  • 25 Nov 2014 in National Assembly: Thank you, hon. Temporary Deputy Speaker. I want to take this opportunity to condole with the families and friends of the departed souls. Indeed, as Kenyans we are all mourning. The security situation in this country is really wanting. I agree with the Members that it is not about what ole Lenku has not done or what he will not do but it is about what ole Lenku will never learn to do. The NIS is a dead branch. It is not their business to be telling us who is moving out with whose wife or daughter in the village. ... view
  • 25 Nov 2014 in National Assembly: When a black woman gets a white baby, we blame the devil just the same way we are blaming Mr. ole Lenku for everything. But to Mr. ole Lenku, sometimes you must make decisions. If somebody or anybody is sabotaging Mr. ole Lenku, in good spirit Mr. ole Lenku should resign and go home. view
  • 15 Oct 2014 in National Assembly: Nakushukuru Mhe. Spika. Mjadala uliopo mbele yetu, kwa maoni yangu, ungekuwa imefanyika mwaka jana. Hata hivyo, ni shukrani maanake leo tumepata kuujadili. Hoja hii ni muhimu sana. Sekta ya boda boda ni sekta ambayo imechangia pakubwa kuinua uchumi wa nchi yetu. Imechangia pakubwa pia kuimarisha uchumi wa jamii, na pia imetoa ajira kwa vijana ambao wamekuwa wakitangatanga mitaani bila ajira, na imeinua pia mapato ya jamii. Cha kusikitisha ni kwamba vijana hawa, wakiwa ni wasichana na wavulana ambao wanaendesha boda boda, ni watu ambao hata kupata leseni imekuwa ni shida. Kwa kusema kweli, maeneo mengi ambayo sisi wengine tumetoka, ni ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus