13 Nov 2024 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Spika. Ni vile sisi ni wawakilishi wa wananchi na wakituona tuko hapa leo lakini hatujauliza maswali yanayowahusu, tukirudi katika maeneo bunge yetu, tutakuwa na shida. Mwanzo, ningependa kumpongeza Waziri kwa vile yeye ni mungwana sana. Tunapoenda ofisini mwake, huwa tunapokelewa vizuri. Ninataka Waziri ajue kuwa Lamu Mashariki ndio eneo bunge pekee Kenya ambalo halina hata inchi moja ya barabara ya lami. Eneo Bunge la Lamu Mashariki lina barabara tatu. Mojawapo ni barabara ya Mtangawanda- Kizingitini ambayo mnaijua. Ninaomba mtueleze mikakati ya ujenzi wa barabara hiyo imefikia wapi angalau tuwe na barabara ya lami. Barabara ya pili ni ya ...
view
13 Nov 2024 in National Assembly:
Mhe. Spika, Lamu Mashariki ina mazingira tofauti. Maeneo yetu sio yale wanabara mnaita landmass . Kwetu ni watermass . Tunahitaji seawalls, yaani zile kuta za bahari. Kuna kijiji kinachoitwa Bwajumwali ambacho karibu kibebwe na maji. Watoto pia wanabebwa na maji. Kijiji hicho kilijengwa kikiwa kidogo.
view
13 Nov 2024 in National Assembly:
hakumaliza ujenzi na akakimbia. Mambo hayo pia yako katika Ministry yako. Kwa hivyo, tafadhali yaangalie. Ahsante, Mhe. Spika.
view
17 Oct 2024 in National Assembly:
Asante, Mhe. Spika. Tuajua kwamba
view
17 Oct 2024 in National Assembly:
zina madhara na sheria ya kuzipinga ilipitishwa hapa. Sijui kama watu wanaona kuwa kule kwangu ni karibu na Somalia kwa hivyo wameamua kutuwachia asbestos. Kuna nyumba za hospitali kule Kizingitini na wanaoishi pale ni madaktari. Nyumba zote hizo ziko na asbestos kwenye paa. Kingine cha kusikitisha ni kwamba contractor aliyepewa kandarasi ya kuotoa asbestos kwenye paa za nyumba katika hospitali ya Kiunga alizitoa. Nina uhakika kwamba BQ ya kandarasi hiyo inaonyesha mahali anapofaa kuhifadhi hiyo asbestos. Jambo la kushangaza ni kwamba mwanakandasi huyo aliwapatia wananchi wa Kiunga asbestos hiyo na hivi ziko kwenye private houses badala ya kuzizika pahali au ...
view
17 Oct 2024 in National Assembly:
aliziwacha hizi asbestos pale Kiunga. Wananchi wamezichukua na kutengeneze maboma. Ni hatari sana. Ninaomba wahusika wahakikishe kwamba hilo jambo limerekebishwa kabla halijaleta madhara. Tumeambiwa kwamba asbestos husababisha cancer . Unatarajia watu wangu wa Kiunga wapate hiyo shida ilihali wenyewe ni maskini wa roho zao?
view
9 Oct 2024 in National Assembly:
Ahsante Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi nichangie Mswada huu kuhusu Maktaba ya Kitaifa. Mwanzo, ninaipongeza Kamati kupitia kwa Mwenyekiti wake, Mhe. Wanyama. Wamefanya jambo la maana kwa sababu sheria hii ilikuwepo kabla ya ugatuzi. Hivyo, kulikuwa na haja kubwa ya kuweka hii sheria baada ya mwaka wa 2010 kuhusu mambo ya ugatuzi. Kwa hivyo, ilikuwa muhimu sana afanye hivyo. Sheria inasema kuwa, kuna haja ya kuwa na maktaba angalau katika makao makuu ya kaunti, lakini kuna kaunti zingine kama Lamu ambazo hazina maktaba hata moja. Hii sheria ikitungwa, ningependa Kamati izingatie kuwa kaunti zingine ambazo hazina maktaba hata ...
view
9 Oct 2024 in National Assembly:
Kwa mfano, pale Lamu Town kuna sheria kwamba huwezi kujenga nyumba iliyo zaidi ya gorofa tatu karibu na bahari. Lakini utaona mtu akikandamizwa na sheria hii. Lazima tutumie utamaduni huu kwa sababu ya makavazi na historical sites . Naomba hii Kamati hata kama Mwenyekiti hayuko hapa, wazingatie sehemu ile ndiyo wapate fidia fulani ili wazidi kuhifadhi na kuweka kumbukumbu vizuri. Maanake maktaba na
view
9 Oct 2024 in National Assembly:
hizo ni kumbukumbu. Zimewekwa na kaunti na hazishughulikiwi. Ukiangalia LamuFort, hakuna maktaba ya kumbukumbu ya kisawasawa ambayo mtu anaweza akasoma. Ile maktaba yao ina kumbukumbu ndogo ya kueleza kitu fulani kimetoka wapi. Kwa hivyo, naona ni mwanzo mzuri na tunaunga mkono hii Kamati. Lakina, ina kazi nyingi ya kufanya na kwa hivyo, wahusishe mambo yote ambayo tunasema. Ahsante sana.
view
8 Oct 2024 in National Assembly:
Asante, Mhe. Spika. Umoja wa taifa ni muhimu sana. Naibu wa Rais haleti umoja. Nataka ieleweke kwamba watu wa mlima wanaishi sehemu zingine. Kule kwangu, Kiunga, niko na watu wa mlima. Kile wanachoona zaidi ni sanddunes . Hawaoni mlima. Wanaona bahari. Naibu wa Rais alizungumzia kuhusu National Intelligence Service (NIS) ambayo ilikuwa grave mistake . Alikosea sana. Afadhali angetaja Noordin kama ako na shida naye kuliko taasisi ya Huduma ya Ujasusi ya Kitaifa. Inatufanya tukae dhaifu mbele ya maadui zetu. Kwa mfano, Al-Shabaab watatuona vipi kama tuko wadhaifu? Kwa mtu yeyote, haswa mwanaume anayetukana mwanamke, kila mtu aliyeumbwa ana shimo ...
view