22 May 2013 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Naibu Spika. Ningependa kuchukua fursa hii kukushukuru kwa kunipatia nafasi hii niweze kuichangia Hoja hii. Vile vile, ningependa kumshukuru mhe. John Mbadi kwa kuileta Bungeni Hoja hii muhimu sana inayotuhusu sana sisi watu wa Pwani.
view
22 May 2013 in National Assembly:
Masikitiko makubwa ni kwamba sekta ya uvuvi katika eneo la Pwani imedharauliwa sana na Serikali kwa sababu tunazoshindwa kuzielewa. Hivi sasa, ukienda kuulizia katika afisi za uvuvi, utapata kwamba licha ya kwamba Pwani ni eneo kubwa sana la uvuvi kwa sababu ya Bahari Hindi, kiasi cha samaki wanaopatikana ni kidogo sana ukilinganisha na kiasi cha samaki wanaopatikana katika Ziwa Victoria na kwingineko. Kusema kweli, hili ni jambo la kushangaza sana. Tukiangazia zaidi, watu wanaofanya kazi hii katika maeneo ya Lamu na kwengineko, na haswa tukiangazia suala la vifaa vya kuhifadhia samaki, kama lilivyozungumziwa; huwezi kuvipata vifaa hivyo katika sehemu hiyo. ...
view
22 May 2013 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika, maskitiko makubwa ni kwamba tatizo kubwa linaloikabili jamii ya wavuvi katika maeneo ya Lamu na sehemu nyingine za Pwani ni kwamba, jamii hiyo haijawahi kusaidiwa ili iweze kujiendeleza. Utapata watu kutoka nchi zingine kama vile Indonesia na China wanakuja kuvua samaki katika maeneo ya nchi yetu kwa sababu wako na vifaa vya kisasa, yakiwemo maboti mazuri yanayowawezesha kufanya kazi hiyo kwa njia bora zaidi. Wanakuja kuvua samaki katika sehemu ya nchi yetu na kuwapeleka samaki hao kwao kwa faida ya nchi zao na faida zao binafsi. Chombo kinachotumiwa na watu wetu kwa shughuli ya uvuvi hakiwezi kumudu ...
view
22 May 2013 in National Assembly:
Ni maskitiko makubwa kwamba ndugu zetu wavuvi wana ujuzi kamili wa kuwawezesha kuifanya kazi hiyo lakini hawajapata usaidizi kikamilifu kutoka kwa Serikali yetu kama walivyosaidiwa Wakenya kwenye sekta ya kilimo na sekta nyinginezo. Hivi sasa, samaki wanatoka sehemu ya Lamu na kupelekwa kuuzwa Mombasa. Kuna sehemu inayoitwa Majengo. Huko ndiko wanakouzwa samaki hao â
view
15 May 2013 in National Assembly:
Ahsante Mhe. Spika wa Muda. Kwanza, ninataka kumshukuru ndugu yangu, Mheshimiwa aliyeleta Hoja hii hapa. Tunafahamu vyema kwamba wazee wetu ni watu ambao wanahitaji kuzingatiwa sana. Hii ni kwa sababu hatungefika hapa leo au hatungefikisha umri huu bila wazee wetu. Hata sisi tutakuwa wazee.

Hoja hii inafuatana na Katiba yetu ambayo tuliipitisha kwa kusema kwamba tutawasimamia na kuwasaidia wazee. Jambo hili liko katika Kipengee cha 57 cha Katiba ya Kenya. Kipengee hiki kinasema: âThe State shall take measures to ensure the rights of older persons.â Kipengee cha 57(d) kinasema: âto receive reasonable care and assistance from their family and the State.â

Mheshimiwa ameelezea usaidizi ambao wazee wetu wanaweza kupata. Moja ni kuwa wazee wa umri wa miaka 60 na zaidi wahudumiwe katika hospitali zetu bila malipo yoyote. Hii ni kwa sababu mzee ataenda hospitalini, aambiwe alipe shilingi mia mbili na hajui atoe hizo pesa wapi. Ningeomba tulizingatie suala hili sana.