6 Nov 2013 in National Assembly:
Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kupata maelezo kamili kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama wa Kitaifa kuhusu masuala haya ambayo ametuelezea. Ni masikitiko makubwa kuona kwamba hali hii imekuwa ikiendelea kwa wale ambao wako na imani kubwa na dini ya Kiislamu. Tunaelewa vyema kwamba Serikali yetu au katika nchi ya Kenya tuko na Katiba ambayo tunataka tuifuate kama wananchi.
view
6 Nov 2013 in National Assembly:
Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Tunaelewa vyema kwamba tuko na Katiba katika nchi hii ambayo sisi kama wananchi tunafaa kuifuata. Vile vile, Serikali inafaa kuifuata hii Katiba. Masikitiko makubwa ni kwamba hali hii inatushangaza sana sisi Waislamu; kwamba yeyote anayeonekana kuwa na imani thabiti kuhusu dini yake, ndiye ambaye anafuatwa katika masuala haya ya mauaji. Mauaji yanapotokea, ni swala ambalo wengi wanajiuliza ni kwa nini jambo hili linafanyika. Hii ni kwa sababu tunaelewa vyema kwamba kuna sheria katika nchi hii. Serikali imejitenga na kusema kwamba haijui watu wote ambao walitajwa na Mhe. Nassir katika mauji hayo, ilhali karibu ...
view
6 Nov 2013 in National Assembly:
Ningependa kupata maelezo kamili kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama wa Kitaifa kwa sababu sidhani mimi na Waislamu katika nchi hii wataweza kutoshelezwa na maelezo ambayo tumepewa katika masuala haya. Tunahitaji kupata maelezo kamili yenye kutupa mwongozo katika suala hili.
view
12 Jun 2013 in National Assembly:
Shukrani, Bw. Naibu Spika wa Muda. Masikitiko makubwa ni kwamba utapata sehemu nyingi za nchi yetu ya Kenya hazipati huduma za afya vile inavyopaswa. Nikizungumzia eneo Bunge langu la Lamu Mashariki, licha ya kwamba kupatikana madaktari ni vigumu, hata hospitali zenyewe, ama hata zahanati zenyewe, hazina madawa. Watu huenda na kurudi; hata ingawa hufika huko akiwa mgonjwa anaambiwa kwamba dawa hakuna. Kwa hiyo, mara kwa mara watu wamekuwa wakisumbuka au kuteseka. Hata huduma za X-ray hazipatikani. Leo Serikali imesema kwamba wanawake hawatatozoa ada ya kujifungua, lakini utapata hakuna sehemu ya akina mama ama akina dada zetu ya kujifungulia katika eneo ...
view
12 Jun 2013 in National Assembly:
Shukrani, Bw. Naibu Spika wa Muda. Masikitiko makubwa ni kwamba utapata sehemu nyingi za nchi yetu ya Kenya hazipati huduma za afya vile inavyopaswa. Nikizungumzia eneo Bunge langu la Lamu Mashariki, licha ya kwamba kupatikana madaktari ni vigumu, hata hospitali zenyewe, ama hata zahanati zenyewe, hazina madawa. Watu huenda na kurudi; hata ingawa hufika huko akiwa mgonjwa anaambiwa kwamba dawa hakuna. Kwa hiyo, mara kwa mara watu wamekuwa wakisumbuka au kuteseka. Hata huduma za X-ray hazipatikani. Leo Serikali imesema kwamba wanawake watajifungua bure, lakini utapata hakuna sehemu ya akina mama ama akina dada zetu ya kujifungulia katika eneo la Lamu ...
view
22 May 2013 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Naibu Spika. Ningependa kuchukua fursa hii kukushukuru kwa kunipatia nafasi hii niweze kuichangia Hoja hii. Vile vile, ningependa kumshukuru mhe. John Mbadi kwa kuileta Bungeni Hoja hii muhimu sana inayotuhusu sana sisi watu wa Pwani.
view
22 May 2013 in National Assembly:
Masikitiko makubwa ni kwamba sekta ya uvuvi katika eneo la Pwani imedharauliwa sana na Serikali kwa sababu tunazoshindwa kuzielewa. Hivi sasa, ukienda kuulizia katika afisi za uvuvi, utapata kwamba licha ya kwamba Pwani ni eneo kubwa sana la uvuvi kwa sababu ya Bahari Hindi, kiasi cha samaki wanaopatikana ni kidogo sana ukilinganisha na kiasi cha samaki wanaopatikana katika Ziwa Victoria na kwingineko. Kusema kweli, hili ni jambo la kushangaza sana. Tukiangazia zaidi, watu wanaofanya kazi hii katika maeneo ya Lamu na kwengineko, na haswa tukiangazia suala la vifaa vya kuhifadhia samaki, kama lilivyozungumziwa; huwezi kuvipata vifaa hivyo katika sehemu hiyo. ...
view
22 May 2013 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika, maskitiko makubwa ni kwamba tatizo kubwa linaloikabili jamii ya wavuvi katika maeneo ya Lamu na sehemu nyingine za Pwani ni kwamba, jamii hiyo haijawahi kusaidiwa ili iweze kujiendeleza. Utapata watu kutoka nchi zingine kama vile Indonesia na China wanakuja kuvua samaki katika maeneo ya nchi yetu kwa sababu wako na vifaa vya kisasa, yakiwemo maboti mazuri yanayowawezesha kufanya kazi hiyo kwa njia bora zaidi. Wanakuja kuvua samaki katika sehemu ya nchi yetu na kuwapeleka samaki hao kwao kwa faida ya nchi zao na faida zao binafsi. Chombo kinachotumiwa na watu wetu kwa shughuli ya uvuvi hakiwezi kumudu ...
view