9 Apr 2025 in National Assembly:
ilhali kuna shule zingine ambazo zimepata Ksh100 milioni. Jibu lako limeonyesha kuwa kuna udhaifu na sehemu zetu zinanyanyaswa, ilihali shule zetu ni maskini na haziwezi kufananishwa na shule za town . Weka mipangilio ya kuhakikisha kuwa shule zile zimepata The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
9 Apr 2025 in National Assembly:
pesa za kutosha. Katika jibu lako, umesema kuwa pesa hizo zimetumika kwa upande wa
view
9 Apr 2025 in National Assembly:
. Hiyo ni kweli kwa maana hawana walimu. Wanatumia pesa hizo kuwaandika walimu. Umeona taabu tulizonazo katika shule hizo. Natarajia kuwa ukija hapa wakati mwingine, useme kuwa umeligawia eneo la Kizingitini Ksh100 milioni kama vile shule ya Alliance na kwingineko.
view
8 Apr 2025 in National Assembly:
Asante bwana Spika. Kwa niaba yangu, familia yangu, na watu wangu wa Lamu Mashariki ninaowakilisha, natoa rambirambi zangu kwa familia ya Mhe. Teiyaa. Tulikuwa naye katika Bunga la Kumi na Mbili. Tulikuwa kwa kamati moja. Alikuwa mtu mzuri. Natoa pole kwa familia. Mungu aiwezeshe kujaza pengo aliloacha. Asante bwana Spika.
view
2 Apr 2025 in National Assembly:
Mhe. Spika. Mwanzo nakupongeza kwa kuwatambua wavuvi wa samaki. Ahsante. Wizara iko na mikakati gani ya kuwasaidia wavuvi kuboresha usalama wao? Wavuvi hawajazingatiwa inchini Kenya. Siku tatu zilizopita kule Lamu, boti ilipata shida mbele ya Mkokoni, na wavuvi wakapiga simu na kuomba wasaidiwe. Hawakusaidiwa, na ikabidi waogolee wenyewe wakafika. Chombo kilikuwa kimebeba mizigo mingi na mawimbi yakaja yakakizamisha. Ingekuwa rahisi wangefikiwa kwa haraka kwa maana si mbali na kambi nyingi za forces zilizoko katika eneo lile. Ni mikakati tuu haijapangwa. Tafadhali Waziri, hao wavuvi ni Wakenya, na wanachangia pakubwa uchumi wa nchi hii. The electronic version of the Official Hansard ...
view
2 Apr 2025 in National Assembly:
Hon. Spika, utanisaidia. Sijui niseme suala hili ni la kitengo cha usalama, ama kile cha utumishi au Blue Economy . Lakini hawa ni Wakenya, na inafaa watafutiwe njia wasaidike.
view
2 Apr 2025 in National Assembly:
ziwekwe. Ahsante.
view
2 Apr 2025 in National Assembly:
Mhe. Spika, Lamu inajulikana kwa kutegemea sana utalii. Tunauza samaki sana katika eneo Bunge langu la Lamu Mashariki. Kwa hivyo, watalii wakiathirika kidogo tu, sisi pia tunaathirika. Nataka Waziri aliambie Bunge hili ni kitu gani kilitokea Mangai, ambapo Chifu alitafutwa na Al-Shabaab. Kuna Gavana aliyesema kwa jambo la vitambulisho kuwa ni vibaya watu wa Lamu wasifanyiwe vetting kwa sababu Al-Shabaab wanaingia nchini. Kwa hivyo mimi na watu wangu tuna wasiwasi hao watu wasifanye kusudi to justify their point . Kwa hivyo, Waziri atuambie ni nani alihusika kumtafuta Chifu Mangai. Kama ni Al-Shabaab utuambie, maanake walikuja kwa njia tofauti kabisa. Eti ...
view
2 Apr 2025 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ya kuzungumzia Hoja hii ya kutengeneza mbolea hapa nchini kwetu. Ninataka kumpongeza Mhe. Atandi kwa kuleta Hoja hii. Hoja hii itawasaidia wakulima kuhakikikisha kuwa mbolea inapatikana kwa wingi na kwa urahisi. Mazao pia yatapatikana kwa wingi ikiwa mbolea itatengenezwa hapa Kenya. Vijana wetu watapata kazi kwa sababu kampuni hizo au viwanda hivyo vikiwa hapa, vitaajiri watu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
2 Apr 2025 in National Assembly:
Tuseme ukweli. Tusiwe wezi wa fadhila. Kitu kizuri kikifanywa, tuseme kimefanywa vizuri au kiboreshwe. Tusikatae kusema kuwa mtu amefanya jambo nzuri kwa sababu ya siasa. Rais wetu na Naibu wake wamejaribu. Ruzuku ama subsidy inayowekwa kwenye mbolea ili isiwe ghali haikuanza na Rais huyu wala Serikali hii. Ilianza na Serikali iliyopita. Hawa nao wamejaribu kuhakikisha kuwa mbolea inapatikana kwa bei nzuri lakini kuna haja ya kuzidisha bidii ili mbolea ipatikane kwa urahisi zaidi.
view