25 Sep 2024 in National Assembly:
Ahsante. Waziri, mwanzo, ningependa kukupongeza na kukushukuru wakati ulikuwa Waziri wa Barabara, Usafiri na Kazi za Umma. Ulijua Lamu Mashariki haina barabara na ukafanya mipango mizuri. Ahsante. Saa hii pia, ningependa ufikirie kuhusu Lamu Mashariki katika upande wa michezo. Hakika kwa miaka kadhaa au tangu uhuru upatikane, hakuna kitu kimefanywa katika Eneo Bunge la Lamu Mashariki katika upande wa michezo. Nimesikia mipango yote ambayo umezungumzia. Kaunti ya Lamu haina uwanja wa Serikali ya Kitaifa wala ya kaunti. Katika mipangilio yote, sisi tunaachwa nyuma. Nakuomba kwa hisani yako kama unaweza kutaja kitu kimoja ambacho kimefanywa Lamu Mashariki na hii Wizara. Niambie ...
view
24 Sep 2024 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii nami nipate kuzungumza kuhusu NG-CDF. Katika maeneo bunge mengi, pesa za NG-CDF ndizo pesa pekee tunazotarajia kufanyia maendeleo. Eneo Bunge la Lamu Mashariki na maeneo bunge mengine mengi yamebaguliwa kwenye mipango ya maendeleo. Kwa mfano, tukiangalia rekodi, tutaona kwamba kwenye Bajeti ya mwaka uliopita, Eneo Bunge la Lamu Mashariki lilipewa Ksh4 milioni, ilhali kuna eneo bunge lingine ambalo lilipewa Ksh450 milioni. Pesa za NG-CDF ndizo pesa pekee ambazo hazihusishwi na ubabe kwa sababu kila eneo bunge linapata mgao wake na linajipangia miradi yake kulingana na jinsi sheria inavyosema. Katika Serikali kuu, pesa ...
view
24 Sep 2024 in National Assembly:
tunaelekezwa wapi. Ninavyozungumza, Rais ametusaidia. Kule kwetu, viwango vya elimu viko chini sana, na madhara kwetu yameonekana. Vijana wameonekana wakienda wanavyokwenda ikabidi tuwasomeshe. Tukapewa nafasi ya kuajiri walimu lakini miongoni mwa walioajiriwa, ni waalimu wawili peke yake kutoka katika Lamu Mashariki. Hazina ya NG-CDF ilikuwa inatuokoa…
view
24 Sep 2024 in National Assembly:
Hivi sasa, katika chuo cha Waislamu cha Mafunzo ya Ualimu, na kile cha Mafunzo ya Ualimu cha Shanzu, tunasomesha zaidi ya wanafunzi 100 kupitia usaidiza wa hazina ya NG-CDF. Hao wanaosoma wataenda wapi? Leo hii niko na msukumo mkubwa. Mkwe wake Nordin, ambaye ni Mwenyekti wa Board, amewafukuza wanafunzi hao kutoka chuoni kama njia moja ya kuniadhibu mimi kwa sababu sijakubali Ishakani na Dar-es-Salaam Point ziende Ijara. Hivi sasa, wanafunzi wamefukuzwa kutoka chuoni kwa sababu hatujalipa hiyo pesa. Hazina ya NG-CDF ikiondolewa, tutaenda wapi?
view
17 Sep 2024 in National Assembly:
Asante, Mhe. Spika. Nami ninatoa rambirambi zangu, za familia yangu na watu wa Lamu kwa jumla, kwa Mheshimiwa aliyefariki. Ningependa pia kuchukua nafasi hii kutoa rambirambi zangu kwa familia ya Naibu wa Gavana wa Lamu aliyefariki. Mungu aiweke roho yake pahali pema. Alikuwa mtu mzuri mwenye ukakamavu na maskini amewacha familia ndogo. Mwenyezi Mungu aisaidie familia yake na ajaze pengo alilowacha. Kwa Gavana wetu wa Lamu na wakaazi wa Lamu, mwenyezi Mungu atupe subira na badali. Mungu amwezeshe Gavana kufanya uamuzi wa busara. Ninatoa pole kwa watu wa Mpeketoni, familia na watu wote wa Lamu kwa niaba ya familia yangu ...
view
14 Aug 2024 in National Assembly:
Ahsante Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi nami niwakaribishe Cambridge Link School Bungeni. Ningependa kurekebisha jambo Mhe. Spika ametaja kidogo. Kwa vile ninatoka sehemu za Lamu, imechukuliwa kuwa hii shule nayo inatoka pale. Ilhali, inatoka sehemu za Nyali, Mombasa. Ninawakaribisha sana. Niliwatafutia nafasi ili wakuje Bungeni. Waliona nimewaleta wanafunzi wa Lamu wengi, na wao pia wakataka kufika mahali hapa. Mtoto wa dadangu, Jamil, anasoma katika hii shule, na akawa anataka kufika mahali hapa. Na hivyo ndivyo waalimu walijiandaa kwa hii safari. Karibuni sana. Ninawahisi msome kwa bidii maana nyinyi ndio viongozi wa kesho. Katikati yenu, tuko na marais, magavana, wabunge na ...
view
14 Aug 2024 in National Assembly:
Karibuni sana na ninawatakia kila la heri. Hii ni shule nzuri iliyo na sifa kocho kocho. Waalimu ni wazuri na wanafunzi pia wako na nidhamu, na tunaifurahia.
view
14 Aug 2024 in National Assembly:
Ahsanteni, na kila la heri. Karibuni
view
13 Aug 2024 in National Assembly:
Bwana Spika, ninaomba tuwe makini sana hapa Bungeni. Si sawa tukisema tusifuate dini. Katiba yetu inatambua dini zote. Katika Uislamu, kujiweka kitanzi ni kati ya dhambi kubwa sana, na ninaamini kwamba hata kwenye Bibilia ni hivyo. Lakini pia Qurani inasema kwamba watu ambao hawaandikiwi madhambi ni watatu; yule ambaye hana akili mpaka wakati akili itakaporudi, mtoto mdogo na yule ambaye amelala mpaka The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
13 Aug 2024 in National Assembly:
atakapoamka. Kwa hivyo, kama kutakuwa na njia ya kuhakikisha kweli hana akili, hapo tutasema hana dhambi. Kuna watu ambao wanatumia hizi nafasi vibaya; kwa mfano, mtu akikosana na bwanake, pengine ameoa bibi mwingine, anakunywa na kuleta sarakasi. Huyo anafaa kuadhibiwa. Sisi wengine angalau tunakubali wanne. Kwa hivyo, mambo mengine yasiingizwe katikati na mtu akatumia nafasi hiyo. Ahsante, Bwana Spika.
view