27 Nov 2024 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Spika wa Muda. Nataka niafikiane na wenzangu katika Hoja hii. Nawaunga mkono wale waliochaguliwa. Kusema kweli, Mhe. Jaldesa atakuwa katika mstari wa mbele kwa sababu tunamjua. Alipokuwa WomanRepresentative, alifanya bidii sana katika kuzingatia mambo ya wanawake. Kwa hivyo, anajua kile kinachotakikana. Nataka kuwaomba wale waliochaguliwa wasikae tu kwa ma -boardroom . Watembee. Watuonyeshe kuwa watahakikisha wanawake wamechaguliwa zaidi kama
view
27 Nov 2024 in National Assembly:
, Members of Parliament na Members of County Assemblies (MCAs).
view
27 Nov 2024 in National Assembly:
The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
27 Nov 2024 in National Assembly:
Nimemsikia mmoja wa Wabunge wanaume wenzangu akisema kuwa wanaume pia wapewe kipaumbele, hususan boy-child . Sikatai lakini kwa sasa, kulingana na mambo ya
view
27 Nov 2024 in National Assembly:
, yule ambaye ni mnyonge kidogo ni mwanamke. Kuna maneno tuliyoyasikia kwenye mtandao, na nimemsikia Leader of the Majority
view
27 Nov 2024 in National Assembly:
akiwatetea wanawake. Imesemekana kuwa ni uongo na mtu huyo hakusema matusi hayo. Basi mtu huyo angejitokeza na kusema kuwa maneno hayo hayakuwa yake na ni propaganda tu . Lakini propaganda hiyo inayowalenga wanawake ikiendelea, mtatufanya tuzungumze ilhali hatutaki kuzungumza. Kila mtu ana maumbile yake. Ikiwa mwanamke anaweza kuyatumia, hata mwanaume anaweza kuyatumia. Nikisema kile ninachotaka kusema, mtasema ninaongea vibaya. Lakini ni kwa nini mwanamke haambiwi maneno hayo mpaka aamue kusimama kuwa kiongozi? Akiwa daktari, hamna shida.
view
27 Nov 2024 in National Assembly:
Sijataja jina la mtu hapa. Kama mtu anaona kofia inamtosha na akaivaa, hiyo ni stori yake. Sijataja jina la mtu.
view
27 Nov 2024 in National Assembly:
Ikiwa mwanamke ni daktari, pilot ama any other professional, hatusiwi vile ambavyo viongozi wanawake wanatusiwa. Lakini ukiwa kiongozi mwanamke, ni lazima utusiwe. Tunahisi uchungu. Sisi pia ni wazazi na wake wa watu. Sio haki ikiwa mtu kila anaposimama anatutusi tu. Itabidi tushirikiane tuunde sheria ili mtu akifanya hivyo, awekwe ndani.
view
27 Nov 2024 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Spika wa Muda.
view
25 Nov 2024 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi ya kuchangia mjadala kuhusu Hotuba ya Rais. Kusema kweli, Rais ni msikivu; yaani anasikiliza maneno. Hiyo ni sifa ya mwanadamu mzuri. Katika swala la Adani, kule
view