25 Nov 2024 in National Assembly:
The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
25 Nov 2024 in National Assembly:
kukataaa kwake kunatokana na kusikiliza. Hata hivyo, Mamlaka ya Kusimamia Viwanja vya Ndege Nchini (KAA) imepewa nafasi tena. Tunataka Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta uwe sawa na viwanja vingine vya ndege, kama vile Doha. Kuna Wakenya wengi kule. Ukiingia Doha, utafikiri uko katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta. Watu wengi wametoka makwao kwa sababu ya shida za kiulimwengu. Ikiwa Airport itaendelezwa vizuri, walio nchini wataandikwa kazi na hata wale watakaotaka kurudi nchini wanaweza kurudi na kufanya kazi nzuri. Kwa hivyo, nataka kuambia KAA kuwa, kwa kuwa President amesitisha Adani, ni lazima wajitahidi Airport iwe nzuri. Mambo madogo madogo ...
view
25 Nov 2024 in National Assembly:
Hili jambo likifaulu, itakuwa legacy ya Rais. Rais alizungumza juu ya mambo ya ICT hubs . Hilo ni jambo muhimu sana kule Kiunga kwa sababu ipo mbali sana na Huduma Centre. Kiunga haipati services za Serikali. Itasaidia sana.
view
25 Nov 2024 in National Assembly:
The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
25 Nov 2024 in National Assembly:
Rais alizungumza juu ya Gender-based violence (GBV). Naona Permanent Secretary na Inspector-General wamesimama kidete. Nawatahadharisha wanawake kuwa hii dunia imekuwa mbaya. Tunaona wakiwaamini watu na wanapoenda makwao, mambo yanaharibika baadaye. Hii Serikali ni ya broad-based Cabinet. Imewakilisha wengine …
view
20 Nov 2024 in National Assembly:
Asante Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi nami nichangie Mswada huu ulioletwa hapa na dada yetu Mhe. Irene, tunayempongeza sana. Irene, twajua kazi unaitenda. Mwenyezi Mungu ndiye mbunifu kushinda watu wote. Naye hakutupa mti ule kwa kuwa alijua hauna umuhimu kwetu. Wakati mwingine tunaleta ufundi lakini Mwenyezi Mungu amepanga mambo kwa mipango yake. Amepanga bila kubagua au mapendeleo. Kwa mfano, tuna Mikoko, Mikoma na mazao mengine Mwenyezi Mungu mwenyewe alitupangia katika Kaunti ya Lamu. Alijua kuwa aina hii ya miti inakua vizuri sehemu hii, wala siyo jukumu langu mimi mkaazi wa Lamu nipange mambo yetu ya kibinadamu. Huenda nikataka ...
view
20 Nov 2024 in National Assembly:
Ni Mkalatusi.
view
20 Nov 2024 in National Assembly:
Iwapo mti huu una shida, basi ni kwa vile umeletwa na binadamu. Nimejulishwa kwamba mti huu haukuwepo Kenya. Ulikuwa ni wa kwingine. Maji ni mhimu. Kukiwa na mti unaokunywa maji zaidi, basi unafaa kuondolewa. Sisi binadamu tuna vita na wanyama kwa sababu ya maji. Hayo maji ni muhimu kwa mazingira, kwetu sisi binadamu, na wanyama kwa jumla. Kuna haja ya kuharakisha hili suala. Sasa hivi kuna Waziri mtendakazi kwenye Wizara husika, Insh’Allah. Kulikuweko Waziri mwingine mtendakazi kule. Insh’Allah, wote walifanya kazi nzuri. Najua tutasaidika. Tuko pamoja naye kurekebisha. Iwapo huu mti waafaa kutolewa, bila shaka utolewe na usipandwe kabisa. Tupande ...
view
20 Nov 2024 in National Assembly:
Mhe. Spika, niko na tatizo lingine linalotokana na swala hili. Waziri, Lamu Mashariki ina wakulima wa simsim na hawatumii madawa yeyote. Lakini kuna shida kwa sababu majirani wetu wanatumia madawa ya kuua wadudu. Kwa hivyo, simsim zao zilizopelekwa kwenye soko za nje, zilirudishwa. Kutokana na hayo, zimeharibia sifa wakulima wote wa simsim. Ninavyoongea, simsim zimejaa kwenye soko za Lamu Mashiriki. Uko na mipango gani ya kuwasaidia wakulima hao ili mazao yao ya simsim yaweze kuuzwa? Wakulima wa Lamu Mashariki wako tayari mazao yao ya simsim yapimwe maana wao hawatumii madawa za kuua wadudu. Kama vile maziwa inapokuwa nyingi kupita kiwango ...
view
20 Nov 2024 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika, swali nililouliza halikujibiwa. Limepotea na ameambiwa aende kisha atarudi. Swali langu ni kuhusu simsim . Ningependa nilirejelee. Watu wangu walikuja kuniambia kwamba wako na shida. Kuna wakulima wa simsim Lamu Mashariki na wameniambia kwamba majirani wao wanatumia madawa na bidhaa zao zilirejeshwa. Hilo limefanya wao kupoteza soko. Simsim iko nyingi kule na haina soko. Je, mko na mipangilio ipi kusaidia hao wakulima wa Lamu Mashariki? Wao pia ni Wakenya. Ministry of Agriculture and Livestock Development inafanya kazi sehemu zingine, lakini Lamu Mashariki ni kama hakuna wakulima ilhali tuko nao. Tunazalisha c ashew nuts nyingi zaidi Kenya. Watu ...
view