Shariff Athman Ali

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 51 to 60 of 512.

  • 20 Nov 2024 in National Assembly: On a point of order, Hon. Deputy Speaker. view
  • 20 Nov 2024 in National Assembly: Naibu Spika, niko kwa hoja ya nidhamu. Je, ni haki Waziri kusema ataenda kuuliza county government na tuna hakika wafugaji wa simsim kwetu Lamu Mashariki hawajawahi kusaidiwa na chochote na serikali hiyo? Wanajitegema wenyewe ilhali sehemu zingine wakulima wa maziwa, majani chai, kahawa, na muguka, wote wanapata fedha kutoka kwa Serikali ya kitaifa. Nilikuwa natarajia aniambie mikakati iliyopo na kama hana saa hii, aniambie atarudi Jumatano anielezee ana mikakati gani. Si vema kuniambia niende kwa serikali gatuzi niulize Gavana. Mimi si Seneta wala mwakilishi wa wadi! view
  • 20 Nov 2024 in National Assembly: Mhesh. Naibu Spika, tukizungumza kuhusu makadamia, tunafaa kuizungumzia pamoja na nuts zingine, haswa korosho ambayo katika packaging, huchaganywa na macadamia. Nataka pia Waziri anapozungumza, azichanganye vivyo hivyo. Akizungumzia makadamia, azungumzie korosho. view
  • 20 Nov 2024 in National Assembly: Mhesh. Naibu Spika, tulienda na Kamati ya Dayaspora kule USA na tukakutana na wanadayaspora wakatuambia – nataka Waziri ajue – kuwa demand ya korosho haijafikiwa hata robo. Wanahitaji korosho sana kule. Lakini kwa sababu mmea huu unatoka Pwani, haufanyiwi bidii. Kwa kuwa naona Serikali hii inazingatia mimea mingine, naomba ishughulikie sana korosho. Hii itainua Kenya kwa ujumla. Wengine wanapotoa chai na kahawa, na sisi tutoe korosho na Kenya itainuka. view
  • 13 Nov 2024 in National Assembly: Ahsante, Mhe. Spika. Ni vile sisi ni wawakilishi wa wananchi na wakituona tuko hapa leo lakini hatujauliza maswali yanayowahusu, tukirudi katika maeneo bunge yetu, tutakuwa na shida. Mwanzo, ningependa kumpongeza Waziri kwa vile yeye ni mungwana sana. Tunapoenda ofisini mwake, huwa tunapokelewa vizuri. Ninataka Waziri ajue kuwa Lamu Mashariki ndio eneo bunge pekee Kenya ambalo halina hata inchi moja ya barabara ya lami. Eneo Bunge la Lamu Mashariki lina barabara tatu. Mojawapo ni barabara ya Mtangawanda- Kizingitini ambayo mnaijua. Ninaomba mtueleze mikakati ya ujenzi wa barabara hiyo imefikia wapi angalau tuwe na barabara ya lami. Barabara ya pili ni ya ... view
  • 13 Nov 2024 in National Assembly: Mhe. Spika, Lamu Mashariki ina mazingira tofauti. Maeneo yetu sio yale wanabara mnaita landmass . Kwetu ni watermass . Tunahitaji seawalls, yaani zile kuta za bahari. Kuna kijiji kinachoitwa Bwajumwali ambacho karibu kibebwe na maji. Watoto pia wanabebwa na maji. Kijiji hicho kilijengwa kikiwa kidogo. view
  • 13 Nov 2024 in National Assembly: hakumaliza ujenzi na akakimbia. Mambo hayo pia yako katika Ministry yako. Kwa hivyo, tafadhali yaangalie. Ahsante, Mhe. Spika. view
  • 17 Oct 2024 in National Assembly: Asante, Mhe. Spika. Tuajua kwamba view
  • 17 Oct 2024 in National Assembly: zina madhara na sheria ya kuzipinga ilipitishwa hapa. Sijui kama watu wanaona kuwa kule kwangu ni karibu na Somalia kwa hivyo wameamua kutuwachia asbestos. Kuna nyumba za hospitali kule Kizingitini na wanaoishi pale ni madaktari. Nyumba zote hizo ziko na asbestos kwenye paa. Kingine cha kusikitisha ni kwamba contractor aliyepewa kandarasi ya kuotoa asbestos kwenye paa za nyumba katika hospitali ya Kiunga alizitoa. Nina uhakika kwamba BQ ya kandarasi hiyo inaonyesha mahali anapofaa kuhifadhi hiyo asbestos. Jambo la kushangaza ni kwamba mwanakandasi huyo aliwapatia wananchi wa Kiunga asbestos hiyo na hivi ziko kwenye private houses badala ya kuzizika pahali au ... view
  • 17 Oct 2024 in National Assembly: aliziwacha hizi asbestos pale Kiunga. Wananchi wamezichukua na kutengeneze maboma. Ni hatari sana. Ninaomba wahusika wahakikishe kwamba hilo jambo limerekebishwa kabla halijaleta madhara. Tumeambiwa kwamba asbestos husababisha cancer . Unatarajia watu wangu wa Kiunga wapate hiyo shida ilihali wenyewe ni maskini wa roho zao? view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus