9 Oct 2024 in National Assembly:
Ahsante Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi nichangie Mswada huu kuhusu Maktaba ya Kitaifa. Mwanzo, ninaipongeza Kamati kupitia kwa Mwenyekiti wake, Mhe. Wanyama. Wamefanya jambo la maana kwa sababu sheria hii ilikuwepo kabla ya ugatuzi. Hivyo, kulikuwa na haja kubwa ya kuweka hii sheria baada ya mwaka wa 2010 kuhusu mambo ya ugatuzi. Kwa hivyo, ilikuwa muhimu sana afanye hivyo. Sheria inasema kuwa, kuna haja ya kuwa na maktaba angalau katika makao makuu ya kaunti, lakini kuna kaunti zingine kama Lamu ambazo hazina maktaba hata moja. Hii sheria ikitungwa, ningependa Kamati izingatie kuwa kaunti zingine ambazo hazina maktaba hata ...
view
9 Oct 2024 in National Assembly:
Kwa mfano, pale Lamu Town kuna sheria kwamba huwezi kujenga nyumba iliyo zaidi ya gorofa tatu karibu na bahari. Lakini utaona mtu akikandamizwa na sheria hii. Lazima tutumie utamaduni huu kwa sababu ya makavazi na historical sites . Naomba hii Kamati hata kama Mwenyekiti hayuko hapa, wazingatie sehemu ile ndiyo wapate fidia fulani ili wazidi kuhifadhi na kuweka kumbukumbu vizuri. Maanake maktaba na
view
9 Oct 2024 in National Assembly:
hizo ni kumbukumbu. Zimewekwa na kaunti na hazishughulikiwi. Ukiangalia LamuFort, hakuna maktaba ya kumbukumbu ya kisawasawa ambayo mtu anaweza akasoma. Ile maktaba yao ina kumbukumbu ndogo ya kueleza kitu fulani kimetoka wapi. Kwa hivyo, naona ni mwanzo mzuri na tunaunga mkono hii Kamati. Lakina, ina kazi nyingi ya kufanya na kwa hivyo, wahusishe mambo yote ambayo tunasema. Ahsante sana.
view
8 Oct 2024 in National Assembly:
Asante, Mhe. Spika. Umoja wa taifa ni muhimu sana. Naibu wa Rais haleti umoja. Nataka ieleweke kwamba watu wa mlima wanaishi sehemu zingine. Kule kwangu, Kiunga, niko na watu wa mlima. Kile wanachoona zaidi ni sanddunes . Hawaoni mlima. Wanaona bahari. Naibu wa Rais alizungumzia kuhusu National Intelligence Service (NIS) ambayo ilikuwa grave mistake . Alikosea sana. Afadhali angetaja Noordin kama ako na shida naye kuliko taasisi ya Huduma ya Ujasusi ya Kitaifa. Inatufanya tukae dhaifu mbele ya maadui zetu. Kwa mfano, Al-Shabaab watatuona vipi kama tuko wadhaifu? Kwa mtu yeyote, haswa mwanaume anayetukana mwanamke, kila mtu aliyeumbwa ana shimo ...
view
2 Oct 2024 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Spika. Nampongeza Mheshimiwa kwa kuleta swala hili la mihadarati hapa Bungeni. Kusema kweli, hili swala linatuathiri sana. Kabla sijaendelea kuchangia, nataka Mheshimiwa achukue tahadhari. Mimi nilitaja majina ya wanaohusika na uuzaji wa madawa ya kulevya katika eneo bunge langu na hiyo ilikuwa mwanzo wa maisha yangu kubadilika. Ilikuwa katika Bunge la 12 ambapo nilikasirika na nikataja majina ya wahalifu hao. Baada ya kutaja majina yao, maisha yangu yalibadilika na ilinibidi niwe nikitembea na askari kila mahali. Niliongezewa askari waliokuwa wakinilinda. Nashukuru Bunge hili kwa sababu lilinisaidia sana. Hii shida ipo na ukiizungumzia, wewe ndio unaonekana mbaya. Wale wanaouza ...
view
2 Oct 2024 in National Assembly:
kwa sababu wako karibu na mpaka na wakitumika vibaya, wanaweza kuhatarisha nchi yetu. Kama Waziri anakuja mbele ya Kamati, ningetaka nije ili nichangie swala hili. Naomba
view
2 Oct 2024 in National Assembly:
niwe friend of that Committee . Tunajua majina yao. Katika eneo bunge langu, ukimuuliza mtoto akupeleke kwa yule anayeuza mihadarati, ataweza kukuonyesha. Sitataja majina yao kwa sababu nitajipata kwa shida tena. Yale yaliyonipata yalinifanya nikaogopa. Utaona mtoto ameumia na anatoa usaha lakini ukimpa Ksh200, anaenda kununua mihadarati badala ya aende hospitalini. Hilo tatizo linatuathiri sana. Tukiliacha liendelee zaidi, litatuathiri zaidi. Angalau mmeanza kuongea kuhusu sehemu nyingine lakini sehemu ya Coast The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
2 Oct 2024 in National Assembly:
ndiyo imeathirika zaidi. Hapo awali, mihadarati ilikuwa janga la eneo la Coast pekee yake. Lakini sasa, cocaine imekuwa janga la Kenya nzima. Kule Lamu East, shida si cocaine pekee yake. Kuna tembe zinazoitwa karambela . Nimezizungumzia mpaka katika security meetings. Nimeambiwa nizilete ili wazione kwa sababu hawazijui. Mwishowe, waliniambia walizipata. Karambela inauzwa kwa Ksh20. Mtu akizikula, anageuka na kuwa kama wild animal . Anaweza kufanya chochote. Zinauzwa na hakuna hatua inayochukuliwa. Ukimtuma mtu azinunue, atapelekwa mpaka mahali zinazouzwa. Hakuna mtu ambaye hajui wanaoziuza. Shida ni kuwa hawachukui hatua yoyote kuwakomesha. Ahsante, Mhe. Spika.
view
2 Oct 2024 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ya kumuuliza Waziri maswali. Mwanzo, ninachukua nafasi hii kumpongeza Waziri. Kusema kweli, tumekukosa hapa Bungeni. Tulikuwa tumezoea kuisikia sauti yako sana. Tumekumbuka sauti yako wakati ulipokuja. Nilipopata nafasi hii, nilijiuliza ni jinsi gani huyu mfugaji wa mifugo atawiana na mazingira. Lakini nimeona umekuwa bingwa wa kuhifadhi mazingira, kiasi kwamba ukiyazungumzia, maneno yako yanatoka rohoni kabisa. Kushughulikia mazingira kumekufanya uyapende. Ninaona ushaingiliana huko vizuri. Pongezi kwa hayo. Niliuliza swali kuhusu eneo la Siu. Kampuni ya Zarara ilijaribu kuchimba gesi lakini gesi hiyo haikupatikana. Hawakufunga kile kisima walichokichimba vizuri kwa hivyo kuna moshi ...
view
26 Sep 2024 in National Assembly:
Yes, I can.
view