2 Oct 2024 in National Assembly:
ndiyo imeathirika zaidi. Hapo awali, mihadarati ilikuwa janga la eneo la Coast pekee yake. Lakini sasa, cocaine imekuwa janga la Kenya nzima. Kule Lamu East, shida si cocaine pekee yake. Kuna tembe zinazoitwa karambela . Nimezizungumzia mpaka katika security meetings. Nimeambiwa nizilete ili wazione kwa sababu hawazijui. Mwishowe, waliniambia walizipata. Karambela inauzwa kwa Ksh20. Mtu akizikula, anageuka na kuwa kama wild animal . Anaweza kufanya chochote. Zinauzwa na hakuna hatua inayochukuliwa. Ukimtuma mtu azinunue, atapelekwa mpaka mahali zinazouzwa. Hakuna mtu ambaye hajui wanaoziuza. Shida ni kuwa hawachukui hatua yoyote kuwakomesha. Ahsante, Mhe. Spika.
view
2 Oct 2024 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ya kumuuliza Waziri maswali. Mwanzo, ninachukua nafasi hii kumpongeza Waziri. Kusema kweli, tumekukosa hapa Bungeni. Tulikuwa tumezoea kuisikia sauti yako sana. Tumekumbuka sauti yako wakati ulipokuja. Nilipopata nafasi hii, nilijiuliza ni jinsi gani huyu mfugaji wa mifugo atawiana na mazingira. Lakini nimeona umekuwa bingwa wa kuhifadhi mazingira, kiasi kwamba ukiyazungumzia, maneno yako yanatoka rohoni kabisa. Kushughulikia mazingira kumekufanya uyapende. Ninaona ushaingiliana huko vizuri. Pongezi kwa hayo. Niliuliza swali kuhusu eneo la Siu. Kampuni ya Zarara ilijaribu kuchimba gesi lakini gesi hiyo haikupatikana. Hawakufunga kile kisima walichokichimba vizuri kwa hivyo kuna moshi ...
view
26 Sep 2024 in National Assembly:
Yes, I can.
view
26 Sep 2024 in National Assembly:
Mhe. Spika, haya mambo yanayoongelewa hapa si ya kweli. Dadangu Mhe. Muthoni amekuja hapa Bungeni kwa sababu hatujahusishwa. Hakuna kiongozi yeyote aliyeitwa, wala hakuna aliyepinga. Asiseme eti political leaders . Mimi sijawahi kuitwa, wala Mhe. Muthama au Mhe. Muthoni. Hao viongozi wengine ni akina nani, ilhali Kaunti ya Lamu iko na Constituency mbili na Women Representative mmoja peke yake? Hatujawahi kuitwa. Huo ni uongo. Jambo la pili ni kuwa kuna kigezo hapo…
view
26 Sep 2024 in National Assembly:
Mhe. Spika, sasa niseme nini badala yake? Kwa sababu sio ukweli huo.
view
26 Sep 2024 in National Assembly:
Well guided, Hon. Speaker. Jambo jingine linalotumika Lamu ni kwamba ukiuliza kama pengine kuna uzembe mahali, wanasema ni
view
26 Sep 2024 in National Assembly:
. Hakuna utovu wa usalama Lamu. Tunaishi na kuenda popote tunapotaka. Hapo Hindi, watu ni wengi na miradi pia ni mingi, kama vile LAPSSET. Utovu wa usalama unatokea wapi sasa? Wamekosa kusema ukweli, na badala yake kutumia kigezo cha utovu wa usalama. Ardhi, sijui kama ni hii ya Swahili Scheme, kwa sababu imeleta utata. Kila gavana akiingia analeta sheria zake, na mambo yasipoenda, anasonga hapo hapo; lakini sio kwamba ni Memberof Parliament au political leaders . Ningeomba huyo Waziri aje ajibu au nilitengeneze swali hili kivingine. Niambieni ni vipi nitafanya. Kwa sasa ni kama tu kumgombeza Mwenyekiti bure, naye hajui ...
view
25 Sep 2024 in National Assembly:
Ahsante. Waziri, mwanzo, ningependa kukupongeza na kukushukuru wakati ulikuwa Waziri wa Barabara, Usafiri na Kazi za Umma. Ulijua Lamu Mashariki haina barabara na ukafanya mipango mizuri. Ahsante. Saa hii pia, ningependa ufikirie kuhusu Lamu Mashariki katika upande wa michezo. Hakika kwa miaka kadhaa au tangu uhuru upatikane, hakuna kitu kimefanywa katika Eneo Bunge la Lamu Mashariki katika upande wa michezo. Nimesikia mipango yote ambayo umezungumzia. Kaunti ya Lamu haina uwanja wa Serikali ya Kitaifa wala ya kaunti. Katika mipangilio yote, sisi tunaachwa nyuma. Nakuomba kwa hisani yako kama unaweza kutaja kitu kimoja ambacho kimefanywa Lamu Mashariki na hii Wizara. Niambie ...
view
24 Sep 2024 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii nami nipate kuzungumza kuhusu NG-CDF. Katika maeneo bunge mengi, pesa za NG-CDF ndizo pesa pekee tunazotarajia kufanyia maendeleo. Eneo Bunge la Lamu Mashariki na maeneo bunge mengine mengi yamebaguliwa kwenye mipango ya maendeleo. Kwa mfano, tukiangalia rekodi, tutaona kwamba kwenye Bajeti ya mwaka uliopita, Eneo Bunge la Lamu Mashariki lilipewa Ksh4 milioni, ilhali kuna eneo bunge lingine ambalo lilipewa Ksh450 milioni. Pesa za NG-CDF ndizo pesa pekee ambazo hazihusishwi na ubabe kwa sababu kila eneo bunge linapata mgao wake na linajipangia miradi yake kulingana na jinsi sheria inavyosema. Katika Serikali kuu, pesa ...
view
24 Sep 2024 in National Assembly:
tunaelekezwa wapi. Ninavyozungumza, Rais ametusaidia. Kule kwetu, viwango vya elimu viko chini sana, na madhara kwetu yameonekana. Vijana wameonekana wakienda wanavyokwenda ikabidi tuwasomeshe. Tukapewa nafasi ya kuajiri walimu lakini miongoni mwa walioajiriwa, ni waalimu wawili peke yake kutoka katika Lamu Mashariki. Hazina ya NG-CDF ilikuwa inatuokoa…
view