Shariff Athman Ali

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 81 to 90 of 458.

  • 29 Feb 2024 in National Assembly: Asante sana, Mheshimiwa Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili nikaribishe wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mt. Kenya, Parklands Law Campus. Wamekuja na kiongozi wao, Bw. Swabir, ambaye ni mwanafunzi kutoka Lamu Mashariki. Watu wanasema watu wa eneo la Lamu Mashariki hawasomi. Hata hivyo, watu wamesoma, ingawa si wengi. Ninachukua nafasi hii niwaambie wanafunzi wa Lamu Mashariki kwamba watu wamekuwa wakisema anga ndio kikomo, lakini saa hii wanasema anga sio kikomo. Nafasi zipo. Wakitaka kusoma, wasome. Saa hii kuna bursary na wafadhili wengi. Kuna wafadhili wengi ambao husaidia wanaosoma sheria au udaktari. Vilevile, ninachukua nafasi hii niwakaribishe wanafunzi hawa ... view
  • 28 Feb 2024 in National Assembly: Hon. Deputy Speaker, I beg to give notice of the following Motion. THAT, aware that Article 239 provides for the National Security Organs, including the Kenya Defence Forces; further aware that, the Kenya Defence and Kenya Special Forces play an indispensable role in promoting and safeguarding national security in accordance with the Constitution; recognising that members of the Forces face life-threating risks as they carry out their duties to protect our citizens, particularly in high-risk and volatile areas; noting that there is currently no token of appreciation for the remarkable dedication, service and sacrifices made by the Kenya Defence and ... view
  • 28 Feb 2024 in National Assembly: Asante, Mhe. Naibu Spika, kwa kunipatia nafasi ya kuchangia Mswada huu. Ninaunga mkono moja kwa moja. Ninamshukuru Mhe. Mejjadonk Benjamin kwa kuleta Mswada huu. Ninaunga mkono wafanyakazi wa serikali wote wastaafu wakiwa na miaka 60. Sasa, Waziri ama wakubwa wa Serikali wana haki ya kuongeza wafanyakazi mwaka mmoja, miwili mpaka miaka mitano. Hii inadhulumu wengine. view
  • 28 Feb 2024 in National Assembly: Watu wangu wa Msitu wa Boni, Kiunga, Faza Ward na Mtangawanda ambao hawajui watu wakubwa serikalini hawapati nafasi hizi. Kwa hivyo, huu Mswada ukipitishwa, itakuwa haki. Kama mwalimu wa kule Kiunga anastaafu akifikisha miaka 60, wale wa huku wanaojua watu wakubwa Serikalini wastaafu wakifikisha miaka 60 pia. Lakini, sio kwa kuwa anajua mtu, basi yeye ndio anaongezewa miaka. Ninaunga mkono sana Mswada huu. Wakenya wote wastaafu wakifikisha miaka 60. view
  • 28 Feb 2024 in National Assembly: Pia, ninaunga mkono vile Mhe. alivyosema hapa kwamba matayarisho yafanywe mapema kwa sababu inachukuliwa kama kigezo ili mwingine aendelee kufanya kazi na kusema hakuna mwingine anawezakufanya taaluma yake. Ni vizuri vile ilivyosemwa kwamba kabla yule mwenye taaluma ile hajaondoka, mwingine atayarishwe achukue hiyo nafasi yake. Isiwe kiegezo cha kukosesha wengine kazi kwa kumpendelea mtu mwingine. Pia, ninaunga mkono pale anaposema wale makatibu washikilizi wasifanye zaidi ya miezi sita. Kusema kweli, tunapoteza sana kwa sababu wakikaa pale, utaona katibu amekuja kazini hata hana morali kwa sababu hajui kesho kutakuwa vipi. Katibu ajue akienda sana ni miezi sita. Aandikwe au atolewe. Kwa ... view
  • 28 Feb 2024 in National Assembly: hivyo watu wasishtuke wakidhani kuwa ni kwa watu wote Kenya. Kuna wale wengine hawapitii huku. Wao wataendelea na zile sheria zao. view
  • 28 Feb 2024 in National Assembly: Ahsante, Mhe. Naibu Spika. view
  • 14 Feb 2024 in National Assembly: Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie. Kwanza, ningependa kumpongeza Mbunge Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Nairobi, Mhe. Esther Passaris, kwa kuleta Hoja hii. Pia, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa katika Eneo Bunge langu la Lamu Mashariki, hakujawahi kutokea mauaji kama haya ya kinyama. Wanaume wetu ni wastaarabu; hawaui wanawake. Nachukua nafasi hii kuwapongeza wanaume wote wa Lamu Mashariki. Ni kweli Lamu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor view
  • 14 Feb 2024 in National Assembly: Mashariki inakumbwa na shida nyingi sana, lakini, alhamdulilahi, tunashukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa kwetu hatujashuhudia mauaji ya wanawake. Hivi leo tunalia na Wakenya wengine. Si sawa wanawake kuuawa. Pia si sawa sisi kulaumu tu Serikali. Kwa maoni yangu, tunazo sheria nyingi kuhusu jambo hili, lakini hazitumiki. Jambo ambalo nataka kutilia mkazo sana ni namba ile ya dharura ya 1195. Wakenya wengi hawajui kuwa kuna namba ya dharura inayoshughulikia maswala haya. Namba hii hutumika masaa 24, na pia inapigwa bila malipo. Unapopatikana na tatizo lolote kama la ubakaji, ukipiga namba hii, unapata nusra na watu wa kukusaidia hata kama ni kwa ... view
  • 7 Dec 2023 in National Assembly: Asante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi ili nichangie Hoja hii. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus