Shariff Athman Ali

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 91 to 100 of 512.

  • 7 Aug 2024 in National Assembly: barabara hiyo haipitiki. Pesa ya barabara hiyo iko na nimefuatilia na kwa sasa, tumepata imani na Serikali hii. Kama mkandarasi hawezi kuitengeneza barabara hiyo, basi ashirikiane na mkandarasi wa ndani ili wamalize kwa sababu Ksh1,000,000,000 iko. Ifanyiwe kazi ndiyo watu waweze kupata huduma kwa urahisi. Kwa sasa, kwa vile barabara haijapelekwa mashinani, ukitaka kufika King Fahd mpaka utumie Ksh7500. Kwa hivyo, huduma ya barabara ikiwekwa, hizi adhabu nyingi za kufikiria zitapungua. Kiunga iko karibu na mpaka wa Somalia na imekatwa na mambo mengi. Ukitaka pasipoti, kitambulisho au cheti cha good conduct, mpaka ulipe Ksh8000 kwenda Mji wa Lamu. Hiyo ndiyo ... view
  • 7 Aug 2024 in National Assembly: Asante sana. Katika Bunge lote, mimi ndiye Mbajuni peke yake. Ninawakilisha Bajuni wote walioko Kenya nzima. Mimi ninatafuta marafiki kutoka kila kabila. Mimi sina ukabila kwa sababu lazima nitafute kila mtu. Sina mwenzangu hapa. Hakuna mtu anayezungumza lugha yangu. Ukitaka kufika Kiwayu, ni lazima uende kwa maji kwa jisaji moja na dakika thelathini. Huduma ziwe ni hizo matatizo. view
  • 7 Aug 2024 in National Assembly: Mkokoni iko ndani ya msitu. Saa hii ndio tunapambana. Mkiona tunalia hapa, mjue kwamba mambo kule ni tofauti. Katika eneo bunge nzima, barabara ambayo imejengwa kwa sasa ni ile ambayo imefanywa na Kenya Rural Roads Authority (KeRRA). Na ndio maana wakati mwingine, hatutaki mtu aitaje KeRRA. Hizi zote zinachangia mawazo mengi na ni muhimu sisi sote tufikirie kama Wakenya. Vile unafikiria kwako inakufaa, kwa mwenzako ni tofauti. Mimi nikisema kuwa ninataka polisi nikienda kwangu, mtu atashangaa sana. Kutoka Mkokoni mpaka Kiunga, ni lazima nipewe gari nzima la polisi kwa sababu ninapitia Boni Forest. Nilipokuwa Mwakilishi wa Wanawake, pesa nyingi ilikuwa ... view
  • 31 Jul 2024 in National Assembly: Mhe. Spika, mimi sijaridhika. Badala ya Mwenyekiti kutumia aya nyingi na sentensi nyingi, kurasa kwa kurasa, nilitaka aniambie kwa sentensi moja kwamba stima inarudi Kiunga lini. Leo ni siku mia moja na tisa, miezi mitatu na zaidi, Kiunga hakuna stima. Na shida ni kuwa generator imeharibika. Kwani Kenya Power ni maskini sana hawawezi kukomboa meli kutoka Mombasa kupeleka generator ? Unaniambia view
  • 31 Jul 2024 in National Assembly: iko Mokowe na haijafika. Watu wenye kisukari wanapata shida. Hakuna insulin . Nataka uniambie siku gani stima itawaka Kiunga. Nakupatia wiki mbili, kama haziwaki nitaenda kulala kwenye hiyo stesheni mpaka siku ile mtawasha stima. Asante. view
  • 31 Jul 2024 in National Assembly: Mhe. Spika, generator iko Mokowe. Kuna view
  • 31 Jul 2024 in National Assembly: mbili. Nimeenda kwa ofisi zote za Kenya Power. Generator moja ndogo ya Kenya Power iko Mokowe na generator nyingine ya contractor iko Mokowe. Shida yao wanatafuta maafisa wa Kenya Defence Forces (KDF) wazibebe. Nyinyi hamna pesa za kuzibeba kweli? Si hiyo ni biashara? Si watu watalipwa? view
  • 20 Jun 2024 in National Assembly: Asante, Mhe. Spika kwa fursa hii ili nichangie huu Mswada. Ninaunga mkono. view
  • 20 Jun 2024 in National Assembly: Niko na imani kuwa Eneo Bunge la Lamu Mashariki litaunganishwa na Wakenya wengine. Hivi sasa, tangu tupate Uhuru, Lamu Mashariki iko kivyake. Haijaunganishwa na Wakenya. Eneo Bunge lote hakuna hata njia moja ya lami wala grid ya kitaifa. Pesa zikipatikana, watu wangu wa Lamu Mashariki wataunganishwa na Wakenya wengine. Kuunganishwa kwa Maeneo Bunge itafanyika kwa sababu ya barabara na grid ya kitaifa. Lamu haijapata grid ya kitaifa wala barabara. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 20 Jun 2024 in National Assembly: Watu wa Lamu Mashariki tumekuwa tukitoa ushuru kama Wakenya wengine. Maeneo bunge mengine yameendelea. Nahisi tuzidi kutoa ushuru sana ndiyo nasi watu wa Lamu Mashariki tupate maendeleo. Ninaunga mkono kwa dhati nikiwa na imani kuwa Serikali hii ndiyo itatuunganisha sisi na Wakenya wengine. Lazima tuwe wavumilivu na tufikirie Wakenya wengine. Wengine wetu bado tuna hamu na maendeleo ambayo hatujapata. Nyinyi mlio mjini mna barabara na stima kila pahali. Mmeshiba. Kule kwetu sisi husema walioshiba samli wanatoa miba. Kwetu bado tuna njaa ya maendeleo. Hatuwezi kupinga pesa kupatikana. Toeni ushuru, wacheni mchezo. Kuna watu wanaumia. Ushuru ndiyo kuendelea kwa nchi. Sisi ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus