Shariff Athman Ali

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 101 to 110 of 458.

  • 7 Dec 2023 in National Assembly: Jambo hilo linatuogopesha. Lisije likatumika. Kwa mfano, ninasikitishwa sana na yale yanatendeka kule Lamu. Ndugu zetu waliokuja Lamu ni wenzetu, Kenya ni moja. Jamii hiyo imekuwa Lamu tangu tuwe wachanga na imekaa na wazee wetu vizuri bila chuki. Siasa zinapoanza, watu huuwawa. Wanapouwawa, hofu inaingia katika jamii. Unapowaambia waende kwa mashamba, wanasema wanaogopa kwa sababu wataonekana kule na kuitwa magaidi. Vijana hawajakuwa wakienda shambani; wanaenda baharini peke yake. view
  • 7 Dec 2023 in National Assembly: Jamii zingine zimehamia katika eneo hilo na kuendelea kuwa wengi hadi wakawa na kiburi na kusema kuwa watachukua viti vyote katika uchaguzi. Ninataka Serikali ichunguze suala la magaidi kwa sababu kuna mambo ambayo yamefanyika na watu wanajificha kwenye ugaidi. Kwa mfano, ningependa kuzungumzia jambo ambalo Wakenya hawalijui. Ningependa kulieleza hapa ili walijue. Kuna kanisa iliyochomwa, jambo ambalo lilileta vita kati ya Wakristo na Waislamu. Kuna watu ambao wanafaidika wanapowagombanisha Wabajuni au wakaazi wa Lamu na jamii zingine. Wanataka kuzidisha ugomvi wa kidini ili mtu ajinufaishe kisiasa. view

  • 7 Dec 2023 in National Assembly: Sisi watu wa Lamu tunapendana, na wale wanaoishi Lamu watakwambia hivyo. Kanisa lilipochomwa, uchunguzi ulifanywa na kubainika kuwa aliyelichoma ni Murithi Robert. Tukio hilo lilirekodiwa kwenye Occurrence Book (OB) Number 371/170/23. Mtu huyo alishikwa, akafunguliwa mashtaka na kufungwa miaka minane gerezani. Mbona mtu achome kanisa? Ili Wakristo waone kuwa Waislamu wamechoma kanisa, waende kuchoma msikiti ndio vita The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor view

  • 7 Dec 2023 in National Assembly: vianze, na Lamu iwe na mgawanyiko kati ya Waislamu na Wakristo. Mungu alitusaidia. Yule aliyechoma kanisa akashikwa. Kanisa mbili zilichomwa wakati mmoja. view

  • 7 Dec 2023 in National Assembly: Ninataka niwaelezee wenzangu jinsi mambo ya Lamu yanavyoendelea. Waziri Kindiki ni mchapa kazi na anajua kazi yake. Achunguze maneno yangu na kuangalia mambo ya Lamu. Kuna shida zaidi kule Lamu. Tulipokuwa wachanga, kulikuwa na Shifta War . Tulikuwa tunajua kuwa ni lazima tunyamaze tunapopita mahali fulani. Hatungeweza kuzungumza tukiwa kwenye basi. Sehemu hizo ndiko watu wanakoishi wakati huu, na Al Shabaab wanapatikana huko. view

  • 7 Dec 2023 in National Assembly: Ninajua kuwa Serikali ina uwezo wa kuchunguza na kufuatilia mambo haya. Wakati wa Shifta War, Wabajuni walioishi barani walifukuzwa wakiambiwa kuna vita. Ugaidi umebadilisha jina kule Lamu lakini mambo haya yapo na yamekuwa yakituathiri. Ni lazima tuhakikishe kwamba wanaotunga sheria hawazitumii kuwagandamiza watu wengine. Hatutaki Mkenya yeyote aumie. Tunataka aishi popote bora watu waheshimiane na wasitumie ugaidi. Wakati watu wanauana wenyewe kwa wenyewe, wasiseme ni ugaidi. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus