9 Mar 2016 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, bila ya kupoteza wakati, ninaunga mkono Mswada huu. Ninawaomba Wabunge wenzangu tuungane ili tuweze kurekebisha pale ambapo panahitaji kurekebishwa na tuuunge mkono Mswada huu.
view
9 Mar 2016 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, bila ya kupoteza wakati, ninaunga mkono Mswada huu. Ninawaomba Wabunge wenzangu tuungane ili tuweze kurekebisha pale ambapo panahitaji kurekebishwa na tuuunge mkono Mswada huu.
view
1 Jul 2015 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ya kuchangia Hoja hii. Vilevile ningependa kumpongeza Mheshimiwa ambaye ameleta Hoja hii baada ya kuzingatia pakubwa suala la afya katika nchi yetu. Kwa kweli hii ni Hoja ambayo inaonekana ni kama imeletwa Bungeni kama Hoja nyingine za kawaida, lakini ukweli ni kwamba suala la afya katika nchi hii limeachwa nyuma sana na limekuwa katika hali ya kutothaminiwa. Mjadala uliopo ni baina ya kauli mbili: Je, huduma hii ipatikane katika kaunti au katika maeneo Bunge? Kwa kweli ni jambo la kusikitisha. Hivi sasa huduma hii haiwezi kupatikana katika baadhi ya kaunti ...
view
1 Jul 2015 in National Assembly:
Wakenya wanaumia. Ni lazima iwapo tumekubaliana kupitisha mambo kama haya, ufuatilizaji na uwajibikaji ni lazima upatikane kwa sababu tunaweza kuyapitisha mambo haya lakini yakabaki vilevile kwamba hayana maana yoyote kama inavyosemwa na wenzangu. Inaonekana ni kama ndoto tunajaribu kupanga hivi sasa. Lakini ninaamini pakubwa hakuna jambo ambalo haliwezekani. Utapata kwamba, kwa mfano, hapa tulipo wakati mmoja palikuwa ni kiwanja tu. Waliofikiria kujenga Jumba hili walikuwa na mpango wakalijenga. Hivi sasa tukisema tutatoa huduma hizi sharti tuhakikishe kwamba kila mmoja amewajibika katika kulitekeleza jambo hili. Hivi sasa tumepeana majukumu ya afya kwa serikali za kaunti. Ingawa hivyo kuna malalamishi mengi.Ni kwa ...
view
1 Jul 2015 in National Assembly:
Ninaunga mkono Hoja hii. Lakini kubwa ambalo nataka tuangazie kama viongozi ni kuwajibika, kutekelza na kujua kwamba wananchi wa Kenya wanaumia popote walipo kwa ajili ya masuala ya afya. Asante.
view
25 Nov 2014 in National Assembly:
Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwa kweli swala hili kuzungumzia kwa dakika mbili hata sijui niache kuzungumza ama nizungumze vipi kwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
25 Nov 2014 in National Assembly:
sababu sisi ni miongoni mwa wale ambao tumeathirika pakubwa katika swala hili. Lakini pengine moja ama mawili ambayo nitazungumzia ni kwamba hivi sasa, nafikiri sote twafahamu ya kwamba hata wale wachezaji katika mpira wakiwa ni wazuri, lakini wanapofanya makosa, lawama zote zinaenda kwa coach . Hali halisi ilivyo katika Kenya yetu kwa maswala ya usalama, imekua ni swala ambalo lazungumzwa kila siku lakini halionekani kupata suluhisho. Ni vyema tukiwa kama viongozi, kama wajumbe, tulitafutie suluhisho jambo hili. Kwa kweli, tulitafutie suluhisho jambo hili. Iwapo tutaliacha kuendelea namna hivi na kulijadili ama kupeana lawama hapa na pale, hatutafika katika zile suluhisho ...
view
12 Aug 2014 in National Assembly:
Hon. Deputy Speaker, pursuant to Standing Order No.44(2)(c), I wish to request a Statement from the Chairperson of the Departmental Committee on Finance, Planning and Trade regarding the transfer of the Ministry of East African Community, Commerce and Tourism offices from Lamu Town in Lamu County to Malindi Town in Kilifi County.
view
6 Aug 2014 in National Assembly:
Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kupata maelezo kutoka kwa mwenyekiti wa kamati ya utawala na usalama wa kitaifa kuhusu mikakati ambayo Serikali imeweka kuzuia janga jingine kwa kuwa imesema kwamba tatizo hili, ama yale yaliyotokea Mpeketoni, lilitokana na Al Shabaab. Tukizingatia kwamba eneo la Ubunge la Lamu Mashariki linapakana na Somalia pale Kiunga, Serikali imeweka mikakati gani kuhakikisha mpaka ule wa Kiunga umekuwa na usalama? Hii ni kwa sababu tunadhani kwamba Al-Shabaab wanatoka Somalia. Mpaka ule wa Kiunga hivi sasa uko hali gani ya kiusalama? Usalama uko Mpeketoni pekee kwa sababu ya yale yaliyotokea ama Serikali imeweka ...
view
10 Jun 2014 in National Assembly:
Thank you, hon. Speaker. I wish to request for a Statement from the Chairperson of the Departmental Committee on Defence and Foreign Relations with regard to the Kiunga-Somalia Border. Hon. Speaker, the Operation Linda Nchi that was initiated more than two years ago led to the closure of the Kiunga-Somalia Border, which has still not been re-opened and has affected the economy of the people. It has also been observed that the other The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view