Shariff Athman Ali

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 451 to 460 of 515.

  • 7 Jun 2016 in National Assembly: Kwa hivyo, ningeomba Serikali ihakikishe kwamba tumefanya mambo ambayo yatawaridhisha wananchi na kuinua nchi hii ili tuweze kuimarisha chumi wetu. Tusifanye haya kwa sababu ya ubinafsi wa watu ama maslahi ya watu fulani katika nchi hii. view
  • 7 Jun 2016 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. view
  • 10 Mar 2016 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua fursa hii nikiwa mmoja wa wanakamati wa Kamati ya Ardhi, kuzungumza kuhusu Mswada huu wa swala nzima la ardhi ambalo limeletwa hapa Bungeni. Ningependa kuipongeza Kamati kwa juhudi zake na yale ambayo wameweza kufanya mpaka kufikisha huu Mswada hapa. Utakubaliana nami ya kwamba swala la ardhi nchini ni nyeti na halihitaji kujadiliwa kiufupi ama kwa namna isio sawa. Hivi sasa Wakenya wengi wana hamu kubwa kujua swala hili limekuwa na mwelekeo upi katika nchi yetu ya Kenya. Tukiangazia pakubwa, Wakenya walipigia Katiba kura na wakaweka Tume ya Ardhi ili kutatua na ... view
  • 10 Mar 2016 in National Assembly: Bunge linapopitisha masuala kama haya, linatatua matatizo ambayo yapo. Matatizo haya yapo na hayajatatuliwa hususan tukizungumzia Pwani. Mbali na hayo, walikuwa na imani kubwa katika Tume ya Kitaifa ya Ardhi. Mpaka wakati huu, Tume hii bado haijatatua matatizo kwa kisingizio kuwa Wizara ya Ardhi haijawapa mamlaka kamili au inawanyima haki yao ya kufanya kazi. Ikiwa kisingizio hicho kitaendelea kwa namna hii, ina maana kuwa yale malengo ya Wakenya kuipigia Katiba kura yatakuwa hayajapatikana. Tukizingatia muda ambao umepita tangu Wakenya waipigie Katiba kura mpaka leo ambapo Mswada huu umefika Bungeni ili tujadili jinsi tutawasaidia Wakenya kama viongozi na wawakilishi wa kila ... view
  • 9 Mar 2016 in National Assembly: Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuandamana na wenzangu kuunga mkono huu Mswada ambao uko mbele yetu leo. Jambo muhimu ambalo nataka tujiulize ni kwamba umuhimu wa huu Mswada ni nini katika nchi yetu ya Kenya? Ni yapi ambayo tumeweza kuyafaidi ama tumeyaona katika nchi yetu ya Kenya kuhusiana na Mswada huu? view
  • 9 Mar 2016 in National Assembly: Kwa kweli kumekuwa na tatizo kubwa katika suala la umeme katika nchi yetu. Tunajua vizuri kwamba kampuni ya Kenya Power and Lighting Company ndiyo iliyokuwa ikishughulika sana na suala hili na wao ndio washikadao katika suala la kusambaza umeme katika nchi yetu ya Kenya. Wachache ndio walikuwa wakipata huduma hii na wengi hawakuwa wakiipata. Kumekuwa na matatizo makubwa sana kwa sababu ukilinganisha na matumizi, utaona kwamba malipo ya huduma hiyo yako juu. Kutokana na hali hii, kumekuwa na utata mkubwa lakini nimeshukuru pakubwa kwamba jambo hili limeweza kusambazwa kwa njia nyingine kiasi kwamba kumekuwa na mashirika mengine ambayo yanasambaza umeme. view

  • 9 Mar 2016 in National Assembly: Jambo ambalo tunahitaji kulizingatia ni kwamba ni lazima kuwe na mwelekeo wa kupunguza umaskini katika nchi yetu. Naamini kwamba umeme utakapokuwepo, viwanda vingi ambavyo vinatumia umeme vitalipa pesa kidogo ili bidhaa kutoka kwa viwanda hivyo ziweze kuuzwa kwa bei nafuu na wananchi wapate huduma ambazo zitawasaidia kujitoa kutoka kwa umaskini. Bidhaa nyingi hivi sasa zimekuwa na bei ya juu kwa sababu zinatumia umeme ambao ni wa bei ya juu sana. Hayo ndiyo matarajio makubwa ambayo tunahitaji kuwa nayo tunapolizingatia suala hili. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus